ZAHERA AKUMBANA NA RUNGU LA TFF

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Septemba 2, 2019 ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2019/2020 iliyoanza rasmi Agosti 24, 2019 na kufanya uamuzi ufuatao;

Mechi namba 9- Yanga 0 vs Ruvu Shooting 1. Mwamuzi Msaidizi Janeth Balama amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria, hivyo kusababisha akatae bao halali lililofungwa na Ruvu Shooting katika mechi hiyo iliyofanyika Agosti 28, 2019 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ametozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi hiyo, kinyume na Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Klabu ya Yanga imepewa Onyo Kali kwa kushindwa kuhakikisha Kocha wake Mwinyi Zahera anaongoza benchi la ufundi la timu yake akiwa katika mavazi nadhifu na ya heshima. Adhabu dhidi ya klabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Mkurugenzi wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametozwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili), kwa kuingia ndani ya uwanja (eneo la kuchezea) baada ya filimbi ya mwisho, kinyume na Kanuni ya 14(10) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefungiwa kuiongoza timu yake katika mechi tatu za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kutoa shutuma na kejeli kwa Bodi ya Ligi katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya Ruvu Shooting. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 41(9) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
#wapendasokaupdates

*RATIBA YA SIMBA 1st ROUND*

1. 29/08/2019 – Uhuru
JKT Tz VS SIMBA

FIFA WEEK (01-10 September)

2. 17/09/2019 -Uhuru
SIMBA VS MTIBWA

3. 22/09/2019 – Uhuru
SIMBA VS LIPULI

4. 03/10/2019 – Bukoba
KAGERA VS SIMBA

5. 06/10/2019 – Uhuru
SIMBA VS PRISONS

FIFA WEEK (07-15 October)

6. 19/10/2019 -Uhuru
KMC VS SIMBA

7. 23/10/2019 – Uhuru
AZAM VS SIMBA

8. 07/11/2019 – Mara
BIASHARA VS SIMBA

FIFA WEEK (11-19 November)

9. 21/11/2019 – Singida
SINGIDA VS SIMBA

10. 24/11/2019 -Uhuru
RUVU VS SIMBA

WEEK YA AZAM FA CUP
20 – 22 December 2019

11. (Itapangwa)- Uhuru
SIMBA VS NDANDA

12. 04/01/2020 -Taifa
*SIMBA VS YANGA*

MAPINDUZI CUP

13. (Itapangwa) – Uhuru
SIMBA VS NAMUNGO

14. 16/01/2020 – Mwanza
MBAO VS SIMBA

15. 19/01/2020 – Mwanza
ALLIANCE VS SIMBA

16. 23/01/2020 Mwadui
MWADUI VS SIMBA

WEEK YA AZAM FA CUP
24 – 26 January 2020

17. 01/02/2020 – Tanga
COASTAL VS SIMBA

18. 04/02/2020 – Moshi
POLICE VS SIMBA

WEEK YA AZAM FA CUP
21 – 23 February 2020

19. 27/02/2020 – Uhuru
SIMBA VS MBEYA CITY

*SIMBA NGUVU MOJA*

Kocha wa Al Ahly SC…kushinda mataji yote ..timu.itakayoshiriki

Kocha mpya wa Klabu ya Al Ahly SC ya nchini Misri Raia wa Uswizi, Rene Weiler, ametambulishwa rasmi na mara akaahidi kushinda Mataji yote ambayo timu hiyo itashiriki… alisema hayo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari Kipindi Cha Utambulisho wake!.
.
– Mabingwa hao wa Misri, walitangaza Jumamosi kuteuliwa kwa Weiler kama kocha mpya wa klabu, Sasa ataanza Kibarua chake kwa Mara ya Kwanza akikabiliana na Mchezo dhidi ya Cano Pillars katika mchezo wa kwanza wa raundi ya 32 ya Ligi ya Mabingwa ya CAF mnamo Septemba 14, na Mechi ya Marudiano itapigwa Misri, wiki mbili baadae!.
#Alahly #Updates #TotalCAFCL
@Harunlugoyah

YANGA YAPELEKA KUBWA KULIKO MWANZA

Uongozi wa klabu ya Yanga umepanga kufanya Tamasha la kubwa kuliko jijini Mwanza keshokutwa Septemba 6 katika uwanja wa CCM Kirumba kwa ajili ya kuchangisha fedha ili kusaidia gharama za timu hiyo.

Kwa mara ya kwanza Tamasha la kubwa kuliko lilifanyika Juni 16 jijini Dar es Salaam ambapo Yanga ilikusanya zaidi ya milioni 900 kutoka kwa wadau mbalimbali wa klabu hiyo.

Kaimu Katibu mkuu wa klabu hiyo, Dismas Ten amesema baada ya Tamasha hilo siku inayofuata walikuwa wacheze mechi ya kirafiki dhidi ya Mbao FC lakini mchezo huo hautafanyika isipokuwa watacheza na Pamba FC.

Baada ya mchezo huo Septemba 9 watacheza mechi nyingine ya kirafiki ambayo bado haijathibitishwa huku wakiwa kwenye mazungumzo na Gwambina FC kwa ajili ya mchezo huo. “Tutafanya Tamasha la kubwa kuliko jijini Mwanza kama ilivyokuwa hapa Dar es Salaam na tutacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Pamba FC,” alisema Ten.

Kikosi cha timu ya Yanga kitasafiri kesho kuelekea Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa hatua ya kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Zesco utakaofanyika Septemba 14 katika uwanja wa Taifa.

#wapendasokaupdates

ABALORA, CHIRWA WAPUMZISHWA AZAM

Wachezaji wawili wa Azam FC mlinda mlango Razak Abalora na mshambuliaji Obrey Chirwa wamepumzishwa katika mazoezi ya siku ya jana baada ya kupata maumivu machache kwenye mechi ya kirafiki.Juzi

Azam ilishuka dimbani katika uwanja wa Uhuru kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Maafande wa Transit Camp ambapo ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1.Kocha msaidizi wa Azam, Idd Cheche amesema wachezaji hao walipata maumivu kidogo ndio maana wamepumzishwa ili waweze kupona vizuri.

“Abalora na Chirwa hawajafanya mazoezi ya jioni kwakua walipata maumivu kidogo kwahiyo tumewaacha kwanza ili wapone kabisa ili wakirudi uwanjani wawe fiti,” alisema Cheche.Azam inajiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza ya kombe la Shirikisho watakao cheza dhidi ya Triangle ya Zimbabwe ambao wataanzia nyumbani wiki mbili zijazo.@azamfcofficial
#wapendasokaupdates

Mashabiki mwanza kuipokea yanga kea shangwe

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa kaimu katibu mkuu, Dismas Ten umesema kuwa ziara ya timu yao jijini Mwanza imeratibiwa na wanachama wa klabu hiyo waishik huko na tayari wametuma tiketi za ndege kwa ajili ya wachezaji na benchi la ufundi.

Aidha, Ten amesema kuwa pamoja na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco, ziara hiyo pia itahusisha tukio linalofanana na lile la ‘Kubwa Kuliko’ lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuichangia klabu hiyo.

Tukio hilo ambalo pia limeratibiwa na wanachama wa Mwanza, linatarajiwa kufanyika mnamo Septemba 6.

#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started