Nicolas Pepe amlambisha vyenga beki Virgil van Dijk

– Winga wa Arsenal, Nicolas Pepe amekuwa mchezaji wa kwanza kumlamba chenga beki wa Liverpool, Virgil van Dijk katika mchezo wa #PL, beki huyo wa Kimataifa wa Uholanzi kacheza mechi 50 kwenye Ligi Kuu bila Mchezaji yoyote yule Kumpiga chenga, Ni tangu Mchezaji wa mwisho Mikel Merino mnamo Machi 2018, Merino akiwa na Newcastle.
#PremierLeagueUpdates
@Sokawaytz

ZAERA ATUMIA PRINCIPLE ZA AMUNIKE KUIONDOSHA TOWNSHIP ROLLERS

Imeandaliwa
Na @josejose189

Ameondoka Amunike ila bado namkumbuka.Nakumbuka maneno aliyozungumza wakati Stars ikielekea Cameroon kuna mashindano ya AFCON.Mnigeria huyo alisema,”mtu yeyote anayewaza kuhusu mafanikio lazima ajikite kwenye mambo matatu ambayo ni nidhamu,nia na kujitolea” haya ni mambo ya msingi sana kwa yeyoye anayewaza kuanza kufikiria kuhusu safari ya kusaka mafanikio.Kwa sasa hayupo,yupo kwao Nigeria lakini maneno yake bado yanaishi.
Nimemkumbuka!
:
Leo Yanga wamefanikiwa kuwatoa Township Rollers ambao ni wenyeji wao katika dimba la Gaborone linalo fahamika kama Botswana National Stadium.Wamewatoa Rollers kwenye mashindano wakiwa nchini kwao,kwenye ardhi yao na mbele ya washabiki wao.
:
Pongezi za dhati kwa Yanga,wametembea kwenye zile points za Amunike.Tuliona Discipline, Commitment pia wachezaji walikuwa dedicated.
:
Yanga waliingia uwanjani kwa discipline kubwa huku wakicheza kwa tahadhari kwa kuwaheshimu wenyeji wao huku wakiwaza zaidi kuhusu matokeo kuliko wale washabiki waliopo pale uwanjani walikoja kuwa support Rollers.
:
Nampongeza Mwalimu kwa kusisitiza nidhamu ama hakika walifanikiwa.Na ndivyo inavyo takiwa,ukiwa mgeni first plan is to defend.Lazima ujiweke vizuri katika kujilinda then ndipo uwaze kwenda kushambulia.
:
Lamine Moro na Kelvin Yondani walisimama katikati kumlinda Metacha Mnata ambaye alikuwa nyota wa mchezo leo.Kelvin alimaliza mkoba akisimama kama Stopper huku Moro akicheza mbele yake kama sweeper. Wali fit vizuri maana kwanza wanafanana kwenye style of playing na namna ya kwenda kujilinda huku wakizidiana vitu vichache mno.Yule Lamine ni mrefu halafu ana nguvu.Mwanzoni alikuja kama mpole Ila siku hizi nae amekuwa katili.
:
Godfrey Paul kwenye full back ya kulia nilitegemea uwepo wake,na ameisaidia mno timu kutokana na push yake wakati wa kuipandisha timu.Nampongeza mno kwani baada ya ile yellow card hakutoka mchezoni kama nilivyo wahi muona kwenye games kadhaa zilizo pita.

Ally Sonso,leo alichezeshwa kama full back wa kushoto lakini lengo kubwa la mwalimu ikiwa ni kuimarisha nguvu kwenye safu ya ulinzi hasa pale kati thus why sometimes akawa anafanya exchange na kina Yondan mana wote ni walinzi wa kati.Muharami alihitajika lakink kutokana na uzito wa game mwalimu alionesha umahiri wake,sometimes class is permanent but Form is temporary.
Yanga wakuja kuwa na safu nzuri ya ulinzi chini ya Yondan Na Moro pia Sonso huku Muharami Na Boxer wakiunda jopo hilo kusimamisha ukuta mgumu wa Berlin.
:
Papy akicheza kama holding huku Banka akiwa juj yake, moja ya combination ambayo imekubali na mwalimu nimemuona akitumia hasa kwa games serious kama hizi.Banka nishazungumza,amezaliwa upya.Amekuwa mchezaji wa mechi kubwa.Papy alifanya kazi kubwa mno in first half na hata kipindi cha pili pia ambapo ndio alifanya kwa weledi zaidi.Alikaba hadi kivuli.Alitibua na alikuwa ana pokonya.Aliyekuwa anamzidi ujanja ni yule jamaa yetu rasta yule (Natto).Sibomana yeye kama kawaida ailiuwasha kutoka pembeni kule upande wa kushoto huku Balama Mapinduzi akicheza inside right wing,kasi,umakini na jicho lake limekuwa na faida mno kwa Yanga.Alikuwa msumbufu,yeye na Sibomana walikuwa wanaamua njia ya kupitisha timu ili ishambulie.Walinzi wa Rollers wakikimbia kuwa mark unakuta Balinya na Sadney wamefika.
:
Balinya Juma,huyu nilieleza tangu mechi ya hapa Taifa na mechi kadhaa za kirafiki walizocheza Yanga.Ni mcheza hatari lakini hataki kujionesha kama yeye ni hatari.Achana na fail aliyopiga,hata driving yake ilikuwa inaweka safu ya ulinzi ya Rollers kwenye wakati mgumu sana.Ana speed,timing na control. Sometimes ni mzuri akiwa anatokea pembeni hasa upande wa kulia.Na huyo ndiye aliyeamua game.Ana hatari kama alivyo Sibomana.Ambaye leo kila aliposhika mpira mwalimu wa Rollers alimsonta kwa wachezaji wake.Sadney Urikhob,mwalimu alimuweka kama mshambuliaji na mtu ambaye atakuwa anabaki mbele wakati timu imerudi kujilinda.Stamina yake na fitness imembeba zaidi.Hiyo imemfanya amalize dk 90 japo wengi tulihisi kuwa kachoka.Alikuwa mtu muhimu wa kuitikisa defense line ya adui.

Kuingia kwa Ngassa,Fei na Daudi ilikuwa ni plan ya mwalimj ya kuongeza nguvu kwenye eneo la kati huku akiwaza zaidi kujilinda na ksaidia kuongeza nguvu ya kushambulia.
:
Yanga wameshida na wataendelea na hatua inayofuata.Hongereni sana Yanga.
:
Mbali na ushindi waliopata suala la Chemistry bado limekuwa tatizo sugu kwa Yanga. Hasa kule mbele.Safu ya ushambuliaji ya Yanga imekuwa ikipoteza mipira mingi na kukosa umakini.Hii ni kutokana na kukosa partnership na chemistry ya kudumu.Balinya,Sadney na Sibomana ndio waliopewa rungu,lakini hawa wote ni wazuri wakiwa wana attack kutokea pembeni. Bado haja patikana mshambuliaji mtulivu ambaye muda wote anawaza kufunga kama alivyo Kagere wa Simba au Makambo zama zile.Pale mbele pana poor finishing
Nafasi chache zinazotengenezwa kutoka kwenye wings na katikati bado hazijaweza kutendewa haki na hasa wakati huu timu ikingia kwenye hatua inayofuata.
:
Madhaifu ya safu ya ushambuliaji yanaigharimu timu.Timu itakuwa inalinda muda wote maana mipira ikifika kwenye final third area inapotea bila sababu.Nadhani mwalimu ana kazi ya ziada kwa hili.
:
Yanga sc watakutana Na Zesco united ya Zambia inayo fundishwa Na Lwandamina kwa sasa.
:
Hongereni Yanga na Azam,Kila la kheri Simba sc kesho dhidi ya Ud do Songo.
: Prepared by @josejose189
#SokaPlaceTanzania

Maombi ya barcelona kumnasa neymar yaendelea kugonga mwamba

Ombi la Barcelona la kumnunua kwa mkopo wa dau la milioni £137 ( zaidi ya bilioni 382 za Kitanzania) pamoja na kumpatia kandarasi ya kudumu mshambuliaji wa Brazil, Neymar (27) limekataliwa na PSG huku mabingwa hao wakiitisha dau la milioni £229 (zaidi ya bilioni 639 za Kitanzania)

Lakini inadaiwa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) wanadhani thamani ya Neymar inakaribia £250 (zaidi ya bilioni 697 za Kitanzania) na pia wanahitaji uhakika kutoka kwa mabingwa hao wa La Liga kwamba watamsajili moja kwa moja Mshambuliaji huyo mwisho wa msimu

Majadiliano baina ya vilabu hivyo bado hayajaisha, huku wote wakiwa wanahangaikia kuweza kumaliza usajili huo kabla ya September 2 ambapo ni mwisho wa dirisha la usajili

@habarizamichezo

Sasa yanga sc kivaa zesco united hatua inayofuata

Baada ya klabu ya yanga sc kufanikiwa kushinda mchezo wao wa mkondo wa pili dhidi ya township rollers ….sasa Yanga sc wanakwenda kukutana Na Zesco united kutoka Zambia hatua ya kwanza ya michuano.ya klabu bingwa barani afrika..

…naikumbukwe lwa sasa zesco united inafundishwa Na Lwandamina ambaye aliiwahi kuwa kocha wa yanga misimu.miwili iliyopita ambapo aliiongoza yanga kutwaa ubingwa wa ligi.kuu soka tanzania bara msimu wa 2016/2017
:

Azam..yanga zasonga mbele….kazi kwa simba leo

Azam Fc imetumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kuichapa Fasil Kenema mabao 3-1 na kujihakikishia kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya kombe la Shirikisho

Azam imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2

Yanga nayo imejitutumua kulipa kisasi huko Botswana baada ya kuichapa Township Rollers bao 1-0

Yanga imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza

Kesho ni zamu ya mabingwa wenyewe wa nchi Simba ambao watashuka uwanja wa Taifa kuumana na UD Songo

Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote kesho ili iweze kuungana na Yanga raundi ya kwanza

Hakuna shaka, leo UD Songo wataondoka na kapu la mabao

Baada ya KMC kutolewa, Tanzania bado ina matumaini ya kulinda nafasi zake nne baada ya timu hizo mbili kufanya vizuri, Simba ikisubiriwa kesho

MATOKEO YA SOKA MICHEZO.YA JANA

#EnglandPremierLeague
FT Norwich City 2 – 3 Chelsea
FT Brighton & Hove Albion 0 – 2 Southampton
FT Manchester United 1 – 2 Crystal Palace
FT Sheffield United 1 – 2 Leicester City
FT Watford 1 – 3 West Ham United
FT Liverpool 3 – 1 Arsenal
:
#SpainLaLigaSantander
FT Osasuna 0 – 0 Eibar
FT Real Madrid 1 – 1 Real Valladolid
FT Getafe 1 – 1 Athl. Bilbao
FT Celta Vigo 1 – 0 Valencia
:
#ItalySerieA
FT Parma 0 – 1 Juventus
FT Fiorentina 3 – 4 Napoli
:
#GermanyBundesliga
FT Mainz 05 1 – 3 Borussia Mönchengladbach
FT Augsburg 1 – 1 FC Union Berlin
FT Fortuna Düsseldorf 1 – 3 B.Leverkusen
FT SC Paderborn 1 – 3 Freiburg
FT Hoffenheim 3 – 2 Werder Bremen
FT Schalke 04 0 – 3 FC Bayern München
:
#FranceLigue1
FT Angers 3 – 0 Metz
FT Dijon 0 – 2 Bordeaux
FT Amiens 1 – 2 Nantes
FT Brest 1 – 0 Reims
:
#NetherlandsEredivisie
FT Willem II 2 – 1 FC Emmen
FT Heracles 1 – 1 Vitesse
FT SC Heerenveen 0 – 0 FC Twente
:
#BelgiumFirstDivisionA
FT Cercle Brugge 1 – 0 Waasland-Beveren
FT Oostende 2 – 1 KV Mechelen
FT St.Truiden 0 – 0 Zulte Waregem
:
#SouthAfricaPremierLeague
FT Black Leopards FC 1 – 1 Highlands Park
FT Lamontville Golden Arrow… 2 – 1 Chippa United FC
FT Kaizer Chiefs 1 – 1 SuperSport United
:
#CafChampionsLeague
FT Platinum FC 3 – 2 Nyasa Big Bullets
FT ZESCO United 1 – 0 Green Mamba
FT Township Rollers 0 – 1 Young Africans
FT Primeiro de Agosto 2 – 0 KMKM
FT Al Merreikh 3 – 2 JS Kabylie
FT Mamelodi Sundowns FC 4 – 0 Otôho d’Oyo
FT Etoile du Sahel 7 – 1 Hafia FC
FT Génération Foot 3 – 0 LPRC Oilers
FT El Zamalek 6 – 0 Dekedaha
FT Orlando Pirates 1 – 1 Green Eagles FC
FT Raja Casablanca Atlhletic 4 – 0 Brikama United
:
#CafConfederationCup
FT Azam FC 3-1 Katema
FT Masters Security FC 0 – 0 Proline
FT Rukinzo 0 – 0 Triangle United FC
FT Young Buffaloes FC 1 – 1 Buildcon
FT Malindi FC 1 – 0 Mogadishu City
FT Ashanti Gold 3 – 0 Akonangui
FT CI Kamsar 1-0 Paradou AC
FT CotonTchad 0-2 CR Belouizdad :
#VodacomPrimierLeague
FT: Namungo FC 2-1 Ndanda SC
FT: Mbao FC 1-1 Alliance FC
FT: Polisi Tanzania 1-0 Coastal Union
FT: Biashara United 0-2 Kagera
FT: Mbeya City 0-0 Tanzania Prisons

#SokaPlaceUpdates VPLResult

Design a site like this with WordPress.com
Get started