Kikosi kilichitajwa cha taifa stars

Hiki ni kikosi cha awali .. Najua kuna mchujo utapita, but benchi la Ufundi limethibitisha kua lnafatilia kwa makini Ligi yetu, msimu huu

1: Mwaita Gereza
2: Yusuf Mhilu
3: Fredy Tangalu
4: Zawadi Mauya
5: Cleopass Mkandala
6: Baraka Majogoro
7: Lucas Kikoti
8: Paul Nonga

For me, hawa wamepewa zawadi waliyostahili kwa jasho walilovuja kwenye klabu zao… Ni jukumu lao sasa kuthibitisha ubora wao ili kuingia kwenye kikosi cha mwisho kitakachokwenda Uganda.. Hongera makocha kwa uteuzi huu👏👏

MOURINHO AANZA KWA USHINDI SPURS

Kocha mpya Wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho amaeanza kazi kwa ushindi Wa bao 3-2 ugenini dhidi ya West Ham United
Son Hueng-Min, Lucas Moura na Harry Kane wote walifunga kwa upande Wa Spurs wakati Michael Antonio na Angelo Agbonna

#wapendasokaupdates
#PLMOURINHO AANZA KWA USHINDI SPURS

Kocha mpya Wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho amaeanza kazi kwa ushindi Wa bao 3-2 ugenini dhidi ya West Ham United
Son Hueng-Min, Lucas Moura na Harry Kane wote walifunga kwa upande Wa Spurs wakati Michael Antonio na Angelo Agbonna

#wapendasokaupdates
#PL

MAN CITY YAINYOOSHA CHELSEA

Mabingwa watetezi Wa Ligi kuu nchi ni England wameibuka na ushindi Wa bao 2-1 dhidi ya Chelsea katika mechi ya ligi kuu ya England katika uwanja Wa Etihadi.

Kevin De Bryune na Rihad Mahrez walifunga mabao ya City baada ya Chelsea kutangulia kufunga kwa goli la N’golo Kante
City imefikisha pointi 28 katika nafasi ya 3 huku Chelsea wakibaki na pointi zao 26 katika nafasi ya nne.

#wapendasokaupdates
#PL

Papasa squared ipo pale pale” Masau Bwire.

.
🗣️”Papasa squared ipo pale pale, ila leo mzigo ulikuwa mzito na uliielemea meli yenye kawaida ya kuelea. Kiwango cha Simba cha kawaida hata ukiangalia magoli yaliyofungwa leo mimi mwenyewe nilikuwa nashangaa haya magoli yanaingiaje”.
.
Maneno ya Masau Bwire msemaji mkuu wa Ruvu Shooting baada ya mechi dhidi ya timu ya Simba, na timi yake kuburuzwa 3-0
.
#bakinasisi__
#NjooKwetu
#TupoNawePaleUlipo

Mambo 10 nilioyaona Ruvu Vs Simba

1: Miraj Athuman at his best 🙌 Bao 2 safi. Mabao 6 kwenye orodha ya wafungaji bora (akiwa na dakika chache kuliko wote).. So far, ndie mchezaji hatari zaidi kwenye kikosi cha Simba

2:Kahata 🙌 Mr Slow but sure! Hii inaweza kua performance yake bora tangu aje Simba🙌 Ile assist ya pili inahitaji akili kubwa mno kuitengeneza🤝🏼
.
.
3: Shaban Msala na Zuberi Dabi (Viungo wa Ruvu) walijiandaa kuwachezea rafu viungo wa Simba na kusahau jukumu lao la kutengeneza nafasi kwa kina Sadat Mohammed.

4: Salum Mayanga🤔 Kipindi cha kwanza, plan ilikuwa kunufaika na kasi ya Sadat na Emmanuel Martin (Ajabu mipira mipira mingi ikawa inatupwa katikati na sio pembeni).. Kipindi cha pili akiwa na Abdallahman Mussa na Fullyzulu Maganga (Mipira ikaondoka katikati ikarudishwa pembeni) … Approach ya Ruvu iliwapa uwepesi mabeki wa Simba🙌

5: Muzamir Yassin atachoka lini 😃 Anakimbia kilomita nyingi, anakaba na jambo zuri leo, alikua na jicho zuri la kupiga pasi baada ya kupokonya mpira🙌 I just Love him🙌

6: Kapombe please 🙏Kama iko nafasi ya kubadili maamuzi yako kwa ajili ya Taifa, rudi Taifa Stars..Taifa linakosa mtu wa aina yako🙌

7: Emmanuel Martin hakustahili kumaliza. Upepo ulikata, nguvu zikapotea. Nafasi zile, kwa uwezo wake wa kupiga, zilitakiwa kutengeneza kitu kwa Ruvu

8: Napenda sana utulivu wa Wawa (Akiwa/asipokua na mpira).. Habutui, mara zote pasi yake hua inaanzisha shambulizi kutokea chini
.
.
9:Yule kipa wa Ruvu, pamoja na yote, bado anastahili kuwa Man of the match kwa timu yake.. Bila mikono yake, msiba ungekua mkubwa zaidi Jeshini.

10: Yule beki Mbrazil ni kama ameanza kuzoea mazingira ya Bongo. Ni muhuni flan hivi anayependa kushindana muda wote🙌 Nimependa sana spirit yake kwa ajili ya Simba.

Nb: January sio mbali jaman😃

“Watanzania waendelee kuiunga mkono timu Yao” Ndayiragije .

Ndayiragije 🗣️”Tutapata muda mwingi wa kukaa pamoja na wachezaji ili kufanya maboresho kwa mapungufu yaliojitokeza ili kujiweka sawa kwa michuano ambayo ipo mbele yetu. Watanzania waendelee kuiunga mkono timu yao, matokeo ni kati ya changamoto zilizopo kwenye soka yasifanye wakate tamaa bali nikuendelea kupambana kufikia ndoto zetu,”
.
#bakinasisi__
#NjooKwetu
#TupoNawePaleUlipo

Arsenal kuleta mshambuliaji mtata

Arsenal imeonyesha juhudi za kumtaka mshambuliaji wa Red Bull Salzburg, Erling Haaland, baada ya kumwalika baba yake, Alf-Inge Haaland, kutembelea uwanja wao wa mazoezi wa London Colney.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ametajwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaohitajika sana katika dirisha la usajili Januari 2020.

Ikubukwe Red Bull Salzburg iliweka bei ya pauni milioni 86 kama dau la usajili kwa mshambuliaji Erling Braut Haaland.

Arsenal wana mkwaja wa kumsajili Haaland? 🤔

Design a site like this with WordPress.com
Get started