Mavugo ang’ara.ligi.kuu zambia

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo, mambo yameendelea kumnyookea nchini Zambia baada ya kuibuka mmoja wa wafungaji bora wa ligi kuu

Mshambuliaji huyo wa Napsa Stars FC, ametwaa kiatu cha dhahabu akifunga mabao 10 sawa na Austin Muwowo na Adam Zikiru Adams

Mavugo alishindwa kuwika wakati akiitumikia Simba hapa nchini, lakini mambo yamemnyookea huko Zambia

Mavugo alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi kilichoshiriki fainali za Afcon 2019, hata hivyo hawakuvuka hatua ya makundi

Mganda Patrick Henry Kaddu..asajiliwa RS Berkane inayoshiriki ligi kuu Nchini Morocco.

Jana Mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda Patrick Henry Kaddu amekamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya RS Berkane inayoshiriki ligi kuu Nchini Morocco.

Kaddu amejiunga na klabu ya Rs Berkane akitokea katika klabu ya KCCA.
#TransferNewsUpdates

MATOKEO YA SOKA JANA JUMANNE +RATIBA YA SOKA LEO

ChampionsLeagueQualification
FT APOEL Nicosia 0 – 0 Ajax
FT CFR Cluj 0 – 1 Slavia Prague
FT LASK 0 – 1 Club Brugge

#EnglandChampionship
FT Birmingham City 2 – 0 Barnsley
FT Derby County 1 – 2 Bristol City
FT Hull City 0 – 1 Blackburn Rovers
FT Middlesbrough 1 – 0 Wigan Athletic
FT Sheffield Wednesday 1 – 0 Luton Town

#SouthAfricaPremierLeague
FT Amazulu Durban 0 – 0 Orlando Pirates
FT Mamelodi Sundowns FC 1 – 1 Cape Town city

Champions League – Qualification
22:00 Dinamo Zagreb vs Rosenborg
22:00 Olympiacos vs FC Krasnodar
22:00 Young Boys vs FK Crvena Zvezda

England – Championship
21:45 Cardiff City vs Huddersfield Town
21:45 Charlton Athletic vs Nottingham Forest
21:45 Fulham vs Millwall
21:45 Leeds United vs Brentford
21:45 Preston North End vs Stoke City
21:45 Queens Park Rangers vs Swansea City
22:00 West Bromwich Albion vs Reading

#SokaplaceUpdates
Imeandaliwa na @officialchristz

Ashley Cole..kustafu soka ..sasa kuwa kocha

MICHEZO: Aliyekuwa Beki wa zamani wa Chelsea na Arsenal, Ashley Cole ametangaza rasmi kustaafu soka na kuanza kuangalia uelekeo mwingine katika kutafuta sifa za kuchukua hatamu za ukocha

Cole alijiunga rasmi na Arsenal mnamo mwaka 1999 baada ya hapo akazitumikia Crystal Palace, Chelsea, Roma, LA Galaxy na Derby

Beki huyo raia wa Uingereza ameshacheza jumla ya michezo 107 katika timu ya Taifa ya England, pia ameshinda kombe la England mara mbili akiwa na Arsenal 2004

DANIEL STURRIDGE KUACHANA NA LIVEPOOL

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool mwenye miaka 29 amewasili nchini Uturuki ili kukamilisha usajili wake katika klabu hiyo ikiwa ni baada ya kuachiwa huru na Liverpool

Liverpool ilimuachia huru katika kipindi cha majira ya joto cha usajili mwaka huu, ikiwa ni baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 6 na kufunga magoli 67 katika michezo 160

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England alianza kucheza soka la kulipwa katika timu ya Manchester City na baadaye kujiunga Chelsea mwaka 2009

Tazama.viingilio vya UD songo

Uongozi wa klabu ya Simba umeweka hadharani viingilio vya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya UD Songo ambao utapigwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ametaja viingilio hivyo;

Mzunguuko Tsh 5,000/-

VIP B na C Tsh 15,000/-

VIP A Tsh 30,000/-

Platinum Tsh 100,000/-

Platinum Plus Tsh 150,000/-

Klabu ya UD Songo inatarajiwa kuwasili Ijumaa, siku mbili kabla ya mchezo huo

Katika hatua nyingine, Manara amezitakia kheri timu zote za Tanzania zipate matokeo katika michezo hiyo ya marudiano ili ziweze kusonga mbele hatua inayofuata

Amesema Tanzania inapaswa kulinda nafasi nne za ushiriki wa michuano ya CAF, hivyo ni vyema kwa timu zote kufanya vizuri ili kujiongezea pointi huko CAF

Manara asema yeye ndiye msemaji wa simba

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema hawezi kukaa katika kiti hicho milele na kwamba itafika siku ataondoka na mwingine atakikalia

Hata hivyo amewataka mashabiki wa Simba na wadau wote watambue hadi sasa yeye bado ndiye msemaji wa klabu hiyo hadi hapo itakapotangazwa tofauti

Haji amesema hakuna tatizo katika klabu ya Simba

Alikuwa akijibu swali la Mwanahabari aliyetaka kufahamu juu ya hatma yake kufuatia taarifa zinazodai Gift Macha anatarajiwa kuchukua nafasi yake

Design a site like this with WordPress.com
Get started