kura zilivopigwa kumchagua Mchezaji Bora wa Dunia #TheBest FIFA Men’s Player 2019 •

Namna kura zilivopigwa kumchagua Mchezaji Bora wa Dunia upande wa wanaume: #TheBest FIFA Men’s Player 2019

☆Kura za Wandishi wa habari za michezo
Messi: 364
Virgil Van Dijik: 462
Ronaldo: 264

☆Kura za Makocha Timu za Taifa:
Messi 379
VVD 289
Ronaldo 307

☆Kura za Manahodha Timu za Taifa:
Messi 377
VVD 337
Ronaldo 330

☆Kura za mashabiki:
Messi 1,359,728
VVD 704,235
Ronaldo 962,919

YANGA YAIFUATA ZESCO KWA MAFUNGU

Kikosi cha Yanga leo kitaondoka mafungu mawili kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Zesco United utakaopigwa Septemba 28.

Kikosi cha kwanza kitaondoka saa 6 mchana na kingine kitaondoka saa 12 jioni huku wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo, Rogers Gumbo amesema kikosi kitafikia Lusaka na keshokutwa Alhamisi kitaelekea Ndola ambapo mechi hiyo ndipo itafanyika. “Kikosi kitaondoka leo mafungu mawili, wengine wataondoka saa 6 mchana wa cha pili kitaondoka saa 12 jioni na tutafikia Lusaka kabla ya kuelekea Ndola siku ya Alhamisi,” alisema Gumbo.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika hapa jijini Dar es Salaam timu hizo zilitoka sare ya bao moja hivyo ili kutinga hatua ya makundi Yanga itapaswa kushinda au kupata sare ya kuanzia mabao mawili.

@yangasc
#wapendasokaupdates

Singida United yaachana na kocha Mkuu, Fredi Felix Minziro

OFFICIAL | Klabu ya Singida United imeachana na kocha wao Mkuu, Fredi Felix Minziro Baada ya game tatu TU za Ligi Kuu Tanzania BARA, Vipigo viwili na Sare Moja… Lakini Sio Matokeo kilicho muondoa klabuni hapo Ni uongozi wa klabu hiyo kutojali mambo ya msingi ikiwemo kumzungusha kuhusu mkataba wa kazi… Inasemekana walimletea mkataba lakini haukuwa maslahi mazuri ndio kuamua kujiweka kando.

– Sababu nyingine inayotajwa kumuondoa Minzirokwenye timu hiyo ni kitendo cha uongozi kujichukulia uamuzi wa kufanya usajili wa wachezaji bila kumshirikisha… Ikumbukwe Minziro ndiye kocha aliyeipandisha Ligi Kuu timu hiyo kabla ya kutimuliwa na mikoba yake kuchukuliwa na Kocha Mholanzi Hans Van Der Pluijm..
#VPLUpdates🇹🇿 #Updates
@Harunlugoyah

Kikosi cha Mbao Fc chawasili Mjini Singida

Kikosi cha Mbao Fc kimewasili salama Mjini Singida ambapo hapo kesho Jumatano 25 Sept 2019 kitacheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom-Tanzania Bara dhidi ya Singida Utd.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza wa ugenini msimu huu baada ya klabi hiyo kucheza mechi tatu za nyumbani huku ikishinda mchezo mmoja,kupoteza mchezo mmoja na kutoa sare mchezo mmoja.

IDD SULEIMAN “NADO” STAR ALIYEACHA MIGUU YAKE IZUNGUMZE

IDD SULEIMAN “NADO” STAR ALIYEACHA MIGUU YAKE IZUNGUMZE.. Na @octa_ayubu_jr
:
Niliwahi kuifuatilia historia ya Gabriel Jesus kwa ufupi nikajifunza maisha sio magumu ila sisi ndio wagumu.Uvumilivu ndio changamoto kwa watanzania wengi,wengi tunakatishwa tamaa na maneno na tunakubali hatuwezi.
:
Idd Suleiman “Nado” hili ni zao la ndondo cup,Moses kitandu,Yusuph mhilu na Joseph kimwaga hawa ni miongoni mwa wachezaji waliokulia katika academy bora,lakini wanazidi kusahaulika huku zao la ndondo cup likionyesha mwanga wa kufika mbali zaidi yao.
:
Nado ni mchezaji mzuri,anayejitambua nini anakifanya.Sijapata bahati ya kuona interview yake licha ya kiwango bora anachokionyesha akiwa na Azam na Taifa stars.Badala yake nimeshashuhudia interview ya Abdulaziz makame ambaye kacheza mechi moja tu ya mashindano makubwa.Waandishi wetu hawamuoni au nini kinatazamwa zaidi?
:
Media zetu zinaweza kukunyanyua na kukupoteza pia.Wachezaji wachache waliojitambua mapema media zimewasaidia ila wengi zimewapoteza na kuwafanya walidhike na kuona kama wamefika mwisho wa ubora wao.
:
Nado ni miongoni wachezaji wanaoweza kulibeba taifa letu kwa baadae,kama ataendelea kujitambua.Movement zake nyingi zinakuonyesha jinsi gani ni mchezaji mzuri,mapungufu yake ni madogo ambayo yanarekebishika hususani kwenye maamzi ya kupiga au kutoa pasi kwa wengine ndipo amekuwa mzito.
:
Goli 5 alizozifunga kwenye ndondo cup zilimpa mkataba kwenye TPL,akatua kwa wagonga nyundo wa mbeya,Mbeya city.Magoli yasiyozidi 15 aliyofunga ndani ya misimu miwili akiwa na mbeya city Yamempa mkataba chamazi.Huku miongoni mwa magoli hayo moja aliwafunga Yanga.Goli lilomshawishi Nsajigwa ageuke refa na kuanza kuhesabu wa mbeya city.
:
Licha ya maisha magumu aliyopitia mbeya city Sijawahi kusikia kagomea mazoezi au mechi,labda mazingira aliyopitia yalimshawishi ajitume bila kuangalia changamoto na sasa anakula matunda ya jasho lake.Inaendelea
Tags @iddy_nado7
@azamfcofficial

Virgil van Dijk….siwezi kufananishwa na messi

✍️ Beki wa Liverpool, Virgil van Dijk amesisitiza kwamba hawezi kufananishwa na Lionel Messi, Pia Beki huyo wa Kimataifa wa Uholanzi alisema kwamba hajakatishwa tamaa kutopata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa FIFA kwa Upande wa Wanaume.

✍️ Van Dijk alimaliza wa pili nyuma ya Mshambuliaji wa FC Barcelona, Lionel Messi aliyeibuka Mshindi Katika utoaji wa Tuzo hizo jana Jumatatu, huku Nafasi ya tatu alikamata Mshambuliaji wa Juventus na Ureno, Cristiano Ronaldo.

🗣 “Watu waliopiga kura wamefanya uamuzi na ni lazima ukubali,” Van Dijk aliwaambia waandishi wa habari… “Ndivyo ilivyo na kama wachezaji huwezi kunilinganisha na Messi kwa sababu yeye ni tofauti kabisa.. Alisema Van Dijk.
..
✍️ Mbali na kuisaidia Klabu yake ya Liverpool kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita mbele ya Tottenham Katika Fainali, Van Dijk aliiongoza nchi yake kwenye fainali ya kwanza ya UEFA Nations League, ambapo walipoteza mbele ya Ureno… Van Dijk aliyetajwa katika Kikosi Bora Cha Dunia “FIFA World XI” Alisema “Nimefurahia sana kuwa hapa, kuwa sehemu ya timu ya mwaka huu, baada ya bidii na kazi kubwa tuliyoifanya mwaka jana, lakino leo, kwa bahati mbaya, sikuweza kushinda Tuzo, lakini sijakata tamaa.”.
#TheBestAwards #FIFAAwards
@Harunlugoyah

BAADA YA MECHI MOJA/MBILI ZA CECAFA U-20 HUKO UGANDA!.. FULL-TIME. …

✍️
– Group A
Sudan 🇸🇩 4-0 🇩🇯 Djibouti
Uganda 🇺🇬 1-1 🇪🇷 Eritrea
Sudan 🇸🇩 3-3 🇪🇷 Eritrea
Djibouti 🇩🇯 1-5 🇺🇬 Uganda
….
– Group B
Kenya 🇰🇪 5-0 Zanzibar
Ethiopia 🇪🇹 0-4 🇹🇿 Tanzania
….
– Group C
Burundi 🇧🇮 3-3 🇸🇸 South Sudan
Somalia 🇸🇴1-2 🇧🇮 Burundi

✍️ MSIMAMO BAADA YA MATOKEO HAYO!..
📌GROUP A
1.Uganda 🇺🇬 P-2, +4, 4Pts
2.Sudan 🇸🇩 P-2, +4, 4Pts
3.Eritrea 🇪🇷 P-2, +0, 2Pts
4.Djibouti 🇩🇯 P-2, -8, 0Pts

📌GROUP B
1.Kenya 🇰🇪 P-1, +5, 3Pts
2.Tanzania 🇹🇿 P-1, +4, 3pts
3.Ethiopia 🇪🇹 P-1, -4, 0Pt
4.Zanzibar P-1, -5, 0Pt

📌GROUP C.
1. Burundi 🇧🇮 P-2, +1, 4Pts
2. South Sudan 🇸🇸 P-1, +0, 1Pt
3. Somalia 🇸🇴 P-1, -1, 0Pt
#CECAFAU20ChallengeCupUganda2019 #CECAFAU20
@Harunlugoyah

Design a site like this with WordPress.com
Get started