Yanga yaomba TFF kusogeza mechi.yao ya ufunguzi ligi kuu TPL

Uongozi wa Yanga umewasilisha barua Tff kuiomba bodi ya ligi isogeze mbele mechi yao ya kwanza ya ligi kuu Tanzania bara.

Makamu mwenyekiti wa kamati ya Mashindano Saad Kimji amesema kwamba sababu ya kuomba mchezo huo kusogezwa mbele ni kutokana na kubanwa na ratiba ya ushiriki wa mechi yao ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana.

Kimji amesema kikosi cha timu hiyo kitacheza mchezo huo ugenini tarehe 24 na tarehe 26 kuamkia 27 timu itaanza safari ya kurejea hapa nchini,hivyo kucheza mechi yao ya Ligi tarehe 28 ni jambo ambalo anaamini halitawezekana.

Amesema kwamba lengo Lao ni kuiomba bodi ya ligi ili mechi hiyo iliyopangwa kuchezwa tarehe 28 sasa ichezwe tarehe 30 mwezi huu ili timu ipate muda wa kupumzika.
📝@daboten

Macha asema hana tatizo manara

Afisa Habari Mpya wa klabu ya Simba Gift Macha amesema anatarajia kupata ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wa klabu ya Simba kama ilivyo siku zote

Macha anayetajwa kuchukua nafasi ya Haji Manara aliyepewa majukumu mapya, amesema amekuwa na ushirikiano mzuri na wafanyakazi wa Simba akiwemo Manara

“Nimekuwa nikifanya kazi vizuri na Manara, ni mtu ambaye nikiwa na shida nampigia na ataipokea simu yangu mara moja,” amesema

“Naamini hakuna kitu kitabadilika baada ya mimi kuingia Simba Sc, tutaendelea kushirikiana kama kawaida”

Awali Manara alionekana hakuwa ameridhishwa na mabadiliko hayo ambayo yamepelekea yeye kuhamishwa kitengo

Lakini baada ya majadiliano na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji, Manara ameonyesha kuridhia majukumu yake mapya ya uhamasishaji ambayo bado yatamfanya aendelee kuwa karibu na mashabiki wa Simba

Jana alifuta mpango wake wa kuzungumza na waandishi wa habari huku akifichua kuwa bosi Mo alimzuia

Inaelezwa jukumu kubwa la Macha ni kuboresha kitengo cha habari hasa kukiendesha kisasa

Miongoni mwa maeneo yake ni pamoja na upashaji habari kupitia kurasa za mitandao ya kijamii, kuiboresha Simba TV ambapo inaelezwa uongozi wa Simba uko mbioni kuifanya kuwa chaneli rasmi itakayopatikana kwenye ving’amuzi vyote nchini

Hivi karibuni Simba imeanzisha chaneli rasmi ya Youtube ambayo itatumika kuwapa taarifa mbalimbali mashabiki wake pale kunapotokea matukio muhimu

Wachezaji wa simba sc wajazwa mamillioni

Nyota wa Simba mbali ya kuonekana kuwa na furaha kwa kufungua vizuri msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuchukua ubingwa mara tatu mfululizo wa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Azam FC, mabao 4-2, lakini kuanza leo Jumatatu muda wote akaunti zao zitajazwa noti.

Hii ni baada ya mabosi wa klabu hiyo kuahidi mapema kwamba wangewamwagia mamilioni kama wangeinyoosha Azam ikiwa sehemu ya utartibu waliojiwekea tangu msimu uliopita na kwa ushindi wa juzi Jumamosi usiku nyota hao watavuta Sh 50 milioni

Mgawanyo wa fedha hizo ni kwamba waliocheza kila mmoja atachukua si chini ya Sh 2 milioni, huku wale walioishia benchi kama kipa Ally Salimu watavuta si chini ya Sh 1 milioni na wale ambao waliishia kukaa jukwaani kama Ibrahim Ajibu watabeba si chini ya Sh 500,000.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema huo ni utaratibu ambao umewekwa katika timu yao ili wachezaji watamani kufanya vizuri katika kila mechi ili kuondoka na ushindi lakini inaongeza motisha kila mchezaji kutamani kushindana na kucheza katika kikosi cha kwanza.

“Ni utaratibu wetu ambao tunao tangu msimu uliopita katika mashindano yote ambayo tunashiriki kama tutashinda ujue kila mchezaji atapata motisha ya posho ila huwa zinatofautina kulingana na michezo husika kwani mechi nyingine ni kubwa na zinahitaji matokeo ya ushindi kuliko jambo lolote,” alisema.

“Kuhusu ushindi wa hilo tayari limeshapita na akili zetu zipo katika mechi ya marudiano ambayo tutacheza Jumapili dhidi ya US Songo ambayo kiu yetu ni kuona tunashinda na kusonga katika hatua inayofuata.

“Kama vile ambavyo wachezaji na uongozi wanajitolea katika kuhakikisha wanawapa mashabiki furaha kwa kushinda mechi basi na wao wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika mechi na UD Songo kama ambavyo tulifanya msimu uliopita ili kuendeleza wimbo la ushindi,” alisema Magori.

Mwanaspoti

Kikosi cha mbeya city charejea nyumbani

Kikosi chetu kimerejea nyumbani Mbeya baada ya michezo kadhaa ya kirafiki huko kanda ya kati. Tumecheza michezo ya kirafiki na vilabu vya ligi kuu dhidi ya Lipuni na Mtibwa pamoja na vilabu vingine vya ligi Daraja la kwanza.

Katika michezo miwili dhidi ya Lipuli na Mtibwa Sugar klabu yetu ilipata ushindi katika mechi zote.

Kwa sasa kikosi kinaendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kwanza dhidi ya Prisons SC tarehe 24.08.19 katika uwanja wa nyumbani. @officialmbeyacityfc
#full_solatzUpdates

Kikosi cha Yanga SC kinachokwenda kupambana na township rollersfc

Kikosi cha Yanga SC kilichosafiri kwenda Bostwana kwa ajili ya kuwavaa @townshiprollersfc

1. Metacha Mnata
2. Paulo Godffrey
3. Kelvin Yondani
4. Muharami Issa
5. Ally Abduljarim
6. Lamine Moro
7. Papy Tshishimbi
8. Mapinduzi Balama
9. Mohamed Issa
10. Ramadhani Kabwili
11. Sydney Khoetage
12. Rafael Daudi
13. Juma Balinya
14. Patrick Sibomana
15. Ally Ally
16. Jafari Mohamed
17.Feisal Salum
19. Issa Brigimana
20. Deusi Kaseke
21. Mrisho Ngasa

Kilala Kheri @yangasc @kmcfc_official @azamfcofficial @simbasctanzania

Shiboub aendeleza shangwe msimbazi

Kiungo Shariff Elden Shiboub juzi aliibuka nyota wa mchezo akiifungia Simba mabao kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam Fc

Kiungo huyo aliyetua Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea klabu ya Al Hilal ya Sudan, kwa sasa ndio habari ya mjini kutokana na umahiri wake anaoonyesha dimbani

Shiboub amesema mabao yake aliyofunga kwenye mchezo huo ni mwanzo tu, mambo mazuri mengi yanakuja Msimbazi

“Tunawashukuru mashabiki wetu kwa kuendelea kutuunga mkono, wao ni chachu ya mafanikio tunayopata”

“Huu ni mwanzo tu, watarajie mambo makubwa zaidi kutoka kwangu,” alisema Shiboub

Kwenye mchezo dhidi ya Azam, Shiboub alionyesha umahiri mkubwa katika kushambulia na hata kwenye ulinzi

Majeraha ya bocco yamtesa Aussems

Wakati Simba ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo ambao utapigwa Jumapili ijayo, kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems amesema itakuwa changamoto kama timu yake itamkosa nahodha John Bocco ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc juzi

Aussems amesema wingi wa majeruhi kwenye kikosi chake unaweza kuwasumbua kuelekea mchezo huo

Bocco ameungana na wajeruhi wengine Aishi Manula, Ibrahim Ajib na Wilker Da Silva

Hata hivyo Manula, Ajib na Da Silva tayari wameanza mazoezi mepesi lakini Aussems amesema wana nafasi ndogo ya kucheza Jumapili

“Kuongezeka kwa majeruhi kunanipa kazi nyingine, kwa sababu walikuwa watatu, Ajib (Ibrahim), Wilker Da Silva, Aishi Manula na sasa ameongezeka Bocco”

“Madaktari wanaiangalia hali yake, natumaini hatakuwa ameumia sana”

Design a site like this with WordPress.com
Get started