
Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuachana na kocha wao mkuu Mwinyi Zahera pamoja na benchi zima la ufundi baada ya kushindwa kufanya vizuri.
Uamuzi huo umetangazwa mbele ya Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo na Mwenyekiti, Dk. Mshindo Msola ambapo kwa sasa timu hiyo itakuwa chini ya kocha wa muda Charles Mkwasa.
Taarifa za awali zilikuwa zinasema kocha wa Bandari FC ya Kenya, Ben Mwalala ndiye atakaye chukua nafasi ya Mkongomani huyo lakini Dk. Msola amemtangaza Mkwasa mchana huu.
Kibarua cha kwanza cha Mkwasa kitakuwa siku ya Ijumaa kitaposhuka dimbani kuikabili Ndanda katika uwanja wa Nangwanda.
#wapendasokaupdates



■Hatua ya makundi imemalizika kwa Afrika kuingiza timu 3 katika hatua ya mtoano:


:











