USAJILI: SIMBA YAMNASA ALIYEWAONDOA MABINGWA AFRIKA

Klabu ya Simba imemalizana na Kiungo wa Kimataifa wa Msumbiji Luis Jose Miquissone ambaye alikuwa akiichezea klabu ya UD Songo ya nchini humo kwa mkopo.

Luis ndiye aliyeifungia UD Songo bao dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka jana na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, matokeo ambayo yaliitupa Simba nje ya michuano hiyo.

Kiungo huyo tayari amekabidhiwa jezi ya ‘mnayama’ na kocha wa timu hiyo Sven Vandenbroeck.

#Usajili #LuisMiquissone #SimbaSC #UsajiliSimba @miquissone7

TFF: MASHABIKI NJOONI MAPEMA JUMAMOSI ILI KUEPUSHA USUMBUFU

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limewataka mashabiki wa soka watakao hudhuria mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga kujitokeza mapema katika uwanja wa Taifa ili kuepuka usumbufu.

Kumekuwa na mazoea kwa mashabiki kuchelewa kujitokeza uwanjani hali inayo sababisha misururu mirefu ambayo wakati mwingine hupelekea watu kuumizana.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi (TPLB) Ibrahim Mwayela makao makuu ya Shirikisho hilo yaliyopo Karume jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza mashabiki kujitokeza mapema.

Kuhusu usalama, Mwayela amesema kila kitu kinaenda sawa na vikao na vyombo vya ulinzi vimefanyika na amewatoa hofu mashabiki watakao jitokeza kuwa suala la ulinzi litaimarishwa vizuri. “Kumekuwa na mazoea ya mashabiki kuchelewa kujitokeza uwanjani na kusababisha usumbufu mkubwa hivyo nawaasa kuhakikisha wanakuja mapema,” alisema Mwayela.

@tanfootball @clifordmariondimbo @yangasc @simbasctanzania
#wapendasokaupdates

Mlinda mlango wa klabu ya Juventus Mattia Perin amejiunga na klabu ya Genoa

OFFICIAL|
Mlinda mlango wa klabu ya Juventus Mattia Perin amejiunga na klabu ya Genoa kwa mkopo hadi mwisho mwa msimu.

Perin ameshindwa kuwania namba mbele ya Mkongwe Gianluigi Buffon na Wojciech Szczęsny
. .
Prepared by @anode360 Proudly Sponsored by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates .

Chama cha soka nchini Ghana ‘GFA’ kimetangaza kumtimua kocha wa timu ya taifa Kwesi Appiah

OFFICIAL |
.
Chama cha soka nchini Ghana ‘GFA’ kimetangaza kumtimua kocha wa timu ya taifa Kwesi Appiah pamoja na wasaidizi wake wote waliokuwa wakisaidiana nae wakati anaitumikia nafasi hiyo.
.
Pia GFA imetanagaza kuwafuta kazi makocha wote wa timu za taifa za wanaume na wanawake yaani kuanzia zile za vijana hadi za wakubwa.
.
Appiah mwenye umri wa miaka 59 alichukua mikoba ya kuifundisha Ghana mwaka 2017 akichukua nafasi ya Avram Grant aliyetimka Ghana kufuatia kutolewa kwa timu hiyo kwenye hatua ya nusu fainali ya Afcon 2017.
.
Kwesi hakuwa na wakati mzuri katika kikosi cha Black stars alikuwa ana matokeo ya yasiyoridhisha ndani ya timu hiyo jambo lililowafanya mabosi wake wachukue uamuzi huu mgumu.
.
Takwimu zake akiwa na Black stars🇬🇭.
🏟Mechi-20.
✅Kushinda-9.
❌kupoteza-6.
⛔Sare-5.
.
Licha ya kushinda mechi za hivi karibuni za kuwania kufuzu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika 2021 dhidi ya Afrika kusini na Sao tome and princes kocha huyo wa zamani wa Khartoum amejikuta akitimuliwa yeye pamoja na jopo la wasidizi wake.
°
°
Prepared by @anode360 Proudly Sponsored by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

PROFESSIONALISM🙌🏿🙌🏿 Philip Lahm raia wa Ujerumani katika maisha yake ya soka

PROFESSIONALISM🙌🏿🙌🏿
Philip Lahm raia wa Ujerumani katika maisha yake ya soka amecheza mechi 752 na hajawahi kupata kadi nyekundu.
.
Mlinzi huyo wa zamani wa klabu za VfB Stuttgart,Ft Gen Munchen na Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani kwa sasa ana umri wa miaka 36.
.
Alistaafu soka mwaka 2017,na anakadiriwa kuwa na utajiri wa zaidi ya $ 100 milioni ana mafanikio kadhaa kwenye soka akiwa amefanikiwa kuchukua makombe na tuzo mbalimbali.
.
Orodha ya mataji na tuzo binafsi alizowahi kushinda Philip Lahm.
🏆Kombe la dunia x1.
🏆Uefa Champions league x1.
🏆German Cup x6.
🏆German Champion x8.
🏅Mchezaji bora wa Bayern munichx1.
🏆Club world cup x1.
🏆Uefa super cupx1.
🏆German Super Cup x3.
🏆German League cupx1.
🏆mchezaji bora wa Ujerumani x1.
.
.
🙃Unamkumbuka Lahm kwa lipi?
°
°
Prepared by @anode360

FATAKI NA CHECHE ZA ARSENAL VS MAN UNITED PALE EMIRATES USIKU WA KWANZA WA MWAKA 2020

.
inaandikwa na @danirito_thomson
.
Bonge la game kama show za L`EMPIRE BAKUBA na ile miondoko ya KWASU KWASU Dance ikiongozwa na Le Grande PEPE
.
L`EMPIRE BAKUBA ni kundi la Muziki lililoongozwa na PEPE KALLE, miaka ya 70, tuachane na Pepe wa kale, kuna NICOLAS PEPE na ile Arsenal waliwachezesha United mithiri ya Kwasu Kwasu dance, united walinata na beat tu
.
Turudi kwenye tactics sasa
.
LineUp ya United ilimkosa McTomminay pia Pogba, hii inamaanisha nini? Anaanza Fred na Matic, Kuanza kwenye lile dimba la chini kuliinyima Man United foward passes, United walipiga sana side way passes, short diagonals nyingi sana, ilikua afya sana kwa Arsenal
.
Ole anajua mwenyewe ni sababu gani anayo mapenzi ya dhati na Lingard, ila alipaswa awe connector ila ukweli ni kwamba alikua poor sana, kulikua hakuna huduma kule kwa Martial,James na Rashford
.
Ila ushindi ulianzia kwenye tactical masterclass ya Mikel Arteta, he had a perfect plan. Kwanza kabisa Arsenal walifika kwenye kila eneo, intensity ya hali ya juu, wali win kila second ball, hadi hapo kwa United ikawa Game Over walicheza kwasu kwasu dance tu
.
Swipe👉 picha utayoiona ni shape ya Arsenal ikiwa inashambulia, Auba anakaa kwenye pembe ya box kumzuia Bissaka asitackle cross za Kolasinac 1v1 ambae hakufanyiwa tracking na James sababu walitegemea kuvizia counter, na kuzuia hilo Xhaka alicover eneo la Kolasinac kwenye half space mbele ya James
.
Pepe akamvuta Shaw kwenye chaki, Maitland Niles akafanya inverted movement kuongeza idadi ya midfield na wakati huo huo akimlinda Rashford, Torreira akifanya kazi chafu kumalizana na Lingard, Ozil akawapa maswali Fred na Matic, game ikawa imeishia hapo
.
“Pitisha yeye, pitisha yeye, zonga na ng’ako ine ..”🎼 aliimba PEPE wa sasa kwa sauti ya Pepe Kalle na akapitishiwa akitoka kule kwenye chaki wakati Shaw kageuza mgongo, na ndio maana alicheza kwenye chaki ili afaidi zile V-PASS akiwa anaingia kwenye box wakati Shaw anaufinya uwanja mpira ukiwa upande wa pili
.
Hiyo mistari aliyoimba Pepe ipo kwenye nyimbo ya Pepe Kale inayoitwa “BONNE ANŃE” ikimaanisha HAPPY NEW YEAR
.
Bonne Anńe 2020.

Design a site like this with WordPress.com
Get started