BAADA YA KIPIGO CHA GOLI 4 KWA 1 MASHABIKI WA MBEYA CITY WALIA NA MWAMBUSI PAMOJA NA KIMBE

Ligi kuuu Tanzania bara iliendelea jana Jijini Mbeya ,Mbeya City waliwakaribisha wanatamu tamu Kagera Sugar kutoka Kagera
:
Mchezo huo ulimalizika kwa Mbeya City kupokea kichapo kizito cha Goli 4-1 kutoka kwa Vijana hao wa Kagera Sugar.
:
Baada ya kichapo hiki Mashabiki wa klabu ya Mbeya City wamesema wamechoshwa na Matokeo kufungwa huku wakimtaka Kocha Juma Mwambusi Pamoja na Emmanuel Kimbe kuwaachia timu yao
:

Mashabiki hao wamesema kuwa Wamechoka kuchekwa mtaani wao hawataki kupigania kushuka Daraja wanataka kushika nafasi za juu katika ligi kuu Tanzania Bara
:
Baada ya Mchezo huu @sokaplace_
ilizungumza na kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi ,Mwambusi alikiri kuwa ni matokeo mabaya kwake na kwa wanambeya kwa Ujumla huku akisema bado kunatatizo katika safu yake ya Ulinzi
:
Naye Emmanuel Kimbe katibu wa klabu ya Mbeya City amesema kuwa mashabiki waache kulalamika wawaachie uongozi kila kitu kitaenda sawa kwani huu umekua mwanzo hivyo anaamini kuna mabadiliko yanakuja katika kikosi chao cha Mbeya City.

#vplupdates🇹🇿 #sokaplaceupdates

Tiketi za mchezo wa Yanga Sc dhidi ya @pyramidsfc zitaanza kuuzwa leo

Tiketi za mchezo wa Yanga Sc dhidi ya @pyramidsfc zitaanza kuuzwa leo Ijumaa kwenye vituo vifuatavyo
:
Nyamagana
Nyegezi Bus stand
Buzurugwa shule ya Msingi
Igoma Stand
Ccm Kirumba
Lenana Hotel Pasiasi
Posta Pamba Road
Mkolani
Busweli Petrostation

Powered by @bikotanzania

Man U yashinda kwa Mara ya,kwanza,ugenini tangu march 10

✈️Manchester United imeshinda mechi yao Ugenini kwa mara ya kwanza Tangu March 10, imefunga goli Ugenini kwa mara ya kwanza Tangu Agosti 31 ✈️

📌 Walishinda mechi 9⃣ za kwanza Ugenini chini ya Solskjaer.
📌 Wameshinda mechi 1⃣ kati ya game 12 zilizopita za Ugenini chini ya Solskjaer…

– Goli Pekee la Penati kutoka kwa Anthony Martial linawafanya The Red Devils kuibuka na Ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Partizan Belgrade katika Michuano ya Europa League…

– Takwimu za @AnthonyMartial akiwa na Man Utd msimu huu.
⚽️v Chelsea
⚽️v Wolves
🅰️v Crystal Palace
⚽️v Partizan Belgrade
#EuropaLeague #ManUtd
@Harunlugoyah

Nicolas Pépé ndiye mchezaji wa kwanza kufunga Magoli mawili ya free kick ya moja kwa moja

2 – Nicolas Pépé ndiye mchezaji wa kwanza kufunga Magoli mawili ya free kick ya moja kwa moja kwenye mchezo wa Europa League… Mchezaji wa mwisho kufanya kama hivyo ni Luis Suárez akiwa na Liverpool dhidi ya Zenit St. Petersburg, ilikuwa ni February 2013.
#EuropaLeague #Arsenal #UEL
@Harunlugoyah

Kagere kuendeleza rekodi yake mpaka mwisho wa msimu?

#MICHEZO Pengine inaweza ikawa ni rekodi mpya ya Ligi Kuu soka Tanzania bara na kwa mshambuliaji Meddie Kagere. Msimu huu amefunga goli katika mechi zote 5 za ligi ambazo Simba imecheza mpaka sasa.

JKT Tanzania ⚽⚽
Mtibwa ⚽
Kagera ⚽⚽
Biashara ⚽
Azam FC ⚽

Unadhani atamaliza na magoli mangapi msimu huu?

MAGORI KUMSHAURI MWENYEKITI WA BODI SIMBA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba Mohammed Dewji amemteua aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Crescentius Magori kuwa mshauri wake binafsi kuanzia jana Jumatano Oktoba 23, 2019.

Kwa mujibu wa taarifa ya uteuzi huo iliyotolewa leo na Uongozi wa Simba, Magori atakuwa na jukumu la kumshauri Dewji mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji ambao utaiwezesha klabu hiyo kupata mafanikio zaidi.
.
.
“Kwa niaba ya Wanasimba, tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya tukiamini kwamba atatoa msaada mzuri kwa klabu ambao utatuwezesha kupiga hatua kubwa na hasa kutokana na uzoefu wake mkubwa kwenye soka”, imeeleza sehemu ya taarifa ya Simba.

Magori amewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF, Mjumbe Kamati ya CAF ya Soka la Ufukweni na Futsal, Mjumbe wa Kamati ya CECAFA, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Mwenyekiti wa Fedha na Mipango wa TFF na Mjumbe wa Kamati za Masoko wa TFF.
#kwako_mwalim_kashasha

PYRAMIDS WASHINDWA KUFIKA MWANZA

✍na saboso Gin jr
>Timu ya Pyramids Kutoka nchini Misri iliyokuwa inatarajia kufika Mwanza leo saa 2 usiku imeshindwa kufika Mwanza Kutokana na hitilafu ya Ndege yao.

>Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mwanza Leonard Malongo amethibithisha kupokea taarifa hizo Kutoka kwa Afisa Mashindano wa TFF Baraka Kizuguto kuwa hawatafika leo hadi kesho saa sita mchana.

“Ni kweli hawaji leo, watakuja kesho saa sita mchana kwa sababu Ndege yao imepata breakdown, hivyo watakuja kesho”

>Kwa upande wa Yanga, Afisa wa Habari wake Hassan Bumbuli Naye amethibithisha kuwa Pyramids wameshindwa kufika leo Mwanza mpaka kesho na watafikia hotel ya Malaika Hotel Mwanza.

MIWANI YANGU: GERSON FRAGA VIERA MZUNGU MWENYE DAMU NYEUSI

NA MESHACK MELELE

Johan Cruffy mmoja ya watu walioupa maana mchezo wa soka, akiwa kama mchezaji na pia kama Kocha, yote tunayoyaona pale Barcelona yalianzia katika kichwa hichi, alijua mpira unataka nini akaupatia, mauti yalimfika mwaka 2016 alilala bila kuamka katika kitanda chake pale Barcelona catalunya.

Kabla hajamaliza pumzi zake pale Barcelona alishawahi kutamka siri ya mafanikio akiwa uwanjani alitamka maneno machache tu, there is only one ball, so you need to have it alimaanisha kwamba kuna mpira mmoja uwanjani, hakikisha unakuwa nao, sikuelewa nini alimaanisha mpaka pale nilipomuona Gerson Fraga.

Gerson Fraga Viera mchezaji mwenye asili ya kibrazil katika uzi wa Simba, akicheza katikati ya dimba la uwanja wa taifa uchezaji wake walau unatupa maana ya maneno aliyotuachia gwiji wa soka Johan Cruffy katika ardhi yetu ya Tanzania, anajua silaha kubwa ya mchezo wa soka ni mpira wenye uzito wa gramu 450g.

Kupitia yeye unaiona Simba inavyocheza katikati anajua kuituliza timu kutokana na ubunifu alionao, control zake pale anapokuwa na mpira haikufanyi kuwa na shaka kuamini ametokea nchi moja na wachezaji kama Fernandinho

Fraga technical master wa Simba uwanjani , pasi zake makini zinaifanya Simba kusogea zaidi mbele, kwa namna anavyozipiga anainua macho juu kisha anatizama wapi pasi iende taratibu anapiga kama hataki, anakufanya umtizame tena

Unyumbulifu wake wa mpira licha ya kuwa na urefu wa futi 5’11” unaridhisha pia kwa namna anavyozidi kupata nafasi ya kucheza, ana maamuzi ya haraka, anajua wapi apige wapi asipige ni mtunzi wa mipango ya Simba inayokufanya kutojutia kuitoa mia tano yako kuitizama kibanda umiza.

Ukabaji wake unanifanya kuwa na wasi wasi na damu yake, sidhani kama ana damu ya wazungu, anakaba haswa, ana ubabe ambao kiungo yoyote makini anatakiwa kuwa nao.

Kwa karibu unaziona chembembe za Claudio makelele katika miguu yake huko ubabe wake ukitukumbusha jeuri aliyokuwa nayo Gennaro Gattuso pale San Siro ulikua huwezi kuchukua mpira kirahisi rahisi.

Fraga movements zake zinamfanya kiungo anaecheza nae kurelax na kuwa mbunifu, anajua sana kucheza na timing, anarudi chini kisha anamfanya Mzamiru Yassin kucheza katika space kwa ufree, huku yeye akihakikisha anatengeneza shield cover nyuma yake.

Yote hayo yananifanya niende Brazil kwa hisia nambiwa huyu enzi akiwa mdogo alicheza timu za vijana za taifa za Brazil ngazi karibia zote timu ya under 15, under 17, na under 20, katika timu ya taifa ya under 17 alikua nahodha wao, amecheza na watu kama Douglas Costa anayecheza Juventus kwa sasa.

Akiwa kijana mdogo alianza safari yake ya soka katika klabu ya Gremio, sehemu ambayo mfalme wa soka la pasi za kuvutia Ronaldinho alipita pale mwishoni mwa miaka ya 90.

Huyo ndo Gerson Fraga Viera anaekufanya umtizame yeye kwanza kisha utizame mpira, anajua stadi za mpira haswa, soka tamu lenye uzuri wa princess diana analiweza, bado shoo za kibabe za kuchafua roho na viungo wasumbufu ni mziki mwingine.

Ukikutana nae mwambie asante kwa kukubali kuja Tanzania kwa kuja kwake, tumeona maana ya maneno ya Johan Cruffy, Asante sana Gerson Fraga Viera.

Joto.la.panda niyonzima.kurejea tanzania

Kwa mujibu wa Waandishi wa habari wa Rwanda na Mashabiki wa Haruna Hiyonzima wamesema Haruna anaipenda Tanzania kuliko nchi Yake.

Baada ya kuachana wananchi Yanga Sc na Simba Sc hatimae kujiunga na As Kigali hajaifungia Bao lolote wala kutoa pasi ya Mwisho Assist.

Mwandishi huyo wa Rwanda amesema ” Haruna hapa Rwanda hatuoni sifa zake kwa sababu yeye haisaidii timu katika goal creation. hawezi kufunga na hawezi kufanya assist”

Hakuishia Hapo akasema Haruna Niyonzima toka aoneshe makali yake katika ardhi ya Rwanda ilikuwa Mwaka 2009 alifanikiwa kufunga bao katika mashindano ya CECAFA.
#kwako_mwalim_kashasha

Design a site like this with WordPress.com
Get started