




















Vikosi Vinavyoanza @chelseafc vs @liverpoolfc



️ Kikosi Cha Yanga SC kuondoka Nchini Siku ya Jumanne September 24 kuelekea Zambia na Jumla ya Wachezaji 22 na Benchi la Ufundi la Watu Saba likiongozwa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera… Yanga inaenda Zambia kwa Ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Wenyeji wao, ZESCO United.
#CAFCL #TotalCAFCL


#EnglandPremierLeague
FT Crystal Palace 1 – 1 Wolverhampton Wanderers
FT West Ham United 2 – 0 Manchester United
#sokaplaceupdates



Timu ya Tanzania bara wameanza vyema Mashindano ya Cecafa ya Vijana U-20 yanayoendelea nchini Uganda 🇺🇬 baada ya kushinda 4-0 dhidi ya Ethiopia kwenye mchezo wao wa kwanza kundi B uliochezwa saa 7:00 kwenye uwanja wa Njeru hapa Jinja.
Mabao ya Tanzania bara yamefungwa na Kelvin John (Mbappe) dakika ya18 na
Andrew Simchimba (pichani) amefunga hatrik dakika 38, 49 na 85.
Saa 10:00 utaendelea mchezo mwengine kiwanjani hapo kati ya Zanzibar vs Kenya 🇰🇪.

Rais Magufuli ametoa shilingi milioni 10 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu inayojiandaa kushiriki mashindano ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Afrika (CANAF) yaliyopangwa kuanza tarehe 01 Oktoba, 2019 katika Mji wa Benguela nchini Angola.
.
.
Katibu wa Rais, Ngusa Samike amekabidhi fedha hizo kwa viongozi na wachezaji wa timu hiyo leo tarehe 22 Septemba, 2019 katika studio za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambalo limekuwa likitangaza taarifa za timu hiyo kuomba msaada ili ifanikishe safari ya kwenda kushiriki katika mashindano hayo.
.
.
Samike amewasilisha ujumbe wa Rais Magufuli ambaye amewapongeza viongozi na wachezaji wa timu hiyo kwa dhamira yao ya kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo na amewatakia heri na ushindi. .
.
“Kwa watu wenye ulemavu kushiriki michezo pia ni tiba, kwa hivyo nawapongeza kwa kushiriki michezo na mashindano haya naamini jamii itaendelea kutilia mkazo walemavu kushiriki michezo” amesema Samike. .
.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi na Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Ulemavu Hamad Komboza wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kutoa msaada huo na kwa kuendelea kuwatambua na kuwathamani watu wenye ulemavu. .
.
Wamesema timu hiyo yenye wachezaji 13, walimu 5 na viongozi 2 itaondoka tarehe 28 Septemba, 2019 kuelekea nchini Angola ambako inakwenda kushiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza na wameahidi kufanya vizuri.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard kasesela amefunguka kuwa yeye ni Shabiki wa kutupwa wa Haji Manara
Kasesela amesema kuwa klabu ya simba inabahati sana kumpata mtu kama haji manara kwani anaufundi mkubwa sana katika kuwamudu watani zao wa jadi.
Kasesela amesema kuwa Yanga ilibahatika kumpata afisa habari machachari sana @jerrymuro1980 ambaye alikua anaweza kupambana na haji Manara.
@hajismanara @simbasctanzania

Matokeo ya michuano ya CECAFA U20


Kagera Sugar imewaondoa Simba kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao Fc
Ushindi huo umeifanya Kagera Sugar ifikishe alama tisa baada ya kushinda michezo yake yote mitatu
Simba, mabingwa watetezi walikuwa wakiongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kufunga
Simba haikushuka dimbani wikiendi hii kutokana na wachezaji wake wengi kuitwa timu ya Taifa kuelekea mchezo dhidi ya Sudan hapo leo
Mchezo unaofuata ni dhidi ya hao hao Kagera Sugar, Septemba 26 dimba la Kaitaba mkoani Kagera