
Takwimu za ADEYUM Vs Biashara
KIPINDI CHA KWANZA
Pasi alizopiga kwenda mbele : 8
Pasi alizopiga kurudi nyuma (Backpass) : 3
Pasi alizopoteza : 3
Pasi aliyopita akiwa kwenye nusu ya Biashara (zilizofika) : 1
Pasi aliyopiga akiwa kwenye nusu ya Yanga (Zilizofika) : 11
Krosi: 0
Block : 1
Faulo alizocheza : 1
Faulo alizochezewa : 1
Mipira ya Juu aliyocheza : 4
Shot on Target : 0
Shot off Target : 1
KIPINDI CHA PILI
Pasi alizopiga kwenda mbele : 5
Pasi alizopiga kurudi nyuma (Backpass) : 3
Pasi zilizopotea: 4
Pasi aliyopiga kwenye nusu ya Biashara : 0
Pasi alizopiga kwenye nusu ya eneo la Yanga (Zilizofika) : 5
Krosi : 0
Block: 1
Faulo alizocheza : 0
Faulo alizochezewa : 0
Mipira ya juu aliyocheza : 3
Shot on Target : 0
Shot of Target : 0
Hii ina maana gani kwa Adeyum?
Kwa jicho la kawaida, kwa kutazama ‘style of play’ ya mahitaji ya mfumo wa 4-3-3 aliotumia Mkwasa, hapa unaweza kuona Adeyum alifeli. Alikua chini mno, hakuonekana kabisa akipanisha timu mbele, kuattack space za pembeni na kupiga krosi.
Lakini kwa kutazama jinsi Yanga walivyokua wanacheza, ni ngumu sana kumlaumu Adeyum. Kwanini?
Ili beki wa pembeni upande na uweze kushambulia ni lazima uwe na uhakika na vitu vitatu
.
.
Kwanza timu yako iwe inamiliki mpira sana kwenye nusu ya wapinzani, uwe na winga atakakutengeneza nafasi/ njia za kupita na tatu, uwe na uhakika ni nani anabaki kuziba nafasi yako.
Kwa Yanga leo, asilimia 65 ya umiliki wa mpira waliufanya wakiwa kwenye zone yao. Makame na Fei walikua eneo moja, walipiga pasi nyingi fupi na back pass.. Hali hii ilimfanya Adeyum na Mustafa kugusa mpira mara nyingi wakiwa nyuma
.
.
Pili, Sibomana aliathirika na mfumo wa leo. Alicheza kwenye mstari wa kati, Ngassa hakua na speed yake tuliyoizoea. Hakutengeneza njia nyingi upande wa kushoto, ilikua ngumu sana kwa Adeyum kusogea juu.
Tatu, ni nani wakumzibia nafasi. Makame ndie holding pekee aliyekua eneo la nyuma. Kasi yake sio nzuri, mtu mwingine wa kumtegemea alikua Sonso, kasi yake haikua nzuri pia. Ni ngumu kwa Adeyum kutake risk kupanda mbele
.
.
Kitakwimu alikua hovyo, lakini kimchezo, alibaki kufanya jukumu lake la msingi, KUKABA TU
.
.
© Imeandaliwa na Allykamwe