Eden Hazard apewa jezi namba 7

OFFICIAL | Klabu ya @realmadrid imethibitisha kwamba Mshambuliaji wao Mpya wa Kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard atakuwa akivaa jezi Namba 7.
.
– Hazard amesajiliwa na Mabingwa hao wa Kihistoria Barani Ulaya akitokea CHELSEA akikokuwa akivaa jezi Namba 10, kabla ya Hazard, jezi Namba 7 ilikuwa ikivaliwa na Mariano Díaz!.
#updates #LaligaUpdates #RealMadrid
@Sokawaytz

NAMUNGO DAY KUFANYIKA TAREHE 10/08/2019

KAA TAYARI KUIPOKEA NAMUNGO FC
.
Namungo FC itaingia Ruangwa Mjini kesho ikitokea Lindi Mjini kwenye Kambi maalumu ya Maandalizi ya Msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/202
.
Timu itaingia Ruangwa asubuhi wananchi wote mnaombwa kujitokeza kuipokea kwa shwangwe na vigeregere Timu yetu pendwa.
.
Aidha Siku ya Jumamosi Tr. 10/07/2019 itakua siku maalumu ya Namungo FC kutambulisha wachezaji, na mambo mengine kuhusu Timu kuelekea msimu ujao. Siku hii maalumu imeitwa “NAMUNGO DAY”
.
Kwenye Namungo Day kutakua na Mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania iliyopanda Ligi kuu msimu huu
.
Hakutakua na Kiingilio. Yaani ni BUREEEEEE!
.
Basi Tukajazane…..wa Kata ya Mnacho, Mandawa, Matambarale, Chunyu, Malolo, Narungombe, Namichiga, Likunja, Luchelegwa nk.
.
Namungooooo Juuuuuu!!
.
#Tumedhamiria
#WeAreNamungo
#SouthernKillers
#KilaHaruaDua
#HatupoiHatuboi .
@namungofc

Mchezo ya UD Songo vs Simba kupigwa saa tisa alasili

Klabu ya UD Songo imepanga muda wa mchezo wa kesho wa ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Simba utapigwa saa tisa Alasiri kwa muda wa Msumbiji ambao huku Tanzania itakuwa saa kumi jioni

Kikosi cha Simba kiliondoka nchini mapema leo kuelekea Msumbiji tayari kwa mchezo huo

Msafara wa Simba ulijumuisha wachezaji 19 ambao watarejea kesho baada ya mchezo

Mabingwa hao wa Tanzania bara, wana kazi moja tu ya kupata matokeo ya ushindi au hata hata sare ugenini ili kujiweka katika nafasi nzuri mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Taifa

Simba inapewa nafasi kubwa ya kufuzu raundi ya kwanza kutokana na uimara wa kikosi chake, hata hivyo matokeo mazuri kwenye mchezo huo wa ugenini ni muhimu

UD Songo sio timu ya kubeza, imekuwa na takwimu nzuri inapocheza katika uwanja wake wa nyumbani

Simba yawasili msumbiji

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimewasili salama nchini Msumbiji tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya wenyeji wao, UD Songo

Mabingwa hao wa nchi waliondoka jijini Dar es salaam mapema leo kwa usafiri wa ndege ya kukodi

Jioni Simba itafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa kesho Jumamosi saa kumi jioni kwa saa za Tanzania

Uhamisho wa Wilfried Zaha kwenda Everton wapata pigo

Winga wa Crystal Palace na Ivory Coast, Wilfried Zaha mwenye umri wa Miaka 26 amepata pigo baada ya uhamisho wake kwenda Everton kutibuka lakini amesisitiza anataka kuondoka Selhurst Park.
.
– Zaha anahofia amepoteza nafasi ya kuhama kwa kitita kikubwa imepotea baada ya dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa siku ya Alhamisi… Meneja wa Palace Roy Hodgson alimzuia Zaha kufanya mazoezi siku ya Alhamisi kwa sababu mchezaji huyo ”hakuwa na utulivu wa kiakili” baada ya kuwasilisha barua ya kuomba uhamisho..

Wachezaji watatu wa yanga kuukosa mchezo wa kesho ….

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba asilimia kubwa ya wachezaji wao wamefanikiwa kupata leseni ambazo zitawawezesha kucheza mechi ya kesho ya klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers.

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Dismas Ten amesema kwamba hadi kufikia sasa ni wachezaji watatu pekee ambao ndio hawajapata leseni za mchezo huo.

Wachezaji hao ni pamoja na Farouk Shikalo,David Molinga na Mustapha Selemani ambao kwa mujibu wa taarifa yake inaeleza kuwa wakati wowote kuanzia sasa leseni za wachezaji hao zitapatikana.

Amesema kwamba anaamini leseni za wachezaji hao zitapatikana kabla ya mchezo huo kwani kuna mawasiliano mazuri yanaendelea kufanyika baina ya Yanga na CAF.

Yanga kesho inataraji kucheza mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers ya nchini Botswana,mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es saalam

Messi atwaa tuzo ya goli bora UEFA ..2018/19

OFFICIAL | Shirikisho la Soka Barani Ulaya, @UEFACOM Limethibitisha kuwa Goli la Mshambuliaji wa Klabu ya FC Barcelona, Lionel Messi alilofunga dhidi ya Liverpool limechaguliwa kuwa Goli Bora la Msimu wa Michuano ya @championsleague 2018/19:.
.
– Messi alifunga goli Maridadi kwa free-kick nje ya Box Katika Uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou, Barça ikishinda 3-0 Siku ya Mei Mosi Mwaka huu Katika hatua ya Nusu fainali… Hata hivyo Barça haikuvuka kucheza fainali Baada ya kutandikwa 4-0 huko Anfield!.

Kahata Adatishwa na Simba day

Baada ya kushuhudia ‘nyomi ya kufa mtu’ Uwanja wa Taifa wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamsos ya Zambia, kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Mkenya Francis Kahata, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuendelea kuisapoti timu yao ili iendelee kufanya makubwa zaidi.

Mashabiki wa Simba, Jumanne wiki hii walijitokeza kwa wingi na kufanikiwa kuujaza Uwanja wa Taifa huku wengine wakilazimika kuwekewa TV katika Uwanja wa Uhuru ili kushuhudia kilichokuwa kikiendelea siku hiyo ya kilele cha Simba Day, ambayo waliitumia kutangaza nyota wao wa msimu mpya pamoja na kucheza mechi hiyo ya kirafiki.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kahata alisema anaamini kutokana na ubora wa wachezaji wanaounda kikosi hicho, wanaweza kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa na kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara.

“Kinachotakiwa ni kuendelea kushirikiana na kucheza kitimu, pia mashabiki wasichoke kutuunga mkono ili kutupa hamasa ya kufanya vizuri zaidi katika mechi zetu kama walivyofanya Simba Day,” alisema.

Kahata ambaye amesajiliwa msimu huu akitokea Gor Mahia, wakati akiitumikia timu hiyo ya Kenya akiwa na Mnyarwanda Meddie Kagere, walitengeneza ushirikiano mzuri na kuifanya safu yao ya ushambuliaji kuwa tishio na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Kenya.

Na kwa muda mrefu, Kagere alikuwa akitamani nyota huyo kusajiliwa Simba ili waweze kuendeleza ushirikiano wao wa kucheka na nyavu, jambo ambalo mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi hao wanasubiri kuliona likitokea.

Simba ambayo msimu uliopita ilifika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf), imeondoka leo asubuhi kwa ndege ya kukodi kuelekea Msumbiji tayari kwa kuanza kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi kwa kuivaa UD Songo kwenye mechi ya raundi ya awali.

Manara awaomba watanzania kuziunga mkono timu zote nne..

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo waziunge mkono timu zote nne zinazoshiriki michuano ya CAF ikiwemo Yanga kwani mafanikio ya timu zote yataendelea kuinufaisha Tanzania

Kwa mara ya kwanza mwaka huu Tanzania imepata nafasi ya kuingiza timu nne kwenye michuano ya CAF kutokana na mafanikio yaliyopatikana msimu uliopita, Simba ikichangia zaidi baada ya kufika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa

Changamoto iliyopo ni kwa timu zote nne kufanya vizuri (angalau kufika makundi) ili kuendelea kuwa na nafasi ya uwakilishi wa timu nne kwenye michuano hiyo

“Imetuchukua miongo kadhaa kama nchi kupata fursa ya kuwakilishwa na vilabu vinne Kwenye Mashindano ya CAF,” amesema Manara

“Ni Simba wenye mchango mkubwa sana katika hili lakini kama Taifa tunatakiwa tufanye vizuri zaidi kupitia wawakilishi wetu ili tuendelee kwa miaka ijayo kuwa na klabu nne katika mashindano ya CAF”

“Najua ni ngumu kunielewa leo , lakini nawaomba Wanasimba wote kesho msizomee Yanga, msilipe kisasi na wekeni maslahi mapana ya nchi,sisi ni waungwana na uungwana ni vitendo”

“Kama hujiwezi usiende Taifa na ikibidi kwenda na huwezi kuwashangilia bora ukae kimya”

“Najua walitukera msimu uliopita lakini tuiangalie nchi kwanza na pia tujue wao, Azam na KMC pamoja na sisi ndio tuna nafasi ya kuendelea kupewa nafasi nne tena msimu ujao”

Tafadhali watu wangu nieleweni katika hili, naiangalia Tanzania kama nchi,utani na kuzodoana kwetu utatugharimu sote,kama kuwacheka tuwacheke baadae lakini kwa sasa interest ya Tanzania iwe moja”

Design a site like this with WordPress.com
Get started