ASILIMIA 92 YA WALIOMALIZA DARASA LA SABA WACHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2020

Wanafunzi 701, 038 sawa na asilimia 92.2 waliomaliza darasa la saba wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2020.
Hata hivyo, wanafunzi 58,699 sawa na asilimia 7.73 waliofaulu hawakuchaguliwa kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametangaza.

#AzamTVUpdates

KIKOSI CHA MWISHO CHA KILIMANJARO STARS

Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Tanzania Bara β€˜Kilimanjaro Stars’ limetaja orodha ya mwisho ya wachezaji 22 wanaoondoka kuelekea nchini Uganda kwaajili ya michuano ya CECAFA Challenge inayotarajiwa kuanza Desemba 7, 2019.

Kwenye orodha hiyo, majina 11 yamekatwa kutoka kwenye kikosi cha awali ili kukidhi idadi inayohitajika ambapo miongoni mwa waliokatwa ni golikipa Juma Kaseja, ambaye taarifa zinaeleza anasumbuliwa na majeraha.

Pia mshambuliaji wa Ik Frej Taby ya nchini Sweden Rashid Chambo ameongezwa kwenye kikosi licha ya kuwa hakutajwa katika kikosi cha awali.

Wachezaji wanaokwenda Uganda ni.

1. Metacha Mnata – Yanga SC
2. Aishi Manula – Simba SC.
3. David Kisu – Gor Mahia.
4. Juma Abdul – Yanga SC
5. Nickson Kibabage – Difaa El Jadid, Morocco.
6. Gadiel Michael – Simba SC.
7. Mwaita Gereza – Kagera Sugar.
8. Mohamed Hussein – Simba SC.
9. Bakari Mwamnyeto – Coastal Union.
10. Kelvin Yondan – Yanga SC
11. Baraka Majogoro – Polisi Tanzania.
12. Jonas Mkude – Simba SC.
13. Zawadi Mauya – Kagera Sugar.
14. Mzamiru Yassin – Simba SC
15. Hassan Dilunga – Simba SC.
16. Ditram Nchimbi – Polisi Tanzania
17. Cleoface Mkandala – Tanzania Prisons.
18. Paul Nonga – Lipuli FC
19. Miraji Athuman – Simba SC.
20. Eliuter Mpepo – Buldcon, Zambia.
21. Lucas Kikoti – Namungo FC.
22. Rashid Chambo – Ik Frej Taby, Sweden.

WALIOKATWA:
Wachezaji 11 waliokuwa wametajwa katika kikosi cha awali na sasa hawamo ni pamoja na

1. Juma Kaseja – KMC
2. Salum Kimenya – Tanzania Prisons.
3. Abdulmajid Mangalo – Biashara United.
4. Fred Tangalu – Lipuli FC
5. Idd Seleman – Azam FC.
6. Kelvin John – Football House.
7. Jaffary Kibaya – Mtibwa Sugar.
8. Salum Abubakar – Azam FC.
9. Eliud Ambokile – TP Mazembe, DR Congo.
10. Yusuph Mhilu – Kagera Sugar.
11. Shaban Chilunda – Azam FC

MGUNDA: TUNAENDA KUSHINDANA NA YOYOTE CECAFA SIO ZANZIBAR PEKEE

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Heroes’ Juma Mgunda amesema ameandaa kikosi chake kwa ajili ya kushindana kwenye michuano ya Cecafa Senior Challenge na haangalii mechi moja dhidi ya Zanzibar Heroes.

Kilimanjaro imepangwa kundi C ikiwa pamoja na Zanzibar ambao wamekuwa wakipata ushindi mara nyingi dhidi yao pamoja na timu za Kenya na Djibouti.

Mgunda amesema lengo lao la kwanza katika mashindano hayo ambayo yatafanyika nchini Uganda kuanzia Jumamosi hii ni kutwaa ubingwa ambao mara ya mwisho kuchukua taji hilo ilikuwa mwaka 2010. “Sisi tunaenda Cecafa kushindana na yoyote, Zanzibar tunaenda kukutana nao kama wapinzani na lengo letu ni kuhahakikisha tunatwaa ubingwa na tuna kikosi kizuri cha kufanya hivyo,” alisema Mgunda.

#wapendasokaupdates

List ya wachezaji wa kike wanaowania tuzo ya Mchezani Bora wa kike wa mwaka barani Afrika

πŸ‘‰List ya wachezaji wa kike wanaowania tuzo ya Mchezani Bora wa kike wa mwaka barani Afrika (Africa Women’s Player of the year)

Majina yaliyosalia Matano.
:
1 Ajara Nchout Njoya πŸ‡¨πŸ‡²
2 Asisat Oshoala πŸ‡³πŸ‡¬
3 Gabrielle Onguene πŸ‡¨πŸ‡²
4 Tabitha Chawinga πŸ‡²πŸ‡Ό 5 Thembi Kgatlana πŸ‡ΏπŸ‡¦
:
#CAFAwards2019
#SokaplaceUPDATES
@officialchristz @sokaplace_ @danirito_thomson

Design a site like this with WordPress.com
Get started