Emerson Palmieri..Lukas njee ya dimba la chelsea

Meneja wa Chelsea, Frank Lampard alithibitisha kwamba beki wa Kushoto wa Klabu hiyo, Emerson Palmieri atakuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi… Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 25 alipata jeraha la paja katika mechi waliyopoteza dhidi ya Liverpool 2-1 Jumapili, Pia mlinzi mwenzake, Andreas Christensen nae alitolewa sababu ya kupata majeraha.

– Tatizo la goti la Andreas Christensen sio “kubwa sana” lakini Emerson hatorudi hadi mapumziko ya kimataifa… Kocha Lampard alisema hafahamu lini Christensen atarejea lakini hatokuwa na muda mrefu Kama mwenzake…. Mechi ya kwanza ya Chelsea baada ya mapumziko ya kimataifa watakuwa nyumbani dhidi ya Newcastle mnamo Oktoba 19.

– Emerson na Christensen, wameanza michezo mitano kati ya sita ya Ligi Kuu msimu huu.. Chelsea Wana michezo minne kabla ya mapumziko ya kimataifa, pamoja na mechi ya Kombe la EFL leo Jumatano dhidi ya Grimsby, na mechi ya Ligi ya Mabingwa ya UEFA huko Lille..
#chelseafc #PremierLeague #Updates
@Harunlugoyah

Pogba arejea kikosini..baada ya majeraha kupona

– Kiungo Paul Pogba ametejea ndani ya Kikosi cha Klabu yake ya Manchester United kwa Mchezo wa raundi ya tatu wa Kombe la Carabao dhidi ya Klabu kutoka League One, Rochdale hii leo Jumatano usiku.
..
– Pogba alipata Jeraha La Ankle lililomfanya atolewe katika Kikosi cha timu yake ya taifa ya Ufaransa kilichoshinda game zao za kuwania Kufuzu kwa EURO 2020 dhidi ya Andorra na Albania mwezi huu, tangu kuumia, Pogba amekosa michezo mitatu ya United, ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester mnamo Septemba 14, ushindi wa bao 1-0 wa Ligi ya Europa dhidi ya Astana na mchezo wa Jumapili wakipokea kipigo cha Magoli 2-0 dhidi ya West Ham katika Premier league.
..
🗣”Labda atapata dakika kadhaa dhidi ya Rochdale,” meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer alithibitisha…. Baada ya kucheza dhidi ya Rochdale huko Old Traord, United itaikaribisha Arsenal kwenye Ligi Kuu Uingereza siku ya Jumatatu..
#PaulPogba #ManchesterUnited #CarabaoCup
@Harunlugoyah

Messi afanyiwa mabadiliko mara 6 tu..tangu.kuwepo barcelona

6 – Lionel Messi amefanyiwa mabadiliko baada tu ya Kipindi cha kwanza kwa Mara Sita pekee akiitumikia @FCBarcelona katika Mashindano yote.

✋ Kabla ya Jana vs Villarreal, Mara ya mwisho Messi kutolewa baada ya Dakika 45, ilikuwa ni January 2016 vs Athletic Club katika uwanja wa Camp Nou na ilikuwa game ya #LaLiga.

✋ Barça imeshinda game tatu tu, Sare mbili na kupokea kipigo Mara Moja katika mechi hizo Sita ambazo King Leo alitoka baada ya kucheza Dakika 45 za Kipindi cha kwanza…
#Laliga #lionelmessi #FCBarcelona
@Harunlugoyah

TATIZO LAO NI UBORA WAO.

.
✍🏽Lionel Messi na Cristiano Ronaldo uenda wakawa ndio wachezaji bora wa soka wa muda wote, sina shaka kuhusu hilo. Kwa takribani zaidi ya miaka dazani (12) wamekuwa kwenye viwango bora kabisa, kitu ambacho hakikuwahi fanywa na wachezaji wengine hapo nyuma.
.
✍🏽Ila imekuwa ikitokea kila ikitolewa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka malalamishi uwa hayaishi kwamba huyu labda hakustahili ama yule alistahili zaidi.
.
✍🏽Imefika wakati hadi tuzo hizi za mchezaji bora wa dunia kila zikitolewa maneno huzuka kwamba kuna rushwa zinapita kwenye ofisi za wenye mamlaka kunako FIFA ili kumchagua mchezaji kwasababu za kibiashara. 👎😕
.
✍🏽Mi siamini hayo maneno, ila ninachoona ni kwamba, viumbe hawa wawili special wamefanya makubwa na kuwa na ubora wa hali ya juu kiasi cha kutengeneza wafuasi na washabiki wengi sana. Mpaka imepelekea huo UBORA wao kuwa ndilo tatizo.
.
✍🏽Utajiuliza kivipi UBORA uwe tatizo!?. Mwendelezo wa UBORA umetengeneza sumu baina ya wapenda soka, ambayo madhara yake kila tuzo zikitolewa wapo wataosema mmoja wao hakustahili ila mwingine alistahili zaidi. Na hata pale akichukua mwingine tofaut na hao bado watu hupinga kisa tu ni ile sumu iliyowaingia kutokana na UBORA wa Messi na Ronaldo kiasi cha kuwatia upofu kutoona ata hao wengine pia kuna muda wanastahili.
.
✍🏽Viwango walivyoweka na ubora wa hawa jamaa ndio sumu ya yote na ndio dawa pia ya yote, ila labda dawa ni pale viwango vyao vikifika tamati, tofauti na hapo tuendelee kushuhudia hii tamthilia isiyoisha mithiri ya ISIDINGO THE NEED.
.
✍🏽Wtitten by: Daniel Mtani Thomson
@danirito_thomson wa @sokaplace_

MATOKEO YA SOKA JANA +RATIBA YA SOKA LEO. :

#EnglandEFLCup
FT Colchester United P (4-3) Tottenham
FT Crawley Town P (5-3) Stoke City
FT Luton Town 0 – 4 Leicester City
FT Portsmouth 0 – 4 Southampton
FT Preston 0 – 3 Manchester City
FT Sheffield 0 – 2 Everton
FT Watford 2 – 1 Swansea City
FT Arsenal 5 – 0 Nottingham Forest
:
#SpainLaLiga
FT Real Valladolid 1 – 1 Granada
FT Real Betis 3 – 1 Levante
FT Barcelona 2 – 1 Villarreal
:
#ItalySerieA
FT Verona 0 – 0 Udinese
FT Brescia 1 – 2 Juventus
:
#FranceLigue1
FT Dijon 0 – 0 Marseille
FT Monaco 3 – 1 Nice
:
#BelgiumBekerVanBelgie
FT Cercle Brugge 0 – 1 RUS Rebecquoise
FT Waasland-Beveren 3 – 4 Westerlo
FT SK Ronse 0 – 3 Genk
:

RATIBA YA SOKA LEO.
:
#SpainLaLigaSantander
20:00 Leganes vs Athletic Bilbao
20:00 Mallorca vs Atletico Madrid
21:00 Valencia vs Getafe
22:00 Real Madrid vs Osasuna
:
#ItalySerie A
20:00 Roma vs Atalanta
22:00 Fiorentina vs Sampdoria
22:00 Genoa vs Bologna
22:00 Inter vs Lazio
22:00 Parma vs Sassuolo
22:00 Napoli vs Cagliari
22:00 SPAL vs Lecce
:
#FranceLigue 1
20:00 Saint-Etienne vs Metz
20:00 Nantes vs Rennes
20:00 Toulouse vs Angers
20:00 Lille vs Strasbourg
20:00 Montpellier vs Nimes
20:00 Amiens vs Bordeaux
20:00 Brest vs Lyon
22:00 Paris Saint-Germain vs Reims
:
#NetherlandsEredivisie
19:30 PSV Eindhoven vs FC Groningen
21:45 Ajax Amsterdam vs Fortuna Sittad
:
#BelgiumBekerVanBelgie
21:00 Rupel Boom vs Sporting Charleroi
21:00 KFC Mandel United vs Oostende
21:00 RFC Seraing United vs Kortrijk
21:00 Royal Cappellen FC vs Eupen
21:00 Zulte Waregem vs KFC Duffel
21:00 Union St.-Gilloise vs R CS Verlaine
21:30 Francs Borains vs Club Brugge
21:30 KFC Dessel Sport vs Royal Excel Mouscron
21:30 SC Eendracht Aalst vs Gent
21:30 St.Truiden vs OH Leuven
21:45 Beerschot vs Anderlecht
:
#VodacomPremierLeague
16:00 Singida United vs Mbao Fc
16:00 KMC FC vs Namungo FC
:
#EnglandEFLCup
21:45 Brighton vs Aston Villa
21:45 Burton Albion vs Bournemouth
21:45 Chelsea vs Grimsby Town
21:45 Milton Keynes Dons vs Liverpool
21:45 Oxford United vs West Ham United
21:45 Sheffield United vs Sunderland
21:45 Wolverhampton vs Reading
22:00 Man United vs Rochdale ✍🏻 @officialchristz

DIHILE ANATAKA NAMBA TAIFA STARS

Golikipa mkongwe Shabani Dihile amesema siri ya kucheza kwake muda mrefu mchezo wa soka ni matunzo anayoyapata kutoka kwa mkewe.
:
“Siri ya kudumu kwa muda mrefu ni kujitunza, namshukuru sana mkewangu kwa kunitunza hadi kufikia hapa”-Shabani Dihile.

Dihile mbaye kwa sasa anaidakia timu ya Green Warrios inayoshiriki ligi daraja la kwanza anasema anasikitishwa na uteuzi wa makocha wa timu ya taifa pamoja na uteuzi wa kikosi chenyewe.

Golikipa huyo amesema uteuzi wa sasa wa wachezaji wa timu ya taifa ni tofauti na ule uliokuwa ukifanywa wakati wa kocha Marcio Maximo.
:
“Maximo alikuwa anatembea ndio maana tulikuwa tunapata timu ya taifa bora na yenye nidhamu. Sasa hivi makocha wanaita tu fulani na fulani, hiyo haiwezi kuwa timu ya taifa ni mkusanyiko wa wachezaji.”
:
“Golikipa au mchezaji haangaliwi kwa mechi moja anaangaliwa kuanzia mechi tatu, nne na kuendelea.”
:
VIPI KUHUSU MPANGO WA KUTUNDIKA DARUGA? “Kwa magolikipa hawa…bado nitadumu hata kwa miaka mitano mbele, kwa sababu makipa wa sikuhizi wakisifiwa kidogo tu wanapotea kwenye game ndio tatizo la makipa wa Bongo.”
:
ANAWEZA KURUDI STARS KAMA ILIVYO KWA KASEJA?
:
“Mwenyezi Mungu akijalia nitarudi kwa sababu mpira ni mchezo wa wazi kama kocha ataniona nitarudi, vinginevyo bado nitaendelea kubaki hapa.”

Design a site like this with WordPress.com
Get started