Watuhumiwa watano wasakwa..tukio la kutekwa MO

Upande wa Mashtaka katika kesi ya kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ‘Mo’ umedai kuwa bado wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa watano ili kuunganishwa katika kesi hiyo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai hayo mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakalima na wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao watano raia wa Msumbiji na Afrika Kusini.

Watuhumiwa ni Henrique Simbue, Daniel Berdardo Manchice, Issac Tomu na Zacarious Junior wote ni raia wa Msumbiji na Phila Tshabalala raia wa Afrika Kusini.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 3, 2019.

Mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ni Dereva taxi, Mousa Twaleb(46).

Katika kesi ya msingi Twaleb alijihusisha na genge la uhalifu `anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Mei Mosi, 2018 na Oktoba 10, 2018 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na Johannesburg, nchini Afrika Kusini, kwa makusudi alitoa msaada wa kutendeka vitendo vya jinai au uhalifu wa kupangwa kwa lengo la kujipatia faida.

Katika shtaka la pili, Twaleb anadaiwa, Oktoba 11, 2018 katika maeneo ya Hoteli ya Colloseum iliyopo wilayani Kinondoni jiji Dar es salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawajafikishwa mahakamani, walimteka nyara Mohamed Dewji kwa nia ya kumhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari.

Katika shtaka la tatu, Wakili Simon alidai Julai 10, 2018 katika maeneo ya Mbezi Beach wilaya ya Kinondoni, mshitakiwa alitakatisha fedha kiasi cha Sh8 milioni wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la kushiriki genge la uhalifu.

Mwanaspoti

Mchezo wa simba vs UD Songo .kupigwa saa kumi.jiono

Uongozi wa klabu ya Simba umepanga muda wa mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo

Mchezo huo utapigwa Jumapili August 25 saa 10 jioni

Msemaji wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki kuendeleza utamaduni wa kuiunga mkono timu yao kwenye michuano hiyo kwa kujaza uwanja siku ya Jumapili

“Kwetu mashabiki sio mchezaji wa 12, ni mchezaji wa kila nafasi uwanjani. Tunashinda lakini mashabiki wanachangia sana,” Manara aliwaambia waandishi wa habari kwenye Mkutano uliofanyika Serena Hotel

“Simba ndio timu ambayo imeongoza msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kujaza mashabiki uwanjani. Tunataka tuliendeleze hilo mwaka huu”

“Na bahati nzuri mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa umepangwa siku nzuri. Utakuwa Jumapili saa 10 jioni”

“Tunataka mashabiki mshabikie mwanzo mwisho, tusisubiri mpaka Shiboub apige mtu chenga, mashabiki tunaenda uwanjani kushabikia”

“Kwa mashabiki wa Simba hii ni Champions League, kazi yetu mashabiki ni kushabikia, twendeni”

“Matumaini yangu tutawatoa UD Songo. Kwa maandalizi yetu, mipango na mapenzi ya Mungu tutashinda”

“Tunawategemea mashabiki waje kutujazia uwanja, waje kutushangilia. Nawaomba Wanasimba tuje kwa wingi kuhakikisha tunaenda kujaza uwanja na tunashinda.”

Chelsea yampeleka beki wake Davide Zappacosta AS Roma kwa mkataba wa mkopo mwaka mmoja

Beki wa kushoto wa klabu ya Chelsea Davide Zappacosta amekubali kujiunga na klabu ya AS Roma kwa mkataba wa mkopo mwaka mmoja.
:
Kwa mujibu wa Skysports Chelsea na Roma tayari zimekubaliana juu ya uhamisho huo na wiki hii anatarajia kufanya vipimo vya afya 🔵 #CFC #Chelsea #Roma #transfers

Kahata atwaa tuzo kenya

Kiungo wa Simba Francis Kahata ameshinda tuzo wa kiungo bora wa ligi kuu ya Kenya msimu wa 2018/19 wakati akiitumikia Gor Mahia

Kahata alitwaa tuzo hiyo msimu wa 2017/18 pia

Kiungo huyo anayekipiga kwenye timu ya Taifa ya Kenya, ameanza vyema maisha yake kunako klabu ya Simba ambapo mwishoni mwa wiki alifunga moja ya mabao ya Simba kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Azam Fc mchezo wa Ngao ya Jamii

Bocco kufanyiwa vipimo zaidi

Nahodha wa Simba John Bocco amefanyiwa uchunguzi zaidi kubaini ukubwa wa jeraha lake alilopata kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc mwishoni mwa wiki

Bocco aliumia kwenye mchezo huo baada ya kugongana na Frank Domayo kwenye dakika ya 22 na nafasi yake kuchukuliwa na Clatous Chama

Daktari wa Simba Yassin Gembe alisema mkongwe huyo alifanyiwa uchunguzi zaidi jana ili kuweza kumpatia matibabu sahihi yatakayomuwezesha kuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoivaa UD Songo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Jumapili

Bocco alishindwa kufanya mazoezi na wachezaji wengine jana

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema anasubiri ripoti ya Daktari kujua hatma ya mchezaji huyo kuelekea mchezo wa Jumapili

Hata hivyo amesema wapo wachezaji wengine wanaoweza kucheza nafasi yake kama hataweza kurejea dimbani mapema

Simba inakabiliwa na changamoto ya majeruhi kwenye kikosi chake, sasa ikiwakosa wachezaji wanne Aishi Manula, Ibrahim Ajib, Wilker Da Silva na sasa John Bocco

Simba kuweka hadharani uongozi mpya..leo

Uongozi wa klabu ya Simba leo utazungumza na wanahabari katika mkutano utakaofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam

Pamoja na mambo mengine, inaelezwa klabu ya Simba huenda itawatambulisha rasmi wafanyakazi wapya wanaojiunga na timu hiyo kwenye nafasi mbalimbali

Kwenye Mkutano huo Simba huenda ikamtangaza rasmi CEO mpya ambapo Senzo Mazingisa kutoka Afrika Kusini ndiye anayezungumzwa sana na vyombo vya habari

Nafasi nyingine ni ya Afisa Habari, Mwanahabari Gift Macha akitajwa kuchukua nafasi ya Haji Manara

Mkutano utafanyika saa sita mchana

Design a site like this with WordPress.com
Get started