




















– Zlatan Ibrahimovic amesema Kuwa anafikiria bado yuko vizuri kucheza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, na kwa utani akasema kwamba Manchester United kama inamtaka inajua yuko wapi, wanaweza Kwenda kumsajili tena.. 😁
:
– Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alifunga mara mbili kwenye game ya El Tràfico derby wakati timu yake ya LA Galaxy ikitoka sare ya 3-3 na mpinzani wao Los Angeles FC katika pambano la ligi kuu ya Marekani “MLS”.
.
– Magoli hayo mawili yamemfanya kufikisha mabao 22 katika michezo yote ya ligi msimu huu – pamoja na magoli sita kwenye michezo mitatu iliyopita.. anashika nafasi ya Pili Katika ufungaji, kinara Ni mtani wake na mpinzani wake mkubwa huko Marekani, Si mwingine Ni Carlos Vela akifunga Magoli 27 Mpaka Sasa Akiwa na Los Angeles FC… Zlatan Ibrahimovic raia wa Sweden anaamini fomu yake ya hivi sasa inaonyesha wazi angeshindana tena kwa kiwango cha juu huko England…Ibrahimovic alitumia misimu miwili huko Old Trafford kati ya mwaka 2016 na 2018 na alifunga mara 29 katika michezo 53..
#Updates #MLS
@Sokawaytz

Hizi nizo timu ambazo zimeshiriki Mara nyingi Zaidi Katika hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika tangu 1997..
:
Al Ahly 🇪🇬 16
Esperance 🇹🇳 16
ASEC Mimosas 🇨🇮 11
TP Mazembe 🇨🇩 10
Zamalek 🇪🇬 9
Etoile du Sahel 🇹🇳 8
Enyimba 🇳🇬 7
Al-Hilal 🇸🇩 7
Mamelodi Sundowns 🇿🇦 6
Raja Casablanca 🇲🇦 6
Wydad Casablanca 🇲🇦 5
USMA🇩🇿 5
#CAFCL#TotalCAFCL#CAFCLUpdates










Mshambuliaji wa zamani wa Simba Laudirt Mavugo amesajiliwa na Difaa El Jadida ya Morocco
Kulingana na taarifa iliyotolewa na timu hiyo, Mavugo amesaini mkataba wa miaka miwili. Katika klabu hiyo, ameungana na Watanzania Saimon Msuva na Nickson Kibabage
Msimu uliopita Mavugo aliitumikia Napsa Stars ya Zambia, akiibuka miongoni mwa wafungaji bora wa ligi hiyo
Mavugo aliondoka Simba misimu miwili iliyopita baada ya kutokuwa na mwenendo mzuri katika klabu hiyo
Ni mchezaji mwenye kipaji, lakini pengine alikosa bahati kun’gara kwenye soka la Tanzania

✍️ Hii leo zinapigwa Mechi za Derby Nne tofauti za kukata na SHOKA 🙌!.
:
🏴 North London Derby (Premier league).
18:30 Arsenal v Tottenham.
.
🏴 Glasgow Derby “Old Firm” (Scotland Premiership).
14:00 Rangers v Celtic
.
🇮🇹 Derby Della Capitale “Rome Derby” (Serie A).
19:00 SSC Lazio v AS Roma.
.
🇦🇷 SuperClásico (Argentina Primera Division).
23:00 River Plate v Boca Juniors
#Derbyday #derby
@harunlugoyah

Msafara wa waandishi wa habari za michezo umeanza safari jana kuelekea Nchini Burundi kuipa hamasa Timu ya Taifa ya @taifastars_ kwenye mchezo wa kufuzu kombe la dunia 2022 nchini Qatar dhidi ya burundi mchezo wa kwanza ukichezwa Burundi Septemba 4 na marudio Uwanja wa Taifa Septemba 8,2019.


– Baada ya kuanza vibaya msimu wa Ligi Kuu Nchini England Klabu ya Chelsea chini ya kocha wao Frank Lampard, wanajiandaa kumpokea, Callum Hudson-Odoi anayekaribia kurudi uwanjani Baada ya Kuwa Majeruhi kwa Muda!.
.
– Mshambuliaji huyo wa miaka 18 amekuwa akijiuguza nje ya Uwanja tangu mwezi Aprili kufuatia kupata Majeraha ya mguu wake kwenye mchezo wa sare ya 2-2 dhidi ya Burnley…. Ulikuwa msimu mwingine wa mafanikio kwa Hudson-Odoi, ambaye alifunga mara nne kwenye Ligi ya Europa kwa The Blues walio kwenda kutwaa Ubingwa wa Michuano hiyo katika fainali dhidi ya Majirani zao Arsenal!.
.
–

Baada ya Sare ya 2-2 dhidi ya Sheffield United katika game ya Premier league Jana, Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard Amethibitisha Kuwa Nyota huyo amefanya mazoezi wiki hii na Wachezaji wenzake, na anatarajia kurejea kucheza Uwanjani Baada ya kumalizia kwa mapumziko ya Kimataifa.. Mchezaji mwingine anatarajia kurejea Uwanjani ni beki Mjerumani, Antonio Rudiger Ambaye Nae Alikuwa Ni miongoni mwa Wachezaji Majeruhi..
#EPLUpdates #chelseafc
@sokawaytz_

– Kiungo, Tiemoue Bakayoko wa Chelsea amekamilisha vipimo vya afya na kutia saini kuitumikia Klabu yake ya zamani, Monaco kwa mkopo na Kipengele cha kumnunua kwa €42.5m ($38m / $46m).
.
– Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alijaribu kumshawishi meneja mpya wa The Blues, Frank Lampard katika Maandalizi ya Msimu huu, lakini alishindwa kuleta ubora unaotakiwa ili kurudi kwenye timu ya kwanza ya Blues… Kiungo huyo pia alirejea Kutoka kwa mkopo huko Serie A Katika Klabu ya AC Milan!.
.
– Ikiwa Monaco italipa ada ya €42m mwishoni mwa msimu, itamfanya Bakayoko kuwa Mchezaji wao wa tatu ghali zaidi wa Muda wote, baada ya Radamel Falcao na James Rodriguez tu..
#TransferNewsUpdate
@harunlugoyah

Winga mpya wa Simba, Miraji Athuman amesema anachokipigania kwa sasa ni kuhakikisha kocha mkuu Patrick Aussems anamshawishi ili kupangwa kikosi cha kwanza.
Aussems amekuwa akimpa nafasi mchezaji huyo na mechi yao ya ufunguzi alifunga bao moja, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezaji huyo amesema anatamani kufanya kazi na sio kuwa mchezaji wa kusugua benchi, akidai anaamini nidhamu na juhudi ndivyo vitakavyofanya afikie anachokiwaza.
“Huwa najipa moyo kwamba ninaweza licha ya Simba kuwa na wachezaji wazoefu ambao uwezo wao upo wazi, hilo haliwezi kuninyima raha kwamba nitakuwa sipati namba,” Miraji aliliambia Mwanaspoti
“Mchezaji ambaye ananifanya nijiamini nitaweza kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha kwanza ni Shiza Kichuya alitoka Mtibwa Sugar na akafanya maajabu, hata mimi nitafanya maajabu,”anasema.
Juzi Miraji alifunga moja ya mabao ya Simba kwenye ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania