ISSUE YA YANGA NA NIYONZIMA IKO HIVI

Uongozi wa Klabu ya Yanga kupitia kwa afisa habari wao Hassan Bumbuli umesema umekua ukipokea maoni mengi kutoka kwa wanachama na mashabiki wao wakitaka kiungo wao wa zamani Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye sasa anaichezea klabu ya AS Kigali arejeshwe katika kikosi chao.

Bumbuli amesema wameyafanyia kazi mapendekezo hayo na tayari upo mpango wa kumfuatilia Niyonzima huko aliko ili kuona kama bado yupo katika kiwango cha kuridhisha na iwapo wataridhika naye basi wataangalia taratibu za kumsajili.

#wapendasokaupdates

AC Milan mbioni kumnasa Ibrahimovic

– AC Milan leo Ilikuwa na mkutano na Mino Raiola kwa ajili ya Mazunguko kuhusu mteja wake, Zlatan Ibrahimovic ili kujiunga na Klabu hiyo.
:
– Waliuliza uwezekano kama upo wa kumsajili Zlatan ambaye anasubiriwa yeye mwenyewe kuamua hatma yake kuhusu jambo hilo wiki ijayo, kwasasa ni Mchezaji huru baada ya kuondoka LA Galaxy ya huko USA ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ.. Hakuna kitu Walichokubaliana, inaelezwa kuwa mazungumzo tu yameanza kati ya Milan na Ibrahimovic..
#TransfersNews #ZlatanIbrahimovic

Samatta awajibu watanzania

Baada ya kupitia Comment za wadau mtandaoni kuhusu kiwango chake katika timu ya taifa Nahodha wa taifa stars Mbwana Ally Samatta amewajibu wadau wa soka kwa kusema haya
:
โ€œNimepata meseji na comment kutoka kwa watu kadhaa kuwa awajaelewa kiwango nilichoonesha ktk mechi za timu ya taifa, anyway ukweli nimefurahi kuona watu wanasema ukweli sichukulii binafsi bali nachukulia km chachu itakayonifanya nijitume zaidi ili niweze Bora zaidi, HAINA KUFELIโ€
:
#SokaplaceUPDATES
#TaifaStars #twenzetutena

Matokeo Ya Soka Jana

:

#England FA Cup
FT Darlington 0 – 1 Walsall
FT Lincoln City 0 – 1 Ipswich Town
FT Newport County 2 – 0 Grimsby Town
FT Wycombe Wanderers 1 – 2 Tranmere Rovers
:
#Kenya – Premier League
FT Kisumu All Stars 2 – 0 Wazito FC
FT Mathare United 0 – 1 Sofapaka
FT Nzoia Sugar FC 0 – 2 Posta Rangers
:
Ratiba ya Soka Leo
:
#Belgium – First Division A
22:30 Royal Antwerp vs Gent
:
#Kenya – Premier League
15:00 Bandari vs AFC Leopards
15:00 Kariobangi Sharks vs Ulinzi Stars
15:00 Tusker FC vs Western Stima
16:00 Gor Mahia vs Kakamega Homeboyz
:
Prepared by @officialchristz
Powered by @bikotanzania

Matokeo mechi kufuzu AFCON 2021

Nigeria ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฌ 2-1 ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ฏ Benin
Cameroon ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฒ 0-0 ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ป Cape Verde

Guinea Bissau ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ผ 3-0 ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ฟ eSwatini
Burkina Faso ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ซ 0-0 ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ฌ Uganda

Sudan ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ฉ 4-0 ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡น Sao Tomรฉ

Angola ๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ด 1-3 ๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ฒ The Gambia
Senegal ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ 2-0 ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ฌ Congo
Malawi ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ผ 1-0 ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ธ South Sudan
Central Africa ๐Ÿ‡จ๐Ÿ‡ซ 2-0 ๐Ÿ‡ง๐Ÿ‡ฎ Burundi
Sierra Leone ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ฑ 1-1 ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ธ Lesotho
Namibia ๐Ÿ‡ณ๐Ÿ‡ฆ 2-1 ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฉ Chad
#wapendasokaupdates
#AFCON2021Q

SHIME: TUNATAKA KUCHUKUA TAJI KWA MARA YA TATU MFULULIZO

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ Bakari Shime amesema wamejiandaa kutwaa taji la Cecafa Chalenji ya Wanawake kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Michuano ya Cecafa kwa Wanawake ktaanza kutimua vumbi keshokutwa Jumamosi katika uwanja wa Azam Complex huku Tanzania wakiwa ndio wenyeji ikishirikisha timu nane kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.

Shime amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 95 na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri morali ipo juu na lengo letu ni kuchukua taji kwa mara ya tatu mfululizo. “Wachezaji wapo kwenye hali nzuri, maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na lengo letu ni kuchukua taji hili kwa mara ya tatu mfululizo tena safari hii tukiwa katika ardhi ya nyumbani,” alisema Shime.

#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started