




1: Abdallah Mohammed Baresi👏 Ushindi wa JKT ulianza kwenye kitabu chake cha ufundi. Ile 4-2-2-2 iliimeza kabisa 4-2-1-3 ya Sven. Kipindi cha kwanza walipoikamata Simba, katikati, wakamaliza hesabu zao
2: Sina hakika kama Sven alifanya research ya kutosha kuwajua JKT. Kwa namna yoyote ile, kwa ugumu wa viungo wa JKT, Ibrahim Ajib hakuwa chaguo sahihi kucheza kwenye ‘role’ ile
.
.
3: Shabani Mgundila🙌 What a player👏 Box to Box midfielder aliyefanya majukumu yote uwanjani. Alikaba kibabe, akaanzisha kibabe. Kipindi cha pili alifanya kazi kubwa sana kuziba nafasi za mikimbio ya kina Chama
4: Mechi ilihimuhitaji Kahata tangu dakika ya kwanza. Skills zake, jicho lake la pasi lingeweza kua na madhara makubwa kwa JKT kuliko ilivyokua Ajib
5: Mechi ya pili mfululizo timu pinzani zinatumia dakika 15 za kwanza kuipress Simba. (Dhidi ya Polisi, Simba walifanya attempt ya kwanza golini dakika ya 18. Dhidi ya JKT wamefanya attempt ya kwanza ya maana dakika ya 16) hii si ishara nzuri kiufundi kwa Simba, hasa inapokua nyumbani
6: Uliwaona wale watu wa 4 wa JKT pale katikati. Nurdin Mohammed alikuwa mtulivu, Mgandila akawa mtukutu. Kazimoto akatengeneza space, Hafidh Mussa akapika mashambulizi. JKT wakiwa na mpira, Fraga akajikuta anashambuliwa na watu watatu kwenye zone yake
7: Adam Adam🙌 Bao la 6 msimu huu. Bado nasisitiza, akiongeza utulivu, aina yake ya uchezaji ni tishio kwa mabeki wengi VPL. Ana akili kubwa ya kunusa hatari, ni mastraika wachache sana ambao wangeweza kujitega pale kati ya Wawa na Kennedy.
8: Presha ya waamuzi dhidi ya Simba, imewaumiza Simba leo. Bao la Fraga lilikua halali kabisa.
9: Edward Songo👏 Asante sana. Nilichokiona kwako mwanzoni, umekithibisha leo. Perfomance bora sana dhidi ya Simba
10: Kichuya hakua fiti. Luis Muquisone, yes. Kuna kitu ndani yake. Alifanya majukumu yake ya msingi na wakati fulani akaingia kati kufanya jukumu la Ajib
Nb: Tukutane Airport😀

Simba imeanza vibaya mzunguuko wa pili ligi kuu ya Vodacom baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa JKT Tanzania katika mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru
Bao pekee la JKT Tanzania lilifungwa na Adam Adam kwenye dakika ya 25 baada ya walinzi wa Simba na mlinda lango Beno Kakolanya kuzembe kucheza krosi

Mabingwa hao watetezi hawakuwa na mchezo mzuri kabisa kwenye kipindi cha kwanza ingawa katika kipindi cha pli juhudi zilionekana
Katika hali ya kushangaza, Fraga alifunga bao maridadi kwa mpira wa kichwa mapema kwenye kipindi cha pili lakini bao hilo lilikataliwa na waamuzi baada kudhaniwa ameotea
Lakini picha za marudio Azam TV zimeonyesha dhahiri Fraga hakuwa ameotea
Matokeo haya yatazidi kumuweka matatani kocha Sven Vandenbroeck na haitakuwa jambo la kushangaza kama atafutwa kazi
Hii ni kutokana na ukweli kwamba Simba imeshuka kiwango ukilinganisha na wakati alipokabidhiwa kutoka kwa Patrick Aussems
Ni wazi ushindi ambao amekuwa akipata umetokana na ubora wa wachezaji na sio mbinu zake



Wachezaji ambao ni wagonjwa (sio majeruhi)
Shomari Kapombe
Rashid Juma

Yanga ilipokuwa chini ya Mwinyi Zahera, mechi ya kwanza ya mzunguko wa kwanza msimu huu iliyochezwa Uwanja wa Uhuru ilifungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting ambayo kesho Februari, 8 itakutana nao tena.
Bumbuli amesema:-“Mwanzo kweli walitufunga na tuliacha pointi tatu, pale walibahatisha wasitarajie tena kuokota dodo chini ya Mbuyu hilo halipo kwa sasa tuna mpango mwingine kabisa.
“Timu imeanza kuimarika na muunganiko ni imara tutapambana kupata pointi tatu tunajua kwamba wao wanaongea sisi tutafanya kwa vitendo,” amesema.
Yanga ipo chini ya Luc Eymael kwa sasa mchezo wake wa hivi karibuni ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Lipuli na Ruvu Shooting nao walishinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar.

Wachezaji majeruhi
1) Mzamiru Yassin
2) Miraji Athumani
3) Deo Kanda
4) Erasto Nyoni
Wachezaji ambao ni wagonjwa (sio majeruhi)
5) Shomari Kapombe
6) Rashid Juma

Mashabiki wa Simba leo wanaweza kupata nafasi ya kuwashuhudia wachezaji wao wapya Shiza Kichuya na Luis Miquissone kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa uwanja wa Uhuru
Nyota hao waliosajiliwa mwezi uliopita kwenye dirisha dogo, baada ya kukaa nje kwa takribani wiki tatu wakisubiri hati za uhamisho wa Kimataifa, sasa zimewasili
Ilianza kuwasili ITC ya Kuchuya juzi usiku na jana Simba ikathibitisha kupokea ITC ya Miquissone
Kichuya alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Simba kabla ya kuuzwa Pharco Fc ya Misri mwanzoni mwa mwaka jana
Amerejea baada ya kuvunja mkataba wake wa miaka miwili na timu hiyo iliyokuwa imemtoa kwa mkopo
Miquissone alionekana kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar

Mshambuliaji Muargentina, Odion Ighalo akiwa ameshika jezi ya Manchester United baada ya kutimiza ndoto za kujiunga nayo kwa mkopo kwa dau la Pauni Milioni 4 kutoka Shanghai Shenhua ya China. Ighalo ambaye amesema yeye ni ‘shabiki kufa’ wa United tangu akiwa mdogo kwao, Nigeria enzi hizo klabu hiyo inaongozwa na mshambuliaji, Andy Cole atakuwa analipwa Pauni 165,000 kwa wiki, nusu tu ya mshahara wake wa China, Paun 330,000 PICHA ZAIDI GONGA HAPA