Real Madrid kunasa mshambuliaji kutoka flamengo

Taarifa kutoka Uhispania zinasema kuwa Real Madrid wamefikia makubaliano ya kumsaini Reinier Jesus kutoka Flamengo – (Sky Italia.)

..
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 amemaliza vipimo na sasa atasaini mkataba miaka mitano huko Santiago Bernabeu.


Reinier alifunga mabao sita katika mechi 14 alizocheza Flamengo mnamo 2019.

Paris Saint Germain wanatarajia kumpa mkataba wa kudumu nyota Mauro Icardi

Paris Saint Germain wanatarajia kumpa mkataba wa kudumu nyota Mauro Icardi kutoka Inter majira ya joto …
..
Mshambuliaji huyo wa Argentina kwa sasa yupo PSG kwa mkopo wa msimu mmoja, lakini atapewa mkataba wa miaka minne na mabingwa hao wa Ufaransa msimu huu.

… Icardi amefunga mabao tisa katika mechi 11 za Ligue 1 kwa msimu huu wa 2019-20.

Taarifa kutoka Coastal Union.

BAKARI NONDO MWAMNYETO NI MCHEZAJI HALALI WA COASTAL UNION NA ANA MKATABA WA KUITUMIKIA COASTAL UNION ZAIDI YA MWAKA.

BAKARI NONDO MWAMNYETO HAJAUZWA WALA KUNUNULIWA NA KLABU YOYOTE NDANI NA NJE YA TANZANIA

HIVYO KUTANGAZA AU KUMUHUSISHA YAKUWA AMENUNULIWA NA KUTOLEWA KWA MKOPO KWA KLABU YAKE YA COASTAL UNION NI KUIKOSEA KLABU YA COASTAL UNION.

COASTAL UNION INATOA ONYO KWA YOYOTE ANAETOA HABARI BILA KUULIZA KWA WAHUSIKA WAKUU WA KLABU.

OWE BONYANGA MRITHI WA MOLINGA.

.
.

Mshambuliaji David Molinga wa Yanga, ni miongoni mwa nyota wawili wakimataifa wanaotarajiwa kuachwa na klabu hiyo wakati huu wa dirisha dogo la usaliji.
.
Tarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Moja ya sababu zilizowakasilisha Mabosi wa timu kwa Molinga. ni kitendo cha utovu wa nidhamu alichokifanya katika mchezo dhidi ya Biashara united (Daresalaam) pale alipofanyiwa mabadiliko na KOCHA Charles Bonface mkwasa kupindi cha kwanza cha mchezo huo, mchezaji huyo hakurishishwa na Sub hiyo akaamua kutoka kwenye vyumba vyakubadilishia nguo nakuvaa nguo zake za kawaida kisha kuchukua usafiri (Bodaboda) nakuondoka uwanjani.
.
Kitendo hicho kilitafusiliwa kama dharau kwa mchezaji huyo kwa KOCHA wake, benchi la ufundi na hata uongozi kwa Ujumla, tayari klabu ya Yanga imeshaleta mrithi wa Molinga ambaye ni mshambuliaji Owe bonyanga kutoka TP Mazembe ya Congo DR

Credit Prisca Kishamba

Beno Kakolanya amesema kuwa mbinu zake binafsi zilimfanya aweze kucheza mkwaju mmoja wa Penati hapo jana.

Baada ya kuiwezesha klabu ya Simba kutinga katika Fainali ya Kombe la mapinduzi ,Golikipa wa klabu hiyo Beno Kakolanya amesema kuwa mbinu zake binafsi zilimfanya aweze kucheza mkwaju mmoja wa Penati hapo jana.

#SokaplaceUPDATES

@danirito_thomson @officialchristz

YANGA KUMTUPIA VIRAGO DAVID MOLINGA


Viongozi wa Klabu ya Yanga wameafikiana kuachana na Mshambuliaji David Molinga aliyekuwa akiichezea klabu hiyo kwa mkopo na kusajili wachezaji wengine wanaoamini wataisaidia timu hiyo kwa nidhamu ya hali ya juu

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema, wapo kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba na Molinga aliyeshindwa kufikia malengo kwa mujibu wa mkataba wake wa miaka miwili akitokea kwao, DR Congo

Amesema, “Mbadala wa Molinga atajulikana kwani bado tuna nafasi na tunaendelea kusaka mchezaji anayeweza kuwa msaada kwenye kikosi chetu ambacho kinahitaji maboresho kabla ya dirisha kufungwa.”

Molinga aliyetibuana na viongozi kwa kitendo alichokionesha alipofanyiwa mabadiliko katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara, amekuwa ni mchezaji wa tano aliyesajiliwa na Kocha Mwinyi Zahera kutimka Jangwani

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Zahera waliondoka ni Sadney Urikhob, Juma Balinya, Issa Bigirimana na Maybin Kalengo. Molinga anaondoka akiwa kinara wa ufungaji wa Yanga katika Ligi Kuu Bara akiwa na magoli manne

James Kotei anatarajia kutua Yanga kwa mkopo.

Kiungo fundi wa zamani wa timu ya Simba sc ambae kwa sasa anakipiga katika klabu ya Kaizer Chiefs James Kotei anatarajia kutua Yanga kwa mkopo.

Awali yanga ilikuwa na mpango wa kumnasa kiungo mkabaji kutoka Zasco Utd Anthony Akum raia wa Kenye, kumbe Kaizer Chiefs nao walikuwa na mpango wa kumnasa mchezaji Huyo.

Sasa bas! kutokana na ukaribu waliyonao Yanga na Kaizer wamefanya kubadilishana, Yanga wamuache Akum, nao Kaizer wamuache James Kotei atue jangwani.

#fullsokatzupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started