AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA POLISI TANZANIA

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa wanahitaji pointi tatu za Polisi Tanzania kwenye mchezo utakaochezwa Jumanne, Februari 11,2020, Uwanja wa Uhuru.

Azam FC jana imeshinda mabao 3-1 mbele ya KMC inafikisha jumla ya pointi 41 ikiwa nafasi ya pili.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga, amesema kuwa kila kitu kipo sawa wataendelea kupambana.

“Tunashukuru kwa kushinda mbele ya KMC, tunahitaji ushindi mbele ya Polisi Tanzania ili kuendelea mwendo wetu wetu wa kufukuzia malengo yetu ambayo tumejiwekea,” amesema.

Visit website

ISHU YA WAAMUZI ITAFUTIWE DAWA MAPEMA, TIMU ZIJIPANGE KIUKWELI

HUKO mtaani wanasema waamuzi hasa wanaochezesha mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ni janga la soka letu.
Kelele hizo zimekuja hivi karibuni baada ya kutokea kwa matukio mfululizo yaliyozua utata, makubwa zaidi ni ya kushindwa kutafsiri vema sheria ya kuotea.
Nikiri wazi kwamba, kama mwamuzi hautakuwa makini wakati unachezesha mechi, suala la kuitafsiri sheria ya kuotea itakupiga sana chenga hasa pale inapotokea wachezaji wawili wanaocheza timu tofauti wanapokuwa karibu sana huku mmoja akizidi.
Hii sheria inahitaji umakini mkubwa sana kuitafsiri ikitokea ishu kama hiyo, wapo waamuzi ambao ni makini wanaoitafsiri sheria hiyo vizuri tu, lakini wengine kwao ni changamoto.
Katika pitapita zangu huku na kule nimesikia kwamba waamuzi wana madai yao, hawajalipwa kwa muda mrefu.
Wapo wanaosema kwamba ishu hiyo ya kudai inaingiliana na hiki kinachofanywa, wapo waliofika mbali zaidi na kuhusisha na suala la rushwa, eti kuna waamuzi wanatumika na baadhi ya timu.
Sijathibitisha hilo, lakini kama lipo, basi si uungwana, naamini haiwezi kuwa hivyo kwa sababu waamuzi wamefundishwa jinsi ya kuepuka vishawishi ambavyo vitaharibu kazi yake.
Kwa haya yaliyotokea, sihitaji kuwalaumu zaidi waamuzi, lakini kikubwa ninachoomba itafutwe dawa ya kuondoa haya malalamiko ya kila kukicha.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT) pamoja na ile Kamati ya Waamuzi, kukaa chini na kutatua hili tatizo.
Inawezekana kuwafungia isiwe dawa ya moja kwa moja kwa sababu unaweza kuwafungia waamuzi wengi, mwisho wa siku ligi itakuwa na uhaba wa waamuzi, hapo pia ni tatizo.
Ligi inatakiwa kuwa na waamuzi wa kutosha kwa maana ya kwamba mwamuzi mmoja asiwe na lundo la mechi, kama ikitokea mwamuzi mmoja akachezesha mechi nyingi, nalo ni tatizo.
Huko nyuma nilishawahi kusikia watu wakisema kuna mwamuzi fulani yeye amechezesha mechi nyingi za timu fulani tu, hilo halileti picha nzuri hata kidogo.
Nimalizie kwa kuziasa timu zinazoshiriki ligi hiyo kucheza kwa umakini mkubwa hasa mzunguko huu wa pili ambao ni wa lala salama.
Ukiangalia hivi sasa Simba inaongoza ligi hiyo, inafuatiwa na Azam, kisha Yanga inashika nafasi ya tatu. Timu hizi ndizo zimeonekana kila msimu zinawania zile tatu bora kwenye msimamo.
Mzunguko wa pili siku zote unakuwa na changamoto zaidi ya ule wa kwanza kwa sababu hapa unaweza kukuta na ratiba inabana zaidi.
Tazama hivi sasa timu kama Yanga kuna mechi mbili za mzunguko wa kwanza haijacheza, hivyo mzunguko huu wa pili ina kazi ya kucheza mechi nyingi zaidi na muda mdogo.
Hivyo lazima timu hiyo itakuwa na ratiba iliyobana zaidi. Hapa kama timu haijajiandaa vizuri, kuna hatari ya kupoteza pointi kirahisi.
Kama timu inawania ubingwa, lazima icheze kwa malengo. Kwanza kuhakikisha nyumbani inashinda, kisha ugenini iambulie angalau pointi moja na si kupoteza kabisa. Ikiwezekana kuondoka nazo zote.
Pia tukumbuke kuna timu za kushuka daraja, kama hazijajipanga vizuri, tunaweza kuzishuhudia zikishuka hata kabla ya msimu kumalizika, hivyo lazima zijipange.

Visit website

GUARDIOLA ISHU YA STERLING, ANAFIKIRIA KINOMA

RAHEEM Sterling nyota wa Manchester City leo atakosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya West Ham.

Nyota huyo ameumia nyama za paja na inasemekana kuwa huenda pia akakosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Pep Guardiola, Kocha Mkuu wa City amesema kuwa ni pigo kubwa na anafikiri ni miongoni mwa wachezaji waliowaweka kwenye wakati mgumu.


“Sterling ameumia na daktari ameshatuelekeza, nafikiri ngoja tuone lakini anaweza kurejea kabla ya mchezo dhidi ya Real Madrid,” amesema.

Visit website

BECKER WA LIVERPOOL AGOMEA KULA BATA, KAZI KAMA KAWA


ALISSON Becker raia wa Brazil mlinda nyavu za Liverpool amegomea kula bata wakati wa mapumziko na badala yake anaendelea kufanya mazoezi kujiweka fiti.
Mlinda mlango huyo ana jumla ya Clean Sheet 30 tangu aanze kuitumikia timu ya Liverpool.
Wakati huu wa mapumziko anaendelea kupiga tizi na timu ya Fluminense ya Brazil.
Inaelezwa kuwa kila siku anaonekana mazoezini kwenye timu hiyo akiwa na kakaye Muriel ambaye anaidakika timu ya Rio De Janeiro ya Ligi Kuu ya Brazil.
Mastaa wenzake wa Liverpool wengine wamekwenda Dubai kula bata.

Visit website

Ni. Ushindi tu morogoro kumnusuru kocha mkuu simba

Kikosi cha Simba kimeelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumanne, Februari 11 kwenye uwanja wa Jamhuri

Baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania, mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck anahitaji kuhakikisha vinara hao wa ligi kuu wanarejesha utamaduni wao wa burudani na ushindi

Ni mchezo ambao kama matokeo yatakuwa tofauti, Mbelgiji huyo anaweza kukutana na mabegi yake mlangoni atakaporejea jijini Dar es salaam

Sven aliitwa kujieleza kwa nini siku za karibuni timu imekuwa ikicheza chini ya kiwango katika kikao ambacho kiliwahusisha mabosi wa Simba wakiongozwa na Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa na Mwenyekiti Mwina Kaduguda

Kikao hicho kilikuwa kama mtego kwake kwani kama timu haitaonyesha mabadiliko anaweza kutimuliwa

Aidha Senzo alipoulizwa kuhusu hatma ya kocha huyo, alisema Sven anaendelea kuinoa Simba lakini hatma yake itabaki mikononi mwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji ‘Mo’

Messi Atamaliza Maisha Yake Barcelona. _

#Updates • Atamaliza Maisha Yake Barcelona.
_
KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa LIGI kuu Uingereza (Man City) bwana Pep Guardiola amefunguka na kusema kwamba Messi hawezi kuondoka Barcelona na atasalia kunako klabu hiyo hadi mwisho wa soka lake
_
🗣️“Anacheza Barcelona na atabaki kwenye timu hiyo, nataka iwe hivyo. Sitaki kuzungumzia mchezaji wa timu nyingine. Nadhani atamalizia maisha yake ya mpira kwenye timu hiyo,” alisema Guardiola.
_
Hivi karibuni kulizuka minong’ono ya kwqmba mchawi huo mweupe wa soka anataka kuihama klabu yake ya BARCELONA ifikapo Mwisho wa msimu huu.
_
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Messi Atamaliza Maisha Yake Barcelona. _

#Updates • Atamaliza Maisha Yake Barcelona.
_
KOCHA mkuu wa mabingwa watetezi wa LIGI kuu Uingereza (Man City) bwana Pep Guardiola amefunguka na kusema kwamba Messi hawezi kuondoka Barcelona na atasalia kunako klabu hiyo hadi mwisho wa soka lake
_
🗣️“Anacheza Barcelona na atabaki kwenye timu hiyo, nataka iwe hivyo. Sitaki kuzungumzia mchezaji wa timu nyingine. Nadhani atamalizia maisha yake ya mpira kwenye timu hiyo,” alisema Guardiola.
_
Hivi karibuni kulizuka minong’ono ya kwqmba mchawi huo mweupe wa soka anataka kuihama klabu yake ya BARCELONA ifikapo Mwisho wa msimu huu.
_
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Kocha Tz-prisons “Tumecheza Hovyo Sana”

#VplUpdates • “Tumecheza Hovyo Sana”
_
Baada ya mechi ya Jana kati ya Tz Prisons dhidi ya MBEYA CITY, Kocha mkuu wa Kikosi Cha Tz Prisons Adolf Rishard alikiri timu yake kucheza hovyo tofauti na matarajio na ndio sababu kubwa ya kupoteza mchezo huo pamoja na kadi nyekundu aliyopewa Mbangula.
_
🗣️ “Tumecheza vibaya tofauti na ilivyopaswa wapinzani wetu wametumia nafasi hiyo kutufunga nawapongeza kwa kupata ushindi pia kadi nyekundu imetuathiri kwa kiasi kikubwa”alisema Rishard.
_
Kwa matokeo hayo sasa Tz Prisons wapo nafasi ya 11 alama 25.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Man UTD Mpo, Striker Ighalo kuikosa kambi. _

#UtdUpdates • Man UTD Mpo, Striker Ighalo kuikosa kambi.
_
Mshambuliaji mpya wa Manchester United Odion Ighalo atakosa mazoezi na klabu hiyo nchini Uhispania kutokana na hofu kwamba virusi vya corona vinaweza kumzuia kuruhusiwa kuingia nchini Uingereza .
_
Ighalo mwenye umri wa miaka 30, alisafiri kuelekea mjini Manchester kutoka China wikendi iliopita baada ya kutia saini kandarasi ya mkopo kutoka klabu ya Shenghai Shenhua.
_
🗣️”Angependelea kujiunga na wachezaji wengine ili kuweza kujuana”, alisema Mkufunzi Ole Gunnar Solskjare akizungumza na runinga ya MUTV.
_
🗣️”Lakini hatari ya masharti ya mpakani, hatutaki kuhatarisha”.
_
Wakati huohuo kiungo wa kati wa Man United Scott McTominay na beki Axel Tuanzebe ambao wote wamekuwa na majeraha ya muda mrefu watasafiri kuelekea Uhispania. United hawatarudi hadi siku ya Ijumaa kabla ya mechi yao ya ligi ya Uingereza dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 17 February.
_
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Design a site like this with WordPress.com
Get started