
Na
Jose Jose
Baada ya KMC juzi jana haikuwa kazi ndogo kwa Azam na Yanga kuipeperusha vyema bendera ya Taifa baada ya kushinda michezo yao ya marudiano,Azam waliwika pale Chamanzi baada ya kuwasukuma Fasil Kenema kwa ushindi wa 3-2 huku Yanga wao wakiuwasha kule Gaborone kunako Dimba la Botswana National Stadium baada ya ushindi wa goli moja bila na kuwasukuma nje wenyeji wao Township Rollers ya nchini humo.
Kwanini?
Commitment, Discipline and Dedication.
Leo Simba wamepoteza nyumbani mbele ya washabiki wao tena katika ardhi yao dhidi ya Ud do Songo ya Mozambique. Baada ya sare ya kutofungana wiki iliyopita pale msumbiji hatimaye jamaa wamekuja kuamua game hapa Taifa na kuwaondosha Simba kwenye mashindano.
MBINU ZA MWALIMU
Prof.Aussems alianza na Wawa na Nyoni kwenye eneo la beki wa kati huku pembeni akimchezesha Gardiel na Shomari wakati wa kumlinda Manula ambaye ni dhahiri kuwa hakuwa na match fitness. Kwa Shomari sina swali,he was good na alitimiza kazi yake effectively. Makosa ya Wawa nilisha zungumza ni mengi mno wakati wa kujilinda na anam overwork Nyoni. Wawa hajui kuji position na hilo ndio tatizo lake kubwa.Hali hii iliyumbisha safu ya ulinzi ya Simba na ikasababisha wenzake kwenda kufanya marking kwa makosa kutokana na uzembe wake wa kuzurura bila kuzingatia nidhamu ya nafasi.Why Gardiel instead of Mohammed? Hapa ndipo Prof.alipotu danganya.Hatukuwa na haja ya kuanza na Gardiel ambaye huwa ana mistakes nyingi za kujisahau pia cross zake hazipo accurate kama alivyo Mohammed. Ukiwa nyumbani first plan is to attack, mfumo ulimuhitaji zaidi Tshabalala ambae ni mzuri kwenye kupandisha timu, ana cross za uhakika pia anawahi kurudi tofauti na huyu rafiki yangu ambaye akienda hadi apigiwe kelele.Nyoni namsifu yupo vizuri na aliwajibika pia alibeba msalaba wa Wawa mpaka mwisho wa game.Ule ndio ukomavu wenyewe.

Shiboub, Deo Kanda,Kahata na Chama ambao walisimama kama viungo kumchezesha Kagere huku wakilindwa na Mkude ambaye alikuwa deep akilinda ngome yake na wale wahuni wa Ud do Songo wakafanikwa kumuweka kati mara kadhaa.Ukitaka kushambulia lazima umiliki mpira.Hii ndio kanuni ya kushambulia.Mfumo ulimuhitaji zaidi Dilunga kwenye first half ambaye angekuja kupokelewa na Kahata Nyambura lakini mwalimu alifanya kinyume.Kahata ni mzuri katika kuchezea mpira lakini sio mwepesi ku create chance na kuachia kama alivyo Dilunga. Square pass nyingi zilizokuwa zikipigwa pale kati zilichelewesha timu ambayo ilikuwa na uchu wa kupata bao la mapema ambalo hali iliyowafanya wacheze kwa pressure kubwa baada ya hilo kishindikana na opponents kuwa win kisaikolojia na kimbinu.Utulivu ulikosekana hasa baada ya makosa ya marking yaliyotendeka na wageni kujipatia bao.Uzembe wa ulianzia kwa Mkude hadi Wawa.
MAANDALIZI
Kipengele muhimu hiki kwa ajili ya kusaka ushindi.Ni lazima timu iandaliwe kimbinu,kiufundi na kisaikolojia.Kwamba we are at home,tunapaswa kufanya nini ili tushinde,hii ni mechi ya aina gani na tukishindwa itakuwa na advantage gani.Ilikuwa ni lazima Ud do Songo waingie kwa tahadhari maana wapo ugenini na wanacheza na timu kubwa kama Simba.Lakini hakukuwa na sababu ya Simba kuingia kwa kuwabeza wale wageni wakijua wameshamaliza mchezo kabla hata ya game.Walitakiwa kujengwa vizuri kisaikolojia ili wacheze kwa ari na kwa kujituma zaidi huku wakizingatia nidhamu na kupunguza makosa kadhaa ambayo mwishowe yaliwa athiri.Wachezaji wameingia kwa pressure kubwa na kuchanganyikiwa zaidi baada ya kufungwa kunako dakika 15 za kipindi cha kwanza.Niliamini baada ya kwenda mapumziko watatulia maana mwalimu atakuwa amewatuliza vyumbani lakini walirudi kwa pressure ile ya mwanzo na kuwapa wageni nafasi ya kuwatawala in mentality

UTIMAMU
Hakukuwa na sababu ya kumchezesha Manula ambaye hakuwa na match fitness pamoja Wawa Paschal. Wale wanaonekana kabisa hawaja recover vizuri na wanacheza kwa tahadhari.Mwalimu na benchi lake wana lazimika kubeba lawama hizi.Yupo Gerson Vieira ambaye ni beki wa kati mbrazil Simba walimsajili kwa ajili ya mechi hizi na si kucheza dhidi ya Namungo tu,Beno alikuwa fit na Ali perform vizuri dhidi ga Azam lakini leo hakucheza,Haya ni baadhi ya mambo yanayo dhihirisha uzembe na kui cost timu.
Mwalimu alichelewa kuwatuliza wachezaji wake mapema na waliendelea kucheza kwa pressure huku wakishibdwa kuwaheshimu wapinzani wao.
Ni wakati wa Simba kujitathmini upya,
Ligi imeanza hivyo nadhani itakuwa na wakati mzuri wa kujiweka sawa.
Mwisho
Tags @simbasctanzania
Powered by @bikotanzania