
Half time’ Young Africans 0-1 Township Rollers #CAFCL

Half time’ Young Africans 0-1 Township Rollers #CAFCL

Mchezo umeisha kwa sare ya bila kufungana. Mchezo wa kumaliza kazi tutacheza Dar kati ya Agosti 23-25, 2019. #CAFCL #NguvuMoja

.

FULL-TIME | West Ham United 0-5 Manchester City
[ Raheem Sterling ⚽⚽⚽, Sergio Aguero, Gabriel Jesus ]
:
Sergio Aguero amefunga mabao saba katika michezo ya kwanza ya Msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza — Wayne Rooney, Frank Lampard na Alan Shearer (wote Magoli Nane) wamefunga zaidi ya Kun!.
.
– Raheem Sterling ni mchezaji wa nane Katika Historia kufunga hat-trick Katika Mechi ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza, na wa kwanza tangu Didier Drogba mwaka 2010-11.
.
West Ham 0-5 Man City
West Ham 0-4 Man City
West Ham 1-4 Man City
West Ham 0-4 Man City
West Ham 0-5 Man City
:
Matokeo ya aggregate ndani ya London Stadium Sasa Ni… West Ham 1-22 Man City. 😳!
#premierleague #ManchesterCity #westham
@Sokawaytz


Mapumziko. #CAFCL #NguvuMoja


Kikosi cha #mabingwawakihistoria🇹🇿 dhidi ya TownshipRollers kwenye mchezo wa kwanza wa klabu bingwa Africa.
#Mchezowaklabubingwaafrica

– Klabu ya Tusker FC ya ligi kuu Nchini Kenya inatarajia kuwasili Jijini Mwanza, Tanzania kwa ajili ya kupiga kambi ya Maandalizi ya Msimu Mpya.
.
– Wakiwa huko, Klabu hiyo inatarajia kucheza mechi Nne za Kirafiki kabla ya kivumbi Cha Lugi Kuu Nchini kwao Kenya kuanza Disemba Mwaka huu… Mechi watakazocheza wakiwa Tanzania 🇹🇿 ni dhidi ya..
Jumatatu, Agosti 12 vs Biashara FC
Ijumaa, Agosti 16 vs Gwambina FC
Jumamosi, Agosti 17 vs Polisi
Jumapili, Agosti 18 vs Alliance FC.
:
– Kikosi kamili Cha Klabu hiyo kinachotua Nchini ni..
👉 MAKIPA: Robert Mboya, Emery Mvuyekure, Michael Wanjala.
👉 MABEKI: Marlon Tangauzi, Sammy Meja, Hillary Wandera, Vincent Ngesa, Gabriel Wandera, Eric Ambunya, Rodgers Aloro, Brian Odhiambo
👉 VIUNGO: Peter Nzuki, Michael Madoya, Apollo Otieno, Kevin Okoth, Eric Zakayo, Boniface Muchiri, Jackson Macharia, Mario Kakai, Faraj Ominde, Sydney Ochieng.
👉 WASHAMBULIAJI: George Odhiambo, Timothy Otieno, David Majak.
#KPL #Updates #tuskerfc
@Sokawaytz
Mabingwa wa Tanzania Simba wako nchini Msumbiji ambapo muda mchache ujao watashuka dimbani kuikabili UD Songo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali
Hiki hapa kikosi kinachoanza;

Ni Abdallah Haji Shaibu,ambaye wengi hupenda kumuita Ninja kutokana na miondoko yake na shughuli yake uwanjani.Mchezaji mwenye uhakika na kuamini anacho kifanya bila kujali kelele za wale wenye maneno ya kejeli au dharau hata matusi pengi.Yeye aliamini alicho kifanya na kile ambacho alikiona sahihi kwake.Ndivyo alivyo kinyonga.
Alisajiliwa Yanga akitokea timu ya Taifa Jang’ombe ya Zanzibar ambayo aliwika nayo kunako mashindano ya Kombe la Mapinduzi yenye historia ya kupigwa kila mwanzo wa mwaka kiadhimisha Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.Ni jicho la Mzambia George Lwandamina lililomuona kamanda huyu na hili lilikuja baada ya Zanzibar kuonekana kuwa na record ya kutoa wachezaji wazuri hasa kwenye safu ya ulinzi kama Kassim Issa aliyewika pale Mtibwa Sugar miaka ya 2000,Nadir Haroub aliyewika na Yanga,Nassoro Masoud Chollo (Simba),Aggrey Morris na Azam,Haji Mwinyi na Yanga huku Ninja akitua Yanga kukamilisha idadi hiyo.Hata kwa sasa bado record inazidi kuwalinda kina Muharami Issa,Ally Ally (Yanga),Abdallah Kheri (Azam) na wengine.

Usajili wake kutoka Taifa Jang’ombe kuja Yanga ulibezwa na wengi huku baadhi wakisema ameletwa bure na Cannavaro ambaye alisemekana kuwa ni mjomba wake wakati huo Yanga ikiwa kwenye kipindi kigumu cha ukata hivyo safari yake ilionekana kuwa kishawishi na sio matakwa ya mchezaji.Ninja alikuwa wa kwanza kabisa kumwaga wino pale Yanga kuelekea Msimu wa 2016-2017 akiwatangulia kina Youth Rostanda (Africa Lyon)Ibrahim Ajib(Simba) na Pius Buswita (mbao).Maneno ya kubeza na dharau yalizidi pale iliposemekana kuwa amesajiliwa Yanga kwenda kuziba pengo la Mtogo Vicent Bossou ambae alitimka kunako klabu hiyo.Kila mmoja aliongea alivyojisikia.
Alianza kuonekana kwenye mechi ya kirafiki ya kujipima nguvu kabla ya kufunguliwa kwa pazia la Ligi ambapo Yanga walicheza na Ruvu Shooting huku Abdallah Haji akijifunga katika harakati za uokoaji,lakini wengi wakimsifu kutokana na ubora wake positioning na guarding akisimama vyema na Dante kwenye eneo la mwisho.
Muda ni mwamuzi sahihi kwenye maisha ya mwanadamu,Ninja alipata muda kidogo wa kuwa nje huku akijengwa vizuri kisaikolojia kutokana na pressure kubwa ya kuchezea kwenye moja ya hivi vilabu.
Alirudi dimbani huku akionekana kuimarika mno,Ni mlinzi mwenye sifa zote za kusimama kama mbele ya mlinzi wa mwisho (sweeper). Urefu wake,kasi na nidhamu ya kimchezo ni baadhi ya mambo yaliyomfanya Ninja aonekane kuwa Ninja haswa.Alikuwa mzuri wakati wa kucheza mipira ya juu na kuokoa hatari zote kuelekea golini.Uhodari wake ulimfanya aonekane kuwa mtu muhimu na tegemeo kwenye safu ya ulinzi ya Yanga na kuwa fit kucheza na yeyote kati ya Yondan au Dante.Ilifika wakati ambapo kwenye kikosi cha Yanga kuliko kukosekana kwa Ninja ilionekana kuwa ni bora hata angekosekana mmojawapo kati ya Dante au Yondan.Kila alipokosekana kwenye mechi ambazo Yanga walicheza pengo lake lilidhihirika uwanjani.

Nidhamu yake,kujituma na kujiamini kumemfanya Ninja aonekane bora na thamani yake kuwa kubwa zaidi ndani ya kikosi cha Yanga hasa kwenye mechi za Ligi,mechi kubwa kama za Derby au mashindano mbalimbali.Maana alikuwa ni mchezaji aliyebeba tafsiri sahihi ya eneo la safu ya ulinzi la timu ya Yanga.Ni mmoja wa wachezaji waliotumikia na kupambania Yanga ambayo imepita kwenye vipindi vigumu hasa kutoka mwanzo hadi mwishoni mwa msimu ulioisha wa 2018-2019.
Msimu umeisha na Ninja alipata dili la kwenda kucheza nje ya nchi kunako klabu ya MFK VYSKOV ya Jamhuri ya Szech ambapo klabu hiyo imemtoa kwa mkopo kwenda klabu ya La Galaxy ya nchini Marekani ambayo anatumikia nyota wa Sweden Zlatan Ibrahimovic ambaye aliwahi kutamba na vilabu vya Intermillan,Barcelona, PSG na Manchester United ya Uingereza.Anaenda kusimama kwenye eneo la ulinzi ambapo kule kwenye final third atakuwemo Zlatan Ibrahimovic.
Atakuwa ametimiza moja ya ndoto yake ya kusakata kabumbu ughaibuni.
Ninja ni mmoja wa wachezaji waliopata fursa ya kutoka nje,na hapa it’s obvious kwamba industry ya mpira wa miguu sasa imekuwa kubwa,Azam Tv wamechukua priority kubwa kuwatoa vijana wetu kama kina Eliud Ambokile,Maka Edward, Ally Ng’anzi,Dickson Kibabage,Habibu Haji Kiyombo,Kelvin John,Shizza Kichuya na wengine.Ni chachu kwa vijana wetu na wanapaswa kujituma zaidi ili kufata nyayo za wenzao.Haya ni matunda ya kazi nzuri ya Azam Tv ambayo wanafanya kazi kubwa ya kurusha Ligi yetu live na kuonekana kunako mataifa mbalimbali.Leo tunawa zungumza hawa kama sehemu ya somo kwa wengine.
Adui wa mafanikio wa mtu ni yeye mwenyewe.
Waaambieni kina Muharami Issa,Makame,Haruna Shamte,Kassim Hamis,Salim Aiyee,Idd Naddo,Ally Sonso,Ally Ally,Rashid Juma na Balama Mapinduzi kuwa Kinyonga ni kiumbe mwenye utajiri ndani yake ambao amejaaliwa na mwenyezi Mungu.
Kujiamini,kujitambua na kujituma.
Kila la kheri Ninja,Tunakutakia mafanikio mema katika kupambana na challenge mpya.
Mwisho,Powered
By @bikotanzania
Imeandaliwa na @josejose189
Tags @a.shaibu_ninja_23

16:00 UD Songo v Simba SC
16:00 African Stars v KCCA FC
16:00 Green Eagles v Orlando Pirates
16:15 KMKM v 1° de Agosto
18:00 Yanga SC v Township Rollers
18:00 Kano Pillars v Asante Kotoko
19:00 Cano Sport v Mekelle
19:00 SM Bamako v Horoya SC
19:00 Big Bullet v Platinum Stars
19:00 Brikama v Raja Casablanca
19:00 Black Mamba v ZESCO United
19:00 Rahimo v Enyimba SC
:
✍🏻 Ratiba ya Mechi za Kombe la Shirikisho Barani Afrika hii leo Jumamosi, Agosti 10..
.
15:00 Bandari FC v Ahly Shendi
16:00 Buildcon v Green Buffaloes
16:00 AS Kigali v KMC FC
16:00 Proline FC v Security
17:30 Pelican v Maniema Union
18:00 Akonangui v Ashanti Gold
18:00 Tornadoes v Santoba
20:00 SNIM v Esae
21:00 Belouizdad v ASCOT
21:00 Mogadishu City v Malindi FC.
#CAFCC #CAFCL #TotalCAFCC #TotalCAFCL
@Sokawaytz

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo saa kumi jioni wanashuka dimbani nchini Msumbiji kuikabili UD Songo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali
Kikosi cha Simba kilitua Msumbiji mapema jana kwa usafiri wa ndege ya kukodi na baadae jioni kikafanya mazoezi ya mwisho
Simba imekwenda Msumbiji ikiwa na kikosi cha wachezaji 19. Meneja wa timu hiyo Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri, hakuna majeruhi
Matokeo mazuri katika mchezo wa leo yataiweka Simba katika nafasi nzuri ya kusonga mbele raundi ya kwanza kwani mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Taifa
Simba ina rekodi ya kipekee inapocheza uwanja wa Taifa
Kocha Patrick Aussems amesema lengo lao ni kuhakikisha wanavuka kwenda raundi ya kwanza