: Misri 🇪🇬 1-0 Tanzania 🇹🇿 #

F

FULL-TIME; Kutoka Dimba La Borg El Arab.. Wenyeji Misri wanaibuka na Ushindi Mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania.. Ulikuwa ni Mchezo wa kutest Mitambo, game nzuri imemalizika salamaa… Taifa Stars kabla ya kuanza kibarua cha AFCON watacheza game nyingine ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe..
:
Misri 🇪🇬 1-0 Tanzania 🇹🇿
#PreAfcon #TotalAFCON2019 #EGYTAN

Man united vs chelsea

– Kwa wahenga 😀😀.. Mara ya mwisho Chelsea kuivaa Man United katika game ya kwanza ya msimu wa Premier League ilikuwa ni 2004/05… Msimu huo kocha alikuwa Jose Mourinho na ilikuwa game yake ya kwanza katika Premier league Kama kocha..
:
– Chelsea walishinda goli 1-0 na mwisho wa msimu walienda kuwa Mabingwa Uingereza.. Goli La Mchezo huo alifunga Mshambuliaji wa Kimataifa wa Iceland, Eiður Smári Guðjohnsen 🇮🇸..
#premierleague #chelsea #manchesterunited

MAGORI KUNG’ATUKA SIMBA BAADA YA SIKU 60

MAGORI KUNG’ATUKA SIMBA BAADA YA SIKU 60

Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Crescentius Magori (pichani) amekubali ombi la bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo kuongeza siku 60 kwenye nafasi hiyo baada ya mkataba wake wa miezi sita kumalizika mwezi Mei mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari leo, Magori amesema aliyeomba kuondoka kwenye nafasi hiyo kwa lengo la kuongeza ufanisi wa kazi, ombi ambalo bodi imeridhia lakini ilimuomba aongeze siku 60 ili ijipange kutafuta mtendaji mwingine.
.
.
“Nitaendelea kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba kwa miezi miwili ijayo lakini wakati huohuo tutatangaza nafasi ya kazi ya Mtendaji Mkuu wa Simba ndani na nje ya nchi, na mimi mwenyewe nitasimamia ili tupate mtendaji mzuri wa kusaidia kwenda mbele”, amesema Magori.

Kuhusu sababu yay eye kutopenda kuendelea na nafasi hiyo, Magori amesema kwa uwezo na uzoefu alionao, anaona nafasi hiyo haimfai badala yake anastahili kuwa kwenye bodi kwaajili ya kufanya maamuzi makubwa ya klabu kuliko kuwa mtendaji.
.
.
“Level yangu ni kuwa kwenye bodi na kwenda juu, lakini kwenye utendaji hapa tunaweza kupata kijana mdogo mchapakazi. Mimi navyojiona ningefurahi zaidi kuwa kwenye bodi kwaajili ya kufanya maamuzi makubwa ya sera ya klabu, kufikiria Simba miaka mitatu tunaipeleka wapi, miaka mitano Simba iweje, kuleta fedha kwenye klabu, tunaingia ushirika upi, tunashirikiana vipi na watu wakubwa..
#Updates

Wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa duniani

– Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ndiye Mwanamichezo anaelipwa mkwanja zaidi duniani, akijiingizia $127m (£99.8m) katika miezi 12 iliyopita, kulingana na takwimu zilizo tolewa na Forbes; Nyota wa Juventus ya Ureno, Cristiano Ronaldo ni wa pili akijiinguzia $109m (£85.6m) na Mbrazili wa Paris St-Germain, Neymar anafuatia wa tatu kwa $105m (£82.5m).
.
– Kinara wa mwaka jana alikuwa ni Mwana masumbwi, Floyd Mayweather ambaye ameshuka katika orodha hii; Mcheza Tennis, Serena Williams ni mwanamke pekee aliye juu top 100, akipata dola 29.2m (£22.9m)…Bingwa Mara tano wa Dunia wa mbio za Magari ya Langa langa “Formula 1”, Lewis Hamilton na bingwa wa zamani wa uzito wa Juu katika Ndondi, Anthony Joshua ndio wanaopata mkwanja Mrefu Kama Wanamichezo wa Uingereza wakiwa nafasi ya 13 wakijiinguzia $55m (£43.2m).
.
– Gazeti hilo La biashara la Marekani limehesabu mapato ya wanamichezo na kuongeza fedha zao za mshahara kati ya Juni 2018 na Juni 2019.. Top 100 ni pamoja na wanamichezo kutoka nchi 25 na $4bn (£3,1bn) ndio mapato yao kwa pamoja yakiongezeka kwa 5% kutoka mwaka uliopita, wakati Mayweather alikuwa kinara mwa $285m (£224m).
.
– Messi ni Mchezaji wa Soka wa nane tofauti kuchukua nafasi ya kwanza katika Orodha hii ambapo takwimu zake zilianza rasmi mwaka 1990.. Pia ni mara ya kwanza kwamba ni wanasoka wote wameshikilia tatu bora…Messi ni mmoja Kati ya Wanamichezo 38 wasiokuwa Raia wa kwenye orodha… Paul Pogba kiungo wa Manchester United ni mchezaji Anaeongoza kutoka Ligi Kuu Uingereza akiwa katika nafasi ya 44 akijiingizia $33m (£25.9m).
✋🏻 TOP 10 inasimama hivii
1. Lionel Messi $127m (£99.8m)
2. Cristiano Ronaldo $109m (£85.6m)
3. Neymar $105m (£82.5m)
4. Canelo Alvarez $94m (£73.8m)
5. Roger Federer $93.4m (£73.3)
6. Russell Wilson $89.5m (£70.3m)
7. Aaron Rodgers $89.3m £70.1m)
8. LeBron James $89m (£69.9m)
9. Stephen Curry $79.8m (£62.7m)
10. Kevin Durant $65.4m (£51.3m)..
#Updates #forbessportsmoney #forbes
@Sokawaytz

– Mshambuliaji wa timu ya taifa ya kina Dada wa Brazil 🇧🇷, Marta Da Silva avunja rekodi

– Mshambuliaji wa timu ya taifa ya kina Dada wa Brazil 🇧🇷, Marta Da Silva amekuwa mwanasoka wa kwanza (mwanaume au Mwanamke) kufunga katika Michuano Mitano tofauti ya Kombe La Dunia.. Mkongwe huyo ameifikia rekodi ya Mjerumani, Miroslav Klose ya kuwa Wachezaji Pekee wenye Magoli mengi katika Historia ya Kombe La Dunia..
🇩🇪 Miroslav Klose (16)
🇧🇷 Marta Da Silva (16)
:
– 🇧🇷 Marta kafunga katika kombe La Dunia
🇺🇸 2003 ⚽️⚽️⚽️
🇨🇳 2007 ⚽️⚽️⚽️⚽️⚽️⚽️⚽️
🇩🇪 2011 ⚽️⚽️⚽️⚽️
🇨🇦 2015 ⚽
🇫🇷 2019 ⚽
👏 CAPTAIN, LEADER, LEGEND 👏🏻👏🏻👏🏻🙌🏻
#updates #FIFAWWC
@Sokawaytz

Real.Madrid yatumian €317m kusajilinwachezaj watano

– Klabu ya Real Madrid mpaka Sasa imetumia jumla ya €317m kusajili Wachezaji Watano tu katika kuhakikisha inajengwa Real Madrid mpya ya ushindani zaidi… Haya yote ni Maandalizi ya kocha Zinedine Zidane kabla ya kuanza kwa msimu ujao.. Ikumbukwe Zizou alikabidhiwa €500m kusajili Wachezaji wapya kikosini hivyo mambo ndio Kwanzaa yameanza kwenye pochi kasalia na kama €183m hiviii..🙌

– Walio mwaga wino kwa miamba hao mpaka Sasa ni..
📝 Eden Hazard [€100m]
📝 Luka Jović [€65m]
📝 Eder Militao [€50m]
📝 Rodrygo [€54m]
📝 Ferland Mendy [€48m]
#transfers #Updates

Design a site like this with WordPress.com
Get started