MEXICO KUPIGA MNADA NDEGE YA RAIS ILI KUDHIBITI UHAMIAJI HARAMU

MEXICO KUPIGA MNADA NDEGE YA RAIS ILI KUDHIBITI UHAMIAJI HARAMU

Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez ametangaza kupiga mnada ndege ya Rais na fedha zitakazopatikana zitatumika kusaidia jitihada za kudhibiti uhamiaji haramu

Hatua hiyo imekuja baada ya Mexico na Marekani kufikia makubaliano ili kuepuka vikwazo vya kiuchumi na ongezeko la kodi katika biashara ya nchi hizo mbili ambapo Mexico iliahidi kuongeza vikosi mipakani kudhibiti wahamiaji haramu kwenda Marekani

Ndege hiyo aina ya Boeing 787 Dreamliner ilinunuliwa mwaka 2016 kwa dola milioni 218 lakini sasa inaweza kuuzwa kwa kiasi kisichopungua dola milioni 150 na imeanza kupigwa mnada miezi michache iliyopita ikiwa California, Marekani

Sehemu ya fedha zitakazopatikana zitatumika kupeleka vikosi vya wanajeshi 60,000 mpakani kwa ajili ya kusaidia kudhibiti uhamiaji haramu

TUME YA SHERIA YAPENDEKEZA UWEPO WA SHERIA MOJA YA UFILISI

TUME YA SHERIA YAPENDEKEZA UWEPO WA SHERIA MOJA YA UFILISI

Tume ya Kurekebisha Sheria imependekeza kutungwa kwa sheria moja itakayosimamia masuala ya ufilisi nchini kutokana na kuwepo na changamoto mbalimbali hasa utoaji wa adhabu ndogo

Pendekezo hilo limekuja baada ya utafiti kubaini zipo sheria za ufilisi ambazo zimepitwa na wakati na baadhi zinatoa adhabu au faini ndogo kwa wale wanaokiuka taratibu za ufilisi kama vile Tsh. 200 au Tsh. 1,000

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu January Msoffe alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akiwasilisha ripoti ya mapitio ya Sheria zinazosimamia mfumo wa ufilisi Tanzania kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga

Jaji Msoffe alisema masuala hayo yamekuwa yakisimamiwa na sheria mbalimbali za kisekta kama vile Sheria ya Makampuni, Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha, Sheria ya Vyama vya Ushirika, Sheria ya Ufilisi, Sheria ya Bima, Sheria ya Mashirika ya Umma na Sheria ya Usajili wa Wadhamini

Jaji Msoffe alisema kuwepo kwa sheria hizo kunasababisha mkanganyiko kwa watumiaji kwa kutojua ni sheria ipi inayopaswa kutumika ili kutatua tatizo linalowakabili

Viwango vya Soka Duniani.. Afrika Mashariki.

✍🏻 Viwango vya Soka Duniani.. Afrika Mashariki.
– Uganda 🇺🇬 Kama kawaida wameendelea kuongoza kwa Afrika Mashariki, Duniani wapo nafasi ya 80 wakishuka nafasi Moja.. Afrika wapo nafasi ya 16.
– Kenya 🇰🇪 nao Kama kawaida wapo wanafuatia huku wakipanda kwa nafasi tatu Duniani Sasa wapo nafasi 105… Afrika wapo nafasi ya 23.
– Tanzania 🇹🇿 hatujapanda wala kushuka, Duniani nafasi ya 131 huku nafasi ya 35 Afrika na nafasi ya tatu Afrika Mashariki.
– Burundi 🇧🇮 Wanafuatia wakitukimbiza Haswaa, wamepanda kwa nafasi mbili Sasa wapo nafasi ya 134 Duniani na nafasi ya 36 Afrika.
– Rwanda 🇷🇼 Wanamaliza, nao wamepanda kwa nafasi mbili Sasa wapo nafasi ya 136 Duniani na nafasi ya 37 Afrika.
:
👉🏻 Majirani zetu wengine.. Ethiopia wapo nafasi ya 150 Duniani na 42 Afrika… Sudan Kusini wameshuka nafasi Moja Sasa nafasi ya 168 Duniani na 46 Afrika… Djibouti wamepanda nafasi mbili Sasa nafasi ya 194 Duniani na nafasi ya 50 Afrika, Eritrea wa mwisho kwa upili Afrika na nafasi ya 202 Duniani wakati wanaoburuza Mkia Afrika ni Somalia Pia nafasi ya 202 Duniani..
#FIFARanking #updates
@Sokawaytz

Viwango vya Ubora wa Soka Duniani.. Top 10 kutoka Bara La Afrika..

✍🏻 Viwango vya Ubora wa Soka Duniani.. Top 10 kutoka Bara La Afrika..
1.Senegal 🇸🇳 (22)
2. Tunisia 🇹🇳 (25)
3. Nigeria 🇳🇬 (45)
4. Morocco 🇲🇦 (47)
5. DR Congo 🇨🇩 (49)
6. Ghana 🇬🇭 (50)
7. Cameroon 🇨🇲 (51)
8. Egypt 🇪🇬 (58)
9. Burkina Faso 🇧🇫 (59)
10. Mali 🇲🇱 (62)
(Ndani ya mabano nafasi yao Duniani).
:
✍🏻 Vigogo 10 waliokosa top 10 ya Juu.
11. Ivory Coast
12. Algeria
13. Afrika Kusini
16. Zambia
17. Benin
18. Gabon
25. Zimbabwe
30. Guinea Bissau
31. Angola
32. Togo.
#FIFARanking #Updates
@Sokawaytz

Viwango vipya vya Ubora wa Soka Duniani

✍🏻 OFFICIAL!! Shirikisho La Soka Duniani “FIFA” hii leo Juni 14 limetangaza Viwango vipya vya Ubora wa Soka Duniani ambavyo hutolewa Kila mwezi… Hii ndio Top 10 Ilivyo Duniani.
1. Belgium 🇧🇪 2. France 🇫🇷 3. Brazil 🇧🇷 4.England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 5. Portugal 🇵🇹 6. Croatia 🇭🇷 7. Spain 🇪🇸 8.Uruguay 🇺🇾 9. Switzerland 🇨🇭 10. Denmark 🇩🇰
:
✍🏻 Vigogo 10 waliokosa top 10 ya juu..
11. Ujerumani
11. Argentina
13. Colombia
14. Italia
14. Netherlands
16.Chile
17. Sweden
18. Mexico
19. Poland
23. Wales.
#FIFARanking #fifawr

Real. Madrid yamnasa kinda wa kijapan

– Real Madrid imewashinda wapinzani wao FC Barcelona kumsajili Kinda Matata wa Kimataifa wa Japan mwenye umri wa Miaka 18, Takefusa Kubo.. Huu ni Usajili wa Sita kwa Real Madrid Dirisha hili Kubwa La Uhamisho wa Wachezaji.
.
– Kubo alidumu miaka Minne katika Academy ya FC Barcelona “La Masia” kabla ya kuachwa Machi 2015 na kujiunga na FC Tokyo mwaka 2016… Kinda huyo kacheza kwa mkopo tangu Agosti 2018 ndani ya Klabu ya Yokohama F. Marinos na Sasa katua Santiago Bernabeu.
.
– Barça walimuendea tena kutaka kumsajili, lakini Mshambuliaji huyo alikataa na kukubali Dau La Real Madrid na kumwaga wino wa Mkataba wa Miaka Sita… Jina Maharufu kwake nchini Japan wanamuita “Japanese Messi” uwezo, akili ya mpira, mbio wamemfananisha Lionel Messi.
#transfers #Updates
@Sokawaytz

Eden Hazard amesema kuwa yeye hajali juu kutovaa jezi namba 10

– Eden Hazard amesema kuwa yeye hajali juu kutovaa jezi namba 10 au kutokuwa na majukumu ya kupiga mikwaju ya penalti katika Klabu yake mpya ya Real Madrid; Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Ubelgiji alijiunga na Blancos kwa €100 (£88m / $112m) kutoka Chelsea wiki iliyopita.
.
— “Nimezungumza na Modric kwa kupitia kwa Kovacic, nikamuuliza kama angeweza kuniachia Mimi jezi No.10, alisema hapana, ni lazima nitafute namba nyingine,” alisema Hazard.
.
— Nyota huyo Pia aliongeza kuwa “Kwangu mimi namba 10 ya jezi si muhimu, lakini kucheza na jezi hii, na nembo hii inatosha”.
.
– Hazard pia amesema hatolazimisha kutaka kuchukua penati ili apige yeye ndani ya Real Madrid, kwani kawakuta wapiga wengine wengi wa penati ndani ya Klabu… Sergio Ramos msimu uliopita alipiga penati Nane Kati ya 12 za Klabu hiyo, Karim Benzema akipiga penati tatu na Gareth Bale akipiga penati moja..
#Updates
@Sokawaytz

Design a site like this with WordPress.com
Get started