
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Wilhelm Gidabuday amethibitisha kujiuzulu nafasi hiyo. masaa machache baada ya kikao cha pamoja cha RT BMT na Waziri wa michezo nchini.
Cc @officialpriscakishamba

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Wilhelm Gidabuday amethibitisha kujiuzulu nafasi hiyo. masaa machache baada ya kikao cha pamoja cha RT BMT na Waziri wa michezo nchini.
Cc @officialpriscakishamba


Orodha ya mabingwa wa FA ngazi ya Mikoa 2019/20 watakaoshiriki kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) @azamtvtz @drfa_tanzania @wilfredkidao @tplboard
:
Powered by @bikotanzania

– Uongozi wa klabu ya Alliance FC kutoka mkoani Mwanza, umeomba radhi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyofanywa na wachezaji wao wawili Israel Patrick na John Mwanda katika mchezo wao na Mbeya City uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Nyamagana… Wachezaji hao wawili wamepewa barua za kuitwa kwenye Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Alliance FC kesho saa nne asubuhi kwa hatua Zaidi.
…
– Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo Yusuph Budodi amesema wamesikitishwa na vitendo hivyo na kama uongozi hawawezi kuvivumilia hivyo watachukua uamuzi stahiki baada ya kamati ya nidhamu ya klabu hiyo kukaa na wachezaji hao kuwasikiliza.
..
– Kwenye mchezo huo, wachezaji Israel Patrick Mwenda ambaye ni nahodha wa timu ya Alliance FC alipewa kadi nyekundu baada ya kuonekana akimshika sehemu za siri mchezaji wa Mbeya City George Chota huku kipa John Mwanda naye akipata kadi nyekundu kwa kumpiga mtama mchezaji wa Mbeya City Idd Gamba.
#VPLUpdates #VPL

✍🏻 Kocha Mkuu wa klabu ya Arsenal, Unai Emery amesema kuwa nahodha wa klabu hiyo, Granit Xhaka hatakuwepo kwenye kikosi kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Wolves…Xhaka alitolewa na kuonekana mwenye hasira pia alizomewa na mashabiki wa klabu yake katika game ya Jumapili dhidi ya Crystal Palace, Pia alikataa Mkono wa kocha wake.
..
✍🏻 “Tunahitaji wakati wa kurejesha usawa ndani yake na kwa sisi, Aliomba msamaha na aliomba msamaha kwa Mashabiki na sasa ni wakati wa kuzingatia katika mechi… alisema Emery.
…
✍🏻 Emery aliulizwa kama kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27 atabaki kuwa nahodha wake lakini hakujibu moja kwa moja, akisema: “Sijuhi kwamba atacheza kesho. Nadhani kesho hatacheza.. Sasa tunahitaji kuzingatia 100% kwenye mechi. tutafanya mazoezi na kwa sasa hayuko akilini mwangu.”
#Arsenal #GranitXhaka #PremierLeague
@Harunlugoyah
Wakati timu ya soka ya Yanga ikitaraji kushuka dimbani siku ya jumapili kumenyana na Pyramids ya nchini Misri,mdau wa soka kutoka Sumbawanga amesema kwamba yeye ana uwezo wa kuipeleka Yanga kwenye hatua ya makundi
:
Mdau huyo anaejulikana kwa jina la Mzee Kataushanga amezungumza na @saidallymwandike wa @daboten kwa njia ya simu ambapo amesema kwamba yeye ana uwezo wa kuisaidia @yangasc kupata ushindi kwenye mchezo huo wa kombe la shirikisho barani Afrika kwa kutumia uwezo wake alio nao.
:
Amesema kwamba yeye yuko radhi kufanya swala hilo endapo kama uongozi wa Yanga utampatia kiasi cha fedha ambazo anazihitaji kwa lengo la kufanikisha jambo hilo. “Mimi nawaambia viongozi kama watakuwa tayari basi hizo pesa wasinipe mimi hadi hapo mechi itakapoisha na timu kupata matokeo yatakayowapeleka hatua ya makundi”alisema mzee Kataushanga.
:
Aidha amesema kwamba hilo jambo si mara ya kwanza kwake kulifanya,kwani kuna kipindi cha nyuma aliwahi kuisaidia timu hiyo kutinga hatua ya makundi katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika. “Kuna kipindi nilimtumia ujumbe Mkwasa akiwa katibu wa Yanga kumweleza jambo hilo ambapo nilifanikisha kulifanya bila malipo yoyote”
:
Hata hivyo ameongeza kwa kusema kwamba kwa sasa hawezi kukamilisha swala hilo kama hakuna uthibitisho wa upatikanaji wa fedha anazohitaji ambazo hakuweka bayana kiasi anachohitaji hadi hapo atakapoongea na muhusika.
:
Yanga inataraji kushuka dimbani siku ya jumapili kumenyana na Pyramids ya nchini Misri katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 2-1 nyumbani
: Cc @daboten

KAMATA MATOKEO YA SOKA JANA :
#EnglandChampionship
FT Barnsley 2 – 2 Bristol City
:
#GermanyBundesliga
FT Hoffenheim 3 – 0 SC Paderborn 07
:
#FranceLigue1
FT Dijon 2 – 1 Paris Saint-Germain
:
#NetherlandsEredivisie
FT PEC Zwolle 2 – 4 Ajax Amsterdam
:
#World Cup U-17
FT Angola 0 – 2 Brazil
FT Canada 0 – 1 New Zealand
FT Australia 2 – 1 Nigeria
FT Hungary 2 – 3 Ecuador
:
#KenyaPremierLeague
FT Mathare United 0 – 0 Posta Rangers
:
#MoroccoBotolaPro
FT Renaissance Club Zemamra 2 – 0 Rapide Club Oued Zem
:
Prepared by @officialchristz
Powered by @bikotanzania

Hali ya Singida United si shwari sana kwenye ligi msimu msimu huu, wamepoteza mechi mbili zilizopita tangu waanze kuutumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kama uwanja wao wa nyumbani baada ya uwanja wa Namfua-Singida kufungiwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kuchezewa mechi za ligi kuu.
Singida United wana pointi tatu tu baada ya kucheza michezo tisa na wanashika mkia kwenye msimamo wa ligi na huenda mwisho wa msimu tusiwenao tena kwa ajili ya msimu ujao.
Edgar Kibwana alikuwepo Arusha wakati Singida United ilipocheza na Simba, kwa mujibu wa kocha wa Singida United Ramadhani Nsanzurwimo anasema amekuja ameikuta timu imeshafanya Pre-season na imeshaanza ligi kwa hiyo jukumu lake ni kutengeneza falsafa yake na kutengeneza timu kwa ajili ya kupata matokeo.
Nsanzurwimo anakiri changamoto za nje ya uwanja huenda zikamkwamisha kufikia malengo yake.

Alex Luambano anasema Namungo ni kama inafuata nyayo za Kariakoo Lindi, ikitoka nje ya Lindi inachezea vipigo lakini ikiwa Ruangwa hatoki mtu.
•
“Kuna msimu mmoja Kariakoo Lindi ilishinda mechi zote za nyumbani isipokuwa mchezo mmoja ilitoka sare dhidi ya Yanga, halafu ikafungwa mechi zote za ugenini isipokuwa mechi moja tu dhidi ya Yanga, ilipata sare.”
•
Namungo inatengeneza rekodi ya aina yake kwenye ligi, hadi sasa imecheza mechi 8, haijapoteza mchezo wowote nyumbani ambapo imeshinda mechi 4 na sare 1.
Namungo ikiwa uwanja wa nyumbani
Namungo 2-1 Ndanda
Namungo 2-0 Singida United
Namungo 0-0 Mwadui
Namungo 1-0 Lipuli
Namungo 1-0 Mtibwa Sugar
Imecheza mechi 3 ugenini na imepoteza zote, haijaambulia pointi yoyote ikiwa ugenini.
Namungo ikiwa viwanja vya ugenini
KMC 1-0 Namungo
Azam 2-1 Namungo
Kagera Sugar 2-0 Namungo

Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limemteua Bw. Baraka KIZUGUTO wa Tanzania kuwaAssistant General Coordinator (AGC) katika Fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 (TOTAL U23 Africa Cup of Nations 2019)
Fainali za U23 zitafanyika jijini Cairo nchini Misri kuanzia Novemba 08 -22, 2019 zikishirikisha timu nane ambapo timu tatu za juu zitafuzu kucheza Fainali za Olympik 2020 nchini Japan.
Kila la kheri AGC @kizuguto

Mara nyingi timu zenye majina madogo zikikutana na timu zetu kubwa huwa wanaingia miguu yote na kushindwa kuziheshimu timu kubwa. Wana misemo yao kwani Simba, Yanga au Azam kitu gani? Wanamiguu miwili kama sisi hakuna wanachotuzidi tunaweza kuwapiga. Kiuhalisia Simba, Yanga, Azam ni timu kubwa.
Kwa hiyo ukiingia mazima unakula tatu, nne, mpira umeisha lakini ukiwakabili kwa nidhamu kama ambavyo wamefanya Mwadui jana unaweza kupata matokeo.
Mwadui waliwaheshimu sana Simba, moja ya mbinu ambayo kocha wa Mwadui Khalid Adam alifanikiwa ni kutowaruhusu Simba kufanya mipango katikati.
Emmanuel Memba, Mussa Nampaka ‘Chibwabwa’ walikichafua sana kati hawakutaka kucheza mpira lakini hawakuwaruhusu pia Simba kucheza mpira pamoja na uwanja kutokuwa rafiki kwa Simba kucheza kwa style yao.
Fraga ni mchezaji ambaye namhusudu lakini jana alipata wakati mgumu inawezekana kwa sababu ya uwanja. Amekuwa ni mtu ambaye anaifanya timu icheze, anaanzisha mipira kwenye maeneo tofauti lakini jana hakupata hiyo nafasi. Muda mwingi alikuwa anagongana na kina Chibwabwa.
Mwadui walijitahidi mbele kucheza mipira yote ya juu iliyokuwa inavushwa pamoja na second balls zote walikuwa wanaiosha kuihamishia kwenye zone ya Simba.
Simba ili wawe bora ni lazima wacheze lakini hawakupewa hiyo nafasi ukiongeza na mazingira ya uwanja yakawazui kucheza kwa hiyo wakawa wanashindana kuwahiana mipira inayowekwa kwenye nafasi.
Kama uliangalia hiyo mechi utagundua Mwadui walitengeneza nafasi nyingi kuliko Simba. Simba hawakupata nafasi, Mwadui waliisoma Simba wakafanya mipango yao na wakapata matokeo.