
Jina la Ndayilagije ni miongoni mwa majina maarufu miongoni mwa watu wa mpira Tanzania!!
Umaaruf wake haujaja hivi hivi bali kuna kazi kubwa ilifanyika mpaka kufikia hapa alipo
Njia alizopitia Ndayilagije ni njia alizopitia Idd seleman au Kwassi kufikia kuwa watu maarufu!! Ndayilagije alianza kujijengea jina msim wa 2016/17 kwa kuifikisha Mbao fc fainali ya shirikisho na kupoteza mbele ya Simba pale Jamhuri stadium Dodoma na kufungwa goli 2-1
Ndayilagije ndiye aliyetuletea kina Jamal Mwambeleko, Pius Buswita, Habib Kayombo, Benjamini Haule, Mveyekule, David Mwassa, Asante Kwasi, Ndikumana, Maganga, hakuna asiyejua balaa la hawa wachezaji na ile mbao isiyoshikika hakuna asiyejua kama huyu ndiye kocha aliyefanya CCM KIRUMBA kuwa sehem hatari kwa hizi tim zetu kubwa hapa Tanzania
Ndayilagije alikuwa na jicho la kuona mchezaji na kutambua ubora na uwezo wake na alikuwa na uwezo wa kumfanya mchezaji mdogo kuwa star hicho ni kipaji na si kila mtu anacho na aliweza kuunganisha wachezaji wa kawaida na kutengeneza tim ya ushindi
Baada ya hapo akatimkia zake KMC na pia huko aliendeleza kila alichoishia nacho Mbao akatengeneza KMC kuwa tim tishio na kuogopewa na kuifanikisha kushika nafasi ya nne kwenye ligi yetu na akaunganisha wachezaji moderate na kuwafanya kuwa tishio na style yake ilikuwa ile ile aliyotoka nayo Mbao
Leo Ndailagije ni Kocha mkubwa Tanzania ukiwaondoa AUSSEMS NA ZAHERA na anachokifanya sasa ni muendelezo wa alichokianza kwanye soka letu
Leo kumekuwa na kelele nyingi kumhusu Ndayilagije baada ya kufungwa na Sudan hapo jana mijadala ni mingi na mpaka inafikia kipindi watu wanadoubt uwezo wa Ndayilagije daaa huu ni upotevu wa fikra, nguvu na akili naweza sema hivyo
Ndayilagije ni mwajiriwa wa Azam yupo Stars kama deiwaka na anakabidhiwa Stars ikiwa kwenye mashindano na mbaya zaidi huku akiwa na majukum makubwa ya klab yake na mkumbuke Azam inashiriki shirikisho Afrika hana muda wa kupumzika kila siku yupo kazini akitoka Azam yupo Stars
Leo watanzania waliokuwa wanamtukana Amunike ndio hao hao wanaomtukana Ndayilagije na kusema bora Amunike daaa shukrani ya punda mateke
Inaendelea
✍🏻 @karimkondo

















#GermanyBundesliga




