
Genk XI
: Coucke; Maehle, Cuesta, Lucumí, Uronen; Bongonda, Berge, Heynen, Ito; Samatta; Onuachu
Liverpool XI
: Alisson; Milner, Van Dijk, Lovren, Robertson; Fabinho, Keita, Oxlade-Chamberlain; Salah, Firmino, Mané.
#UCL

Genk XI
: Coucke; Maehle, Cuesta, Lucumí, Uronen; Bongonda, Berge, Heynen, Ito; Samatta; Onuachu
Liverpool XI
: Alisson; Milner, Van Dijk, Lovren, Robertson; Fabinho, Keita, Oxlade-Chamberlain; Salah, Firmino, Mané.
#UCL

Kabla ya mchezo dhidi ya Azam Fc leo, winga Miraji Athumani ‘Sheva’ alikabidhiwa zawadi yake baada ya kuibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi wa tisa
Amekabidhiwa kitita cha Tsh Milioni Moja pamoja na kin’gamuzi cha Azam TV
Kocha Patrick Aussems nae aliibuka kuwa kocha bora wa mwezi wa tisa

Nani wa kuizuia Simba msimu huu? Ni swali ambalo timu za ligi kuu zinajiuliza kutokana na moto walioanza nao mabingwa hao watetezi leo wakiichapa Azam Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Wakicheza kwa kujiamini katika mchezo huo uliotawaliwa na ufundi mwingi pamoja na ubabe wa hapa na pale, alikuwa Meddie Kagere aliyepeleka kilio Chamazi kwenye dakika ya 49 akimalizia kwa kichwa krosi murua iliyochongwa na Francis Kahata

Pamoja na mashabiki kutoridhishwa na kasi yake kwenye kipindi cha kwanza, Kahata alionekana katika wakati muafaka akitengeneza bao hilo muhimu
Kagere ameendeleza rekodi yake ya kufunga katika kila mchezo sasa akifikisha mabao saba

Hakuna shaka kwa mwendo alionao, Kagere anaweza kufunga mabao zaidi ya 30 msimu huu ikiwa ni ahadi aliyoiweka mwanzoni mwa msimu
Ushindi huo ni wa tano mfululizo kwa Simba ambayo imefikisha alama 15 na kuendelea kujikita kileleni
Matokeo ya mechi zote zilizopigwa leo


Harry Kane alifunga hat-trick yake ya kwanza kwa Tottenham…na kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka akacheza nafasi ya golikipa
Kipa Hugo Lloris alitolewa kwa kadi nyekundu wakati wa mechi hii ya Europa League, Kane aliyekuwa amefunga hat-trick kwenye mchezo huo, alilazimika kuvaa jezi ya kipa na kuingia langoni katika dakika za mwisho za mchezo kutokana na Spurs kuwa wametumia nafasi zao zote za kufanya mabadiliko uwanjani.
Leo katika dimba la Maraçana pale nchini Brazil itapigwa mechi ya mkondo wa pili kati ya Gremio na Flamengo kuwania kutinga katika hatua ya fainali ya kombe la Copa libertadoes ili kumpata atakaeiwakilisha Amrika kusini katika kombe la Dunia la klabu litakalofanyika pale Qatar mwezi disemba!.
.
Mchezo wa awali kati ya Vigogo hawa wa nchini Brazil walitoka sare ya 1-1 Flamengo wakiwa nyumbani!.
.
Achana na ndugu zake Neymar pale kwa akina ‘Magician’ Leo Messi ilipigwa Superclassico Derby pale nchini Argentina kati ya River Plate na Bocã Juniors pale Estadio J.Alberto Armando uwanja wa the Blue and gold.
.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza katika dimba la El monemental Boca Junior walikufa 2-0 pale Buenois Aires!.
.
Katika hali ya kushangaza Watoto wa La Boca karibu na jiji la Buenois Aires the Blue and Gold wakiwa chini ya nahodha Carlos Tevez,Tevez yule aliesumbua wakati yupo West Ham ,Man utd,Man city na Juventus alishindwa kuwafanya Boca watinge fainali goli la Jioni la Hurtado halikuweza kupindua meza kibabe!.
.
Tevez akili bado inautaka mpira lakini mwili unakataa kabisa kufanya kile akili inataka!muda umemtupa mkono sasa!.
.
SuperClassico derby ni mchezo unaokuwa na mambo mengi ya furaha,karaha na hata kuhatarisha maisha kutokana na jinsi mashabiki na wapenzi wa klabu hizi mbili wanazifanya timu zao kuwa zaidi ya maisha!.
.
Iwe pale Armando au Monumental hali huwa ni ileile spirit ya kuhamasisha na kuhanikiza ushindi haibadiliki kamwe!!Fire works huwa ndo mahala pake ikishafika katika superclasico barabara za mitaa hufungwa!.
.
Fainali ya kumpata mwakilishi wa shirikisho la Amerika kusini katika kombe la dunia la klabu itafanyika tarehe 23 novemba 2019 pale nchini Chile katika dimba la Nacional katika jiji la Santiago!
.
.
Prepared by @anode360 Sponsored by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates
.
Klabu ya Yanga Sc imethibitisha kuwa mshambuliaji wake Maybin Kalengo atakuwa nje kwa muda wa wiki nane hadi 12 baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa leo wa kirafiki dhidi ya Pamba Sc ya Mwanza
.
.
Get well soon Kalengo
.
Sponsored by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo saa kumi na moja jioni watashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Azam Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu
Hiki hapa kikosi kitakachoanza;


Mtanzania Mbwana Samatta akiwa nahodha wa KRC Genk, leo ataiongoza timu yake kuikabili Liverpool, mabingwa wa Ulaya kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa
Samatta ambaye ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushiriki michuano hiyo na kufunga bao, amesema ni heshima kubwa kwake kupata nafasi ya kukiongoza kikosi cha Genk kwenye mchezo huo
Aidha amesema kucheza na Liverpool sio jambo dogo, ni kumbukumbu ambayo itabaki katika historia yake
Akiungumzia mchezo huo, Samatta amesema watahakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya wababe hao wa soka la Ulaya hasa ikizingatiwa wanacheza kwenye uwanja wao wa nyumbani
Mchezo uliopita, Genk ilitoka suluhu ya bila ya kufungana dhidi ya Napoli

Wakati mabingwa watetezi Simba wakitarajiwa kushuka dimba la Taifa leo saa 11 jioni kuikabili Azam Fc, nyasi za viwanja vingine sita, zinatarajiwa kuwaka moto kwa michezo mbalimbali kupigwa
Ukiondoa mchezo wa Simba dhidi ya Azam Fc, mechi nyingine zote zinatarajiwa kupigwa kuanzia saa kumi jioni


Wakati Azam FC imetangaza kuachana na Etienne Ndayiragije, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa bado halijakamilisha mchakato wa kupata Kocha Mkuu mpya atakayekinoa kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars)
Rais wa TFF, Wallace Karia, alimesema hayo juzi na kuongeza kwamba bado wanasubiri ripoti ya Taifa Stars kutoka kwa Ndayiragije, ambaye amefanikiwa kuipeleka kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).
Karia alisema kuwa Watanzania hawapaswi kuwa na haraka juu ya uamuzi wa kocha mpya kwa sababu jambo hilo hutekelezwa kwa umakini.
Kiongozi huyo amekanusha uwepo wa taarifa kuwa TFF inatarajia kumpa mkataba rasmi kocha huyo, baada ya kuachana na klabu ya Azam FC.
“Nawaomba Watanzania wawe na subira, sisi bado hatujamtangaza kocha mpya wa Stars, Watanzania wanapaswa kuwa na subira, kama Azam walisema ni wao na si sisi, subirini,” alisema Karia.
Aliongeza kuwa bado wanaendelea kupokea maombi kutoka kwa makocha mbalimbali, na mara baada ya mchakato huo kukamilika, wataweka wazi mrithi wa Mnigeria Emmanuel Amunike.