: WATU 11 WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE 25 KUJERUHIWA KWENYE MILIPUKO

Milipuko miwili ya kujitoa muhanga iliyohusisha gari mbili imetokea kwenye Mji Mkuu wa Somalia na kusababisha vifo vya watu 11 na kujeruhi wengine 25 ambapo kikundi cha Al-Shabab wamekiri kuhusika nayo

Mlipuko wa kwanza ulitokea karibu na sehemu ya ukaguzi kwenye Kasri ya Rais na kusababisa vifo 9

Mlipuko wa pili ulitokea kwenye njia inayoelekea uwanja wa ndege wa mji huo ambapo alifariki dereva wa gari hiyo na mshirika wake

Al-Shabab wamesema lengo la milipuko hiyo kwenye maeneo hayo illikuwa kulipua eneo la ukaguzi la uwanja wa ndege kwa kuwa wanadiplomasia wengi hutumia uwanja huo na pia kasri la Rais kwa kuwa ni eneo ambalo huwa wanalilenga mara nyingi

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started