Mambo yaliyo gundulika …simba sc vs kagera

Mambo kadhaa niliyogundua kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba. .
.
Kagere, wakiwa washambuliaji wao walikuwa wakicheza 4-4-2 na washambuliaji wawili mbele pale mpira wanapopoteza au kushambuliwa wao walikuwa wakitumia mfumo wa 4-5-1 kwa kujilinda zaidi.
.
.
Awesu, kijana mdogo mwenye vitu kibao mguu naweza kusema kwenye mchezo wa leo kwa upande wa Kagera Sugar, ameonyesha uhai mtulivu anapiga pasi fupi ndefu lakini kulikuwa na utofauti na viungo wa Simba, walikuwa wakicheza kitimu. .
.
Kagera walijiamini sana katika uwanja wa nyumbani kwa sababu historia ilikuwa inawabeba wakasahau ubora wa Simba ,kwenye uwezo wa mchezaji moja moja.
.
.
Ile pitch ya Kaitaba, nimeielewa sana mpira unatulia chini mpira ukipiga inafika sehemu husika ila ni mdogo sanaπŸ€”.
.
.
Santos, what man πŸ™Œ akupi nafasi ya kugeuka ana hakikisha mpira yote ya hewani ni yake huyu sio Mbrazil, ni Mjerumani mwenye roho kama ya Adolf Hitler πŸ’ͺ.
.
.
Simba, waliamua kumaliza mechi ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza walifahamu ugumu wa uwanja huo wa Kaitaba.
.
.
Rudi kwenye ile mechi ukipata mda rudia ile pasi ya Shiboub, kutika ya uwanja, mpaka kumfikia Mohamed Hussein, na kufunga zile huwa tunasema tigo pesa,amenikumbusha ubora wa Lampard, Scholes, Gerrard na Schweinsteiger πŸ‘.
.
.
Deo Kanda, badae anaweza akawa CD, ana maamuzi ya haraka kwenye, nimeona utofauti leo wa Miraji na Kanda, akae chini na kujitafsiri. .
.
NB, mwenye namba ya Mecky Mexime, anipe kuna swali nataka nimuulize kwa nini alimuacha nje Juma Nyoni, na kumuingiza kipindi cha pili.
.
.
@azizi_mtambo_15 wa @sokaplace__

Antonio Conte..aweka rekodi mpya.series A

– Kocha Mkuu wa Inter Milan, Antonio Conte aliweka rekodi mpya ya klabu kwa kuwa kocha wa kwanza wa Inter kushinda mechi zake tano za kwanza za Serie A baada ya kuiongoza Klabu hiyo katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lazio Jana.
..
– Nerazzurri waliendeleza mwanzo wao mzuri wa msimu huu kwa Goli Pekee la kichwa cha Danilo D’Ambrosio katika kipindi cha kwanza huko San Siro, Milan…. Ushindi huo wa Jumatano umeendelea kuiweka Inter juu ya Juventus kileleni mwa ligi, pointi 15 kwa Inter hadi sasa…
….

– Conte, ambaye alichukua Mikoba ya kuinoa Inter Milan kutoka kwa Luciano Spalletti, alitwaa mataji matatu mfululizo ya Serie A wakati alipokuwa Kocha Mkuu wa Juventus… Bosi huyo wa zamani wa Chelsea na Italia sasa anawania Ubingwa wa Scudetto akiwa n Inter, ambao Wana ukame wa kulitwaa Ikiwa Mara yao ya mwisho walitawazwa Mabingwa mnamo Msimu wa 2009-10..
#Inter #InterMilan #SerieA
@Harunlugoyah

Nahodha timu ya Taifa U17 Issa Makamba (19)..kwenda kukipiga misri

Nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki michuano ya AFCON U-17 nchini Gabon, Issa Makamba (19) anatarajiwa kutimkia Israel mwishoni mwa wiki hii baada ya kupata timu ya kucheza soka la kulipwa

Imeripotiwa kuwa anaenda Israel kufanya majaribio katika klabu ya Kiryat Shmona FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Israel na kama akifanya vizuri atasalia katika kikosi hicho

Hata hivyo, licha ya Makamba kuwa nahodha wa Serengeti Boys katika michuano ya AFCON U 2017 hakupata nafasi ya kucheza mchezo hata mmoja kufuatia kuvunjika mguu siku mbili kabla ya kuanza kwa mashindano

RATIBA YA SOKA LEO.

KAMATA RATIBA YA SOKA LEO.
#VodacomPrimierLeague
16:00 Lipuli Fc vs Mbeya City
16:00 Kagera Sugar Vs Simba Sc :
#SpainLaLiga
20:00 Eibar vs Sevilla
21:00 Celta Vigo vs RCD Espanyol
22:00 Real Sociedad vs Deportivo Alaves
:
#ItalySerieA
22:00 Torino vs Milan
:
#BelgiumBekerVanBelgie
21:30 Royal Antwerp vs Lokeren
21:30 Standard Liege vs Lommel

Imeandaliwa na @officialchristz wa @sokaplace__

CHELSEA VS MAN UNITED; LIVERPOOL VS ARSENAL CARABAO CUP.

Droo ya hatua ya 16 bora katika michuano ya kombe la Ligi maarufu kama Carabao Cup pale England imefanyika muda mchache baada ya mechi za mzunguko Wa Tatu.

Chelsea baada ya kuiadhibu Grimsby Town Football Club kwa jumla ya mabao 7-1 imepangwa kukutana na Manchester United katika hatua inayofata. United ambayo imepita baada ya kushinda kwa Penati 5-3 dhidi ya Rochdale AFC.

Mabingwa watetezi Manchester City wao wamepangwa kucheza dhidi ya Southampton mechi itakayopigwa katika uwanja Wa Etihadi.

Liverpool baada ya uahindi Wa bao 2-0 dhidi ya MK Dons sasa watacheza mechi yao inayofata dhidi ya Arsenal mchezo utakaochezwa Anfield.

Mechi za hatua ya 16 bora zitachezwa wiki inayoanzia Oktoba 28

RATIBA KAMILI YA MICHUANO HIYO HII HAPA

#wapendasokaupdates
#carabaocup

Design a site like this with WordPress.com
Get started