
Usiku wa jana Mtanzania Mbwana Samatta aliiongoza klabu ya KEC Genk kuikabili Liverpool kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya
Haukuwa usiku mzuri sana kwa Genk iliyokubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa mabingwa hao wa Ulaya
Watanzania wengi waliushuhudia mchezo huo kupitia runinga zao
Samatta alifanikiwa kufunga bao lakini waamuzi wa VAR walilikataa katika mazingira ya kutatanisha
Kumekuwa na mjadala ambapo baadhi ya wachambuzi nguli duniani wameshangazwa na kukataliwa kwa bao hilo
Nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingereza Gary Leneker ambaye sasa anafanya kazi kituo cha televisheni cha BT Sports ni miongoni mwa walioshangazwa na kukataliwa kwa bao hilo


Mfululizo wa kupachika Magoli muhimu kwa Timu ya Taifa ya England na Klabu yake ya Man United hivi karibuni kwa msimu huu wa 2019/2020 imemtambulisha upya kinda Marcus Rashford Kama mmoja ya Nyota vijana wakutazamwa Sana katika Soka Ulimwenguni kwa Sasa. .
















