Mambo machache niliyoyaona kwenye mchezo wa ligi kuu England kati ya Leicester City dhidi ya Everton. .

.
1 kabla ya mechi kuanzia nilisikilizia Interview ya kocha wa Everton Marcos Silva, amesema kuwa yeye ahofii kufukuzwa alikuwa akiongea kwa hisia sana πŸ€” anasema aelewi tatizo la timu yake ipo wapi mpaka sasa.
.
.
2 alifahamu ubora wa Leicester City msimu huu alikuja na mfumo wa 3-4-3 kutumia wachezaji wa pembeni kwenye kushambulia wakiwa hawana mpira wanarudi kwenye mfumo wa 4-5-1 kipindi cha kwanza walifanikiwa kwa hilo.
.
.
3 beki wa pembeni wa Everton Digne alifanikiwa kumzuia Ayo Perez, alijua ubora wake ampi nafasi ya kufanya maamuzi ni mchezaji hatari akiwa na mpira ukiachana na Maddison na Vardy. .
.
4 iweobi sijui leo kazaliwa tena alikuwa πŸ™Œ akipata mpira anaingia ndani anakuwa kama kiungo alifanikiwa kuwasaidia viungo wa Everton.Alikuwa kuna Davies na Sigurdsson. .
.
5 Richarlson yule Mbrazil aliwahi kusema anatamani kucheza timu ya Taifa ya Brazil, na alifanikiwa ni mchezaji mwenye kasi aliwapa tabu sana mabeki wa Leicester City πŸ‘.
.
.
6 kipindi cha pili Marcos Silva, nahisi aliwambia Wachezaji wake sasa wafunguke waanze kushambulia aliamini Leicester City amewashika ndipo matatizo yalianza hapo πŸ€”.
.
.
7 Leicester City, mfumo wa 4-1-4-1 ni mfumo mzuri kwao Ndindi ni kama Mmakonde πŸ™Œ anakaba anazisha mashambulizi kila mda nilikuwa naenjoy kumuangalia kwenye eneo la kiungo ndo roho ya timu kwa sasa.
.
.
8 kutoka kwa Ayo Perez, mechi ilimshinda kuingia kwa Inheacho kulimfanya Vardy arudi pembeni πŸ™Œ na kumpa Inheacho uhuru kama mshambuliaji wa kati. .
.
9 bao la Vardy halina utofauti aliyowahi kuwafunga Arsenal msimu huu pale King Power upande ule ule wa kushoto eneo lile lile πŸ€” huu uwanja wa King power anaufahamu vizuri. .
.
10 bao la Inheacho ingekuwa Simba na Yanga mechi ingeendelea? Maana πŸ€” Inheacho alitumia akili sana. .
.
11 Marcos Silva next game anaenda Anfield πŸ™ŒπŸ˜Š siku ya Jumatano kibarau chake kipo shakani. .
.
Prepared by Azizi_mtambo_15
@danirito_thomson @officialchristz Powered by @bikotanzania

Ratiba Ya Soka Leo

:
#TanzaniaFDL
16:00 Rhino Rangers vs Gwambina
16:00 CosmoPolitan vs Boma Fc
:
#TanzaniaPremier League
16:00 Young Africans vs KMC FC
16:00 Biashara Mara vs Ndanda Sc
:
#EnglandFA Cup
22:45 Solihull Moors vsRotherham United
:
#GermanyBundesliga
22:30 Mainz 05 vs Eintracht Frankfurt

#ItalySerie A
22:45 Cagliari vs Sampdoria
:
#EnglandChampionship
22:45 Preston North End vs West Bromwich Albion
:
#EgyptPremier League
18:00 Smouha SC vs El Geish
:
#MoroccoBotola Pro
17:00 Youssoufia Berrechid vs Olympic Club de Safi
21:00 MAT Tetouan vs Rapide Club Oued Zem
:
Prepared by @officialchristz
@sokaplace_

Domayo asafiri kwenda south Africa kwamatibabu

NAHODHA Msaidizi wa Azam FC, Frank Domayo ‘Chumvi’, ameondoka nchini alfajiri ya leo Jumatatu kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya tatizo la kuchanika msuli wa nyama ya paja ya mguu wa kulia.

Domayo alipata maheraha hayo, wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa, iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 nchini Cameroon dhidi ya Guinea ya Ikweta.

Nyota huyo wa Azam FC ameambatana na Daktari wa timu, Dr. Mwanandi Mwankemwa, ambapo matibabu yake yatachukua takribani siku 10 atakazokuwa huko, yakifanyika kwenye Hospitali ya Vincent Palotti chini ya Dr. Robert Nickolas.

#wapendasokaupdates

Baadhi ya Nyota ambao waliwahi kufunga mabao manne katika mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya .

βœ… Lewandowski mwenye miaka 31, aliyafunga mabao yake katika mchezo huo katika dakika ya 53, 60, 64 na 68 huku mabao mengine ya Bayern Munich, yakifungwa na Leon Goretzka na Corentin Tolisso. Hiyo siyo mara ya kwanza kwa Lewandowski kufunga mabao manne katika mchezo mmoja, mara yake ya kwanza ilikuwa kipindi alipokuwa akiichezea Borussia Dortmund, Aprili 24, 2013, alipoitungua Real Madrid mara nne katika ushindi wa 4-1.
.
βœ… Serge Gnabry
Nyota huyo wa zamani wa Arsenal, alifunga mabao manne katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Oktoba 22 dhidi ya Tottenham Hotspur ambao Bayern Munich waliibuka na ushindi wa mabao 7-2.Alitumia dakika ya 53, 55, 83 na 88 kufunga mabao hayo.
.
βœ… Cristiano Ronaldo
Desemba 8, 2015, Ronaldo alifunga mabao manne kipindi hicho akiichezea Real Madrid katika mchezo ambao miamba hiyo ya soka la Hispania, waliitwanga MalmΓΆ FF ya Sweden mabao 8-0.
Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Ureno, alifunga mabao hayo dakika ya 39, 47, 50 na 58, Karim Benzema katika mchezo huo, alifunga mabao matatu β€˜hat trick’.
.
βœ… Zlatan Ibrahimovic
Mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita alifanya vizuri akiwa na LA Galaxy ya Marekani, alufunga mabao manne, Oktoba 23, 2013 wakati akiongoza Paris Saint-Germain ya Ufaransa kuizamisha Anderlecht ya Ubelgiji mabao 5–0. Alitumia dakika ya 17,22, 36 na 62 kufunga mabao hayo huku Edison Cavan akifunga moja.
.
βœ… Lionel Messi
Lionel Messi
Messi ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya wanasoka bora duniani kwa sasa, alifunga mabao manne, Aprili 6, 2010 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambao FC Barcelona waliifunga Arsenal mabao 4-1.
.
#bakinasisi__
#NjooKwetu
#TupoNawePaleUlipo

Nyasi za taifa kuungua leo Yanga Vs KMC .

Yanga Vs KMC .
🏟️ Uhuru Stadium
⏱️ 10:00 Jioni
πŸ† Vodacom Premier league
.
.
Kinondoni boys :
Mechi tatu za mwisho kmc wamefungwa zote na wakifunga magoli 2 tu.
.
Vs Mbao 0-2
Vs Alliance 1-2
Vs Kagera Sugar 1-2
.
.
Yanga Sc:
Mechi tatu za mwisho yanga imeshinda zote na imefunga magoli 5.
.
Vs Ndanda 1-0
Vs JKT Tanzania 3-2
Vs Alliance 2-1
.
Kmc msimu huu sio salama kwao kwani hadi hivi sasa Katika mechi walizocheza wamefunga magoli 6 tu. .
Dondosha utabiri wako ___?
#bakinasisi__
#NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Flamengo yaendeleza ubabe ligi.kuu brazil

.
.
Jana ligi kuu soka Brazil (Brazil Serie A) iliendelea na moja ya mechi iliwakutanisha vinara wa ligi hiyo Flamengo dhidi ya anayeshika nafasi ya tatu Palmeiras. .
Matokeo ya mechi hiyo Flamengo waliibuka na Ushindi wa goli 3-1 huku Gabriel Barbosa mshambuliaji hatari kwa Huko Brazil akiweka kambani goli 2 pekee na kumfanya kufikisha magoli 24 kimiyani na ndiye kinara wa magoli Nchini humo.
.
Msimamo wa ligi hiyo kwa timu tano za juu πŸ‘‡
1: Flamengo > 87 pts
2: Santos > 71 pts
3: Palmeiras > 68 pts
4: Gremio > 62 pts
5: CA Paranaense > 60 pts
.
#bakinasisi__
#NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Design a site like this with WordPress.com
Get started