Rasmi kampuni ya nike kutengeneza jezi za liverpool

Rasmi leo kampuni ya Nike ndio itakayo husika na utengenezaji wa jezi za Liverpool 2020/2021

New balance waliweka pingamizi mahakamani kuwa kwenye mkataba walioingia kuna kipengele ambacho kilikuwa kuwazuia Liverpool kuingia mkataba na kampuni nyingine pasipo kuwashirikisha wao hata kama kampuni wanayo ingia nayo mkataba itatoa dau kubwa kuwazidi new balance,

Leo ndio walipelekwa mahakamani muda mfupi uliopita na Nike ndio wameshinda 🔥🔥🔥
Awali new balance alikuwa anatoa dau la 45m wakati Nike wameweka 70m

Asante new balance kwa muda mliotumika mmetutoa mbali tunawashukuru saiv liver pool inahitaji kampuni yenye ushawishi wa kibiashara zaidi.

Hakuna mchezaji tutamtaka akakataa 🔥🔥🔥🔥🔥 YNWA

Vilabu vya ulaya kutoshiriki Klabu ya Bingwa ya Dunia. .

.
China 🇨🇳 watakuwa wenyeji wa mashindano yenye mfumo mpya ya Klabu Bingwa ya Dunia mwaka 2021, huku Rais wa FIFa Gianni Infantino akiyaelezea mashindano hayo kama ‘mashindano ya kweli kabisa ya klabu bingwa ya dunia.’
.
Mashindano hayo ambayo kwasasa yanahusisha timu 7, sasa yataanza kuhusisha timu 24 kutoka June 2021.
Vilabu vikubwa vya bara la ulaya vimeshasema huko nyuma kwamba vitasusia mashindano hayo.
.
“Mashindano haya mapya – yatakuwa na ushindani ambao kila mpenda soka atavutiwa nayo.”
.
Qatar watakuwa wenyeji wa mashindano mawili ya mwisho yatakayohusisha timu 7. Mashindano hayo kwa mwaka huu yataanza mnamo December 11 – mabingwa wa ulaya Liverpool wakianzia hatua ya nusu fainali wiki moja baadae. .
Mnamo mwezi March, Chama cha vilabu vya soka vya ulaya (ECA) kilieleza kutoridhishwa na mfumo mpya wa mashindano ya dunia.
Wajumbe wa bodi ya ECA, akiwemo CEO wa Manchester United Ed Woodward, walisaini barua ya pamoja wakipinga juu ya mabadiliko ya mfumo mpya wa Club World Cup, wakisisitiza hakuna klabu ya ulaya itakayoshiriki kwenye mashindano hayo pindi yatakapoanza rasmi.

Patashika leo league 1 monaco akiwa ugenini

MECHI KALI LIGUE 1 🔥🔥 ⚽ Nantes vs Monaco
⌚ 3:45 usiku
🏟 Beaujoire
📺 Sports Premium

Nantes leo hii atamkaribisha Monaco kwenye uwanja wa Beaujoire katika mchezo wa raundi ya 11 Ligi kuu Ufaransa- Ligue 1

The Canaries (Nantes) wameanza vyema msimu huu na wanashika nafasi ya Pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 19, nyuma ya mabingwa Paris SG

Monaco hadi sasa wanashika nafasi ya 14 wakiwa na pointi 12, lakini mechi zao zimekuwa nzuri kutazama kwani kumekuwa na idadi kubwa ya mabao (wastani wa goli 4 kwa kila mchezo)

Hakuna sare iliyopatikana katika mechi sita zilizopita kati ya timu hizi mbili. Monaco ameshinda michezo mitano, ikiwa ni pamoja na mechi tatu zilizopita

Kupitia chaneli ya St Sports Premium Lipia Sasa UHURU-Antenna(Tsh18000) TU! Na SMART-Dish(Tsh21000) TU.. Kufurahia kabumbu mwezi mzima.
Pia unaweza cheki kupitia app ya #Startimeson link kwenye bio ya @startimestz
#MpiraPasimpiraGoli
#ligue1onstartimes
#startimespekee

LIGI YA WANAWAKE KUANZA KESHO

Ligi kuu ya Wanawake ‘Serengeti Lite Primear League’ itaanza kesho kwa timu zote 12 kushuka dimbani katika viwanja tofauti.

Ligi hiyo itachezwa kwa utaratibu wa mechi za nyumbani na ugenini kama ilovyokuwa misimu iliyopata.

Msimu uliopita mabingwa wa ligi hiyo walikuwa JKT Queen’s wao wamepangwa kuanzia ugenini kwa kucheza na Baobab Queen’s.

Mwenyekiti wa soka la Wanawake, Amina Karuma ameomba wadhamini waendelee kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili kuongeza ushindani kama ilivyo kwa upande wa wanaume.

Ratiba kamili kwa mechi zitakazo chezwa kesho

Mlandizi Queen’s vs Panama Girls
Simba Queen’s vs Ruvuma Girls
TSC Queen’s vs Marsh Academy
Tanzanite Queen’s vs Yanga Princess
Baobab Queen’s vs JKT Queen’s

@tanfootball

#wapendasokaupdates

CEO MAZINGISA KUHUSU WALIOSIMAMISHWA SIMBA.

. “Hakuna mchezaji aliyeadhibiwa bali walisimamishwa kutokana na madai ya utovu wa nidhamu. . “Nilikutana na wachezaji hao na kuzungumza nao mambo yakaisha.
. “Niseme tu, hili si kwa wachezaji pekee kwamba ndiyo wanapaswa kuwa na nidhamu bali kwa wote ili kuisaidia Simba kwenda inavyotakiwa ili mambo yaende kwenye mstari.

#wapendasokaupdates

USIKU WA PEPE

.

Pepe, bahati mbaya sio Leo Messi ametia kamba hizo za freekick zingeongelewa sanaa, kutokea benchi unakuja kuchukua point 3 unatia mfukoni af unawaambia wana twendeni kati tayari kazi imeisha, the technique was on point, freekick mbili hatari sana, hadi saivi sijui ipi kali zaidi. MAN OF THE MATCH PERFOMANCE
.
Sitaki mwongelea sana UNAI, niliangalia Pre Match Conference kabla kabisa alisema ataendelea kufanya rotation, ila nadhani pia huku Europa ni sehemu za kuwapa nafasi pia seniors ambao hawapati sana nafasi first XI na sio tu madogo. Hii itasaidia kurudisha confidence.
.
Maitland-Niles ana roho ya mjeshi mpambanaji ila ana vimakosa vidogo vidogo sana vinavyogharimu timu, ‘hey warrior relax and be composed’.
.
Guendouzi yule ni mpambanaji sana, na utamuenjoy sana juu yake acheze wajina wangu Ceballos, wana muunganiko flani iv safi sana, ila dah UNAI kuhusu Ozil bado tunakuhitaji kituoni uje utoe maelezo.
.
Kule Serbia Manchester United walienda nyumbani kwa wahuni Partizan, hawa jamaa ni wahuni kweli na mashabiki wao, nikipata wasaa nitawapa stori yao na ile “The Eternal Derby”
.
MAN OF THE MATCH PERFOMANCE mbili mfululizo Europa kwa kijana Brandon Williams, mchezaji mzuri sana, Left Back anaetumia zaid mguu wa kulia, mzuri kishambulia na anasababisha penalty jana, sio mrefu sana ila nmeona anaruka pia mipira ya juu, anahitaji consistence, lile shavu la kushoto saiv yupo Young bado anaweza pata nafasi na Shaw tunajua tatizo lake ni majeruhi.
.
Ila United bado aise, wanastruggle kutengeneza nafasi kwenye open play, Juan Mata whats wrong? Ok nahisi jua limeanza kuzama labda, United bila Pogba inastruggle kucreate chances, mara ya mwisho naona nafasi nzuri open play ikitengenezwa na kuscore hasa kwa timu iliyorudi nyuma ni lile goli vs Wolves.
.
J.Garner pia perfomance nzuri, namuona kama namba 8 mzuri baadae, na ni moja ya nafasi United wanahitaji sana. Pale Arsenal yule Martineli mchezaji mzuri sana analijua goli, hizi mechi zitamsaidia sana.
.
Oya leo kuna mechi usiku pale EPL, Danny Ings yupo moto, na Vardy yupo moto, patawaka kwa Mtakatifu Maria Stadium.
.
(Tag watu wa mpira and share)
.
Written by Daniel Mtani Thomson
@danirito_thomson

Miaka.mitano ya suares ndani ya barcelona

📅 Miaka Mitano (5️⃣) imepita Tangu Luis Suárez alipocheza game yake ya kwanza kabisa akiwa kama Mchezaji wa FC Barcelona : Oktoba 25, 2014, Suarez alianza XI katika klabu ya yake mpya sambamba na Lionel Messi na Neymar Jr, Ilikiwa ni mechi ya El Clásico vs Real Madrid.

– Ilimchukua Dakika Nne tu, Suarez alitoa Assist ya goli likifungwa nae Neymar, hakumaliza Dakika 90, alitolewa Kipindi cha Pili akiiacha Barça ikipokea kipigo cha Magoli 3-1.. Goli lake la kwanza alifunga Novemba 24 katika game ya Makundi ya UEFA Champions league wakishinda 4-0 vs APOEL.. Disemba 20 alifunga goli lake la kwanza la Ligi katika mechi ya Nane katika klabu, wakishinda 5-0 vs Córdoba.

– Akaendelea kufunga tu ambapo mpaka sasa ndio mfungaji bora Namba Nne wa muda wote wa FC Barcelona, Rekodi yake na FC Barcelona..
🏟 Mechi 257
⚽ Magoli 184
🎯 Assist 97
🏆 Mataji 13 🔥 El Pistolero.
#fcbarcelona #LuisSuarez
@Harunlugoyah

Matokeo ya Soka Jana.

#VodacomPrimierLeague
FT Mbeya City 1-4 Kagera sugar :
#UefaEuropaLeague
FT Qarabag FK 2 – 2 APOEL Nicosia
FT Sevilla 3 – 0 F91 Dudelange
FT Dynamo Kyiv 1 – 1 FC Koebenhavn
FT Malmoe FF 2 – 1 Lugano
FT Getafe 0 – 1 Basel
FT Trabzonspor 0 – 2 FC Krasnodar
FT PSV Eindhoven 0 – 0 LASK
FT Sporting CP 1 – 0 Rosenborg
FT Celtic 2 – 1 Lazio
FT Rennes 0 – 1 CFR Cluj
FT Arsenal 3 – 2 Vitoria de Guimaraes
FT Eintracht Frankfurt 2 – 1 Standard Liege
FT FC Porto 1 – 1 Rangers
FT Young Boys 2 – 0 Feyenoord
FT CSKA Moscow 0 – 1 Ferencvaros
FT Ludogorets Razgrad 0 – 1 RCD Espanyol
FT Gent 2 – 2 Wolfsburg
FT Saint-Etienne 1 – 1 Oleksandriya
FT Istanbul Basaksehir 1 – 0 Wolfsberger AC
FT Roma 1 – 1 Borussia Mönchengladb
FT Besiktas 1 – 2 SC Braga
FT Slovan Bratislava 1 – 2 Wolverhampton Wande…
FT AZ Alkmaar 6 – 0 FC Astana
FT Partizan Beograd 0 – 1 Manchester United
:
#AfricaChampionsLeague
FT El Zamalek 1 – 0 Generation Foot
:
#MoroccoBotolaPro
FT Raja Casablanca 2 – 0 Raja Beni Mellal
:
#TunisiaLigue I
FT Esperance 4 – 1 Ben Guerdane
FT Etoile Metlaoui 0 – 2 Club Africain
FT US Tataouine 0 – 1 Etoile du Sahel

#sokaplaceupdates

1 – Sevilla na Manchester United ndio timu pekee kuwa na clean Sheets katika michezo yote mitatu

1 – Sevilla na Manchester United ndio timu pekee kuwa na clean Sheets katika michezo yote mitatu iliyochezwa msimu huu wa Europa League..

– Kwa kuongeza, hakuna timu nyingine ambayo imekabiliwa na shots chache on target kuliko Sevilla kwenye mashindano msimu huu… Sevilla wamekumbana na Shuti moja tu On Target 🎯.
3⃣ – 0️⃣ vs Dundelange
1️⃣ – 0️⃣ vs APOEL
0️⃣ – 3⃣ vs Qarabag
….
– Man United Mashuti 7️⃣, huku Manne wakipokea game moja 😆😆.
#EuropaLeague #Sevilla #ManUtd
@Harunlugoyah

Design a site like this with WordPress.com
Get started