
Na Junior wa Pastor
Nchi yetu ni yenye wajuaji wa mazoea kila mtu ni daktari ule mtindo wa kumshika mtu pembeni ya shavu na kuthibitisha ugonjwa wake sina uhakika kama ni njia sahihi ya kujua afya ya mtu ndio.
Tanzania pekee ndio watu hupima kiuno cha suruali kwa kutumuia shingo na si kuangalia namba ya kiuno ,kuna watu wanazeeka na hawajui namba ya viatu vyao maana wanapima kwa kuvaa na si kujua namba ya kiatu kinachomuenea.
Soka la Tanzania ni kama filamu ya Isidingo kila siku inazua jambo jipya , wekundu wa msimbazi waliona kujifunza kwa walioendelea ni jambo jema wakafanya hivyo na ndiyo klabu inayoendeshwa kisasa zaidi hapa nchini.
Kama huna redio au televisheni basi utaona ukipita bunju hata kwa bahati mbaya mbele ya magazeti utajionea tofauti ya mkutano wa simba na timu zingine hata mipango yao ni tofauti kabisa na vilabu vingingine hapa nyumbani , kongole kwa wana msimbazi wote.
Wamejua mgonjwa soka la bongo anapaswa kutibiwa na wameanza kumtibu lakini katika matibabu yao kuna maswali kidogo ndani yake tena yasipopata majibu ni hatari zaidi maana bado tunatibu pasipo kujua ugonjwa wetu ni upi lakini tuna dozi tayari .
Tumempokea Sven Vanderbroeck kama kawaida yetu kwa shangwe , akianzia taifa kutengeneza tangazo linalotazamika baadae tukamuona bunju ni sahihi kujua maeneo muhimu maana ndio kaingia nchi ya mswahili ambayo mkataba wa miaka miwili ni kama chai na chapati mbili ndio Maisha yetu.
Ulimsikia Haji Manara baada ya kuondoka Patrick Ausems ? Manara alisema hadharani kuwa Ausems aliwahi kupingana na uongozi juu ya upangaji wa kikosi kuhusu Dilunga na hata Miraji , hivi ni kweli Ausems alipaswa kupangiwa timu na akubali?
Simba mpya imetuleta Kocha msaidizi kabla ya kocha mkuu , Dhahiri vita ya Ausems na Masoud Djuma haikuwa fundisho japo ilizaa Simba ukawa (watetezi wa Masoud) kipindi kile.
Inaendelea
Prepared by @junior_wa_pastor
#SokaplaceUPDATES
@officialchristz @danirito_thomson

.
:
👉EnglandPremier League










