Juma Balinya raiaa wa uganda amesaini Mkataba wa miaka Miwili.. Yanga

Mshambuliaji mpya wa Klabu ya Yanga SC, Juma Balinya amesaini Mkataba wa miaka Miwili kuwatumikia Mabingwa hao wa Kihistoria nchini.. @officialbalinya amejiunga na Yanga akitokea Klabu ya Police FC ya Uganda.
:
– @officialbalinya ambaye Pia ni Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya nyumbani kwao Uganda msimu uliomalizika wa 2018/19, ametambulishwa na uongozi wa Yanga mbele ya wanachama wa klabu hiyo katika hafla ya kuichangia Yanga inayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam..
#WawekezajiNiWananchi #YangaSc #transfers
@Sokawaytz

Manchester United kumsajili Beki wa Kimataifa wa Ufaransa

BREAKING: Manchester United inajiandaa kufanya Usajili wao wa pili wa msimu kwa kumsajili Beki wa Kimataifa wa Ufaransa na Klabu ya West Ham, Issa Diop.. United imeandaa dau La £45m + Mchezaji wao mmoja ili kuinasa saini ya Beki huyo.. West Ham imeripotiwa kutosikiliza ofa hiyo badala yake wanadai £60m ili kumuachia Issa Diop. (Sky Sports)..
#transfers

ORODHA YA BAADHI YA WACHANGIAJI KATIKA KUBWA KULIKO YA YANGA

1.Rostam Azizi tzs. 200ml.
2.Kikwete tzs. 5ml.
3.GSM Co ltd tzs. 300ml
4.Waziri Mkuu 10ml.
5.Kamati ya Hamasa tzs. 50ml.
6. Magembe jr. Tzs. 1.4ml
7.Kamati ya Utendaji tzs. 50ml.
8.Wabunge wa washabiki wa 9.YANGA tzs. 40ml
10.Mariam Ditopile (mb) tzs. 1ml.
11. Mwigulu tzs. One player
12.RC Makonda tzs. Katoa Uwanja wa Mpira (kajibu mapigo ya kikwete kuwapa Simba uwanja wa BUNJU wakati akiwa Rais)

KIKOSI..CHA *🇬🇭GH⚽A vs RSA🇿🇦*…friend. Match

⚽ *🇬🇭GH⚽A vs RSA🇿🇦*

*GHA🇬🇭*
1 Richard Ofori
20 Kwadwo Asamoah
22 Andy Yiadom
15 Kasim Adams
14 Lumor Agbenyenu
21 John Boye
9 Jordan Ayew
7 Christian Atsu
5 Thomas
10 André Ayew
23 Thomas Agyepong

*RSA🇿🇦*
1 Ronwen Williams
2 Ramahlwe Mphahlele
6 Samuel Mabunda
5 Hlompho Kekana
3 Innocent Maela
11 Lars Veldwijk
4 Daniel Cardoso
7 Bongani Zungu
8 Sibusiso Vilakazi
9 Themba Zwane
10 Lebohang Maboe

⏰ Game begins in *3 mins*!

*To follow Football on Duta:*
*Add to your group: +917395963274*

HONG KONG: MUSWADA WA SHERIA WASITISHWA KUFUATIA MAANDAMANO

HONG KONG: MUSWADA WA SHERIA WASITISHWA KUFUATIA MAANDAMANO

Serikali inayoongoza Jimbo la Hong Kong imetangaza kusitisha muswada uliolenga kuruhusu watuhumiwa wa makosa mbalimbali kushtakiwa China bara

Wananchi waliandamana kupinga muswada huo kutokana na uhalisia kwamba Hong Kong ni Jimbo la China lenye mamlaka kamili hivyo muswada huo ungeharibu uhuru wa jimbo hilo

Taarifa ya Serikali imeleeza kuwa muswada huo umesitishwa ili itolewe nafasi ya kufikiri upya

SUDAN KUSINI KUFUNGA BAADHI YA BALOZI ZAKE ILI KUBANA MATUMIZI

SUDAN KUSINI KUFUNGA BAADHI YA BALOZI ZAKE ILI KUBANA MATUMIZI

Sudan Kusini inapanga kuzifunga balozi zake kadhaa kwa ajili ya kubana matumizi ikiwemo balozi zilizopo nchini Norway na Ufaransa

Serikali ya mjini Juba imesema uamuzi wake huo ni kutokana na kuzorota kwa uchumi katika nchi hiyo huku bado ikikabiliwa na ukosefu wa utulivu wa kisiasa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mawien Makol amesema kwamba Sudan Kusini imechukua hatua ya kuzifunga balozi zake katika nchi za Ufaransa, Norway, Ghana, Kuwait na Italia

Makol amesema wameamua kujaribu kufanya matumizi kwa busara kulingana na uwezo wa nchi hiyo kwa kuwa wanagharamia balozi zao kutokana na rasilimali za nchi hiyo pamoja na fedha za misaada ya kuunga mkono mipango ya ujenzi baada ya nchi hiyo kutoka kwenye migogoro

KODI KUANZA KULIPWA BAADA YA MIEZI 6 TANGU KUPATA TIN –


Serikali imesema mfanyabiashara ama mwekezaji atakapopatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) atatakiwa kuanza kulipa kodi baada ya miezi sita

Hatua hii inatofautiana na hali ilivyo sasa ambapo mfanyabiashara anapopewa TIN anaanza kufanyiwa tathmini (tax assessment) ya mapato yake ya biashara na kutakiwa kulipa kodi

Hatua hii itawezesha wafanyabiashara na wawekezaji wapya kupata muda wa kujiandaa na mahitaji yanayotakiwa katika shughuli wanazofanya na kuondoa usumbufu au dhana ya woga wakati wa kuanzisha biashara

Aidha, Serikali imeiagiza Mamlaka ya Mapato kuanzisha dawati la kushughulikia mapingamizi ya makadirio ya kodi ambapo mapingamizi ya uthaminishaji na utambuzi yatashughulikiwa ndani ya saa 24

Kodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa Julai 1 mwaka huu isipokuwa pale ilipoelezwa vingine

AFRIKA MASHARIKI: KENYA KINARA BAJETI KUBWA KWA MWAKA 2019/2020q

AFRIKA MASHARIKI: KENYA KINARA BAJETI KUBWA KWA MWAKA 2019/2020

Nchi ya Kenya imeongoza kwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha ukilinganisha na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo imetenga kiasi cha Ksh trilioni 3.02 sawa na Tsh trilioni 60

Bajeti hizo kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ziliwasilishwa jana ambapo nchi zilizotoa bajeti zao ni Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda

Waziri wa Fedha nchini Rwanda, Uzziel Ndagijimana amesema nchi yake imepanga kutumia Rwf trilioni 2.8 ambayo ni sawa na trilioni 6 kwa fedha za Tanzania

Uganda inakadiria kutumia kiasi cha dola bilioni 10.9, ambayo ni karibu trilioni 25 za Tanzania na Tanzania imetenga bajeti ya Tsh trilioni 33.1

Design a site like this with WordPress.com
Get started