kiungo wa Ajax Donny van de Beek amesema kuwa hata kwenda vilabu vingine mnamo Januari

kiungo wa Ajax Donny van de Beek amesema kuwa hata kwenda vilabu vingine mnamo Januari, licha ya kuripotiwa kusakwa na Manchester United pamoja Real Madrid.


“Nimesema hapo awali na nitasema tena: Nitaendelea kubaki Ajax msimu huu. Na labda msimu ujao pia. “Hizi ripoti kuhusu Real Madrid au Man United ni ishara nzuri, lakini sio muhimu sasa. Nimesema nitabaki Ajax na nitafanya hivyo kwa asilimia 100.”

..
Van de Beek amefunga mabao sita na amehusika kwenye pasi 4 za mwisho katika mechi 16 za Eredivisie msimu huu.

Michael Olunga ameteuliwa kuwania tuzo ya Soya AWARDS (KENYA) katika kipengere cha mwanamichezo bora wa mwaka, ….

Mchezaji wa kimataifa wa Kenya anayechezea klabu ya Kashiwa Reysol ya Japan Michael Olunga ameteuliwa kuwania tuzo ya Soya AWARDS (KENYA) katika kipengere cha mwanamichezo bora wa mwaka, ….

Na hii ni baada ya kuwa na msimu bora katika timu ya taifa pamoja na klabu yake huko Japan kwani alifanikiwa kufunga mabao 29 katika mechi 33 na kufunga mabao 4 katika mechi 7 za timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars)

Serie A joto la ubingwa lapamba moto

#Updates | Mtafutano Serie A |
:
✍️ Baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Atalanta, Inter sasa wamefikisha alama 46 kileleni wakiwa wamecheza mechi 19, mechi 1 zaidi ya anayemfuata Juventus yenye alama 45 wakicheza mechi 18. Endapo Juventus watashinda hii leo watapaa kileleni katika msimamo wa ligi hiyo.
:
Msimamo timu tano za juu ulivyo.
1: Inter pts 46 | mechi 19
2: Juventus pts 45 | mechi 18
3: Lazio pts 42 | mechi 18
4: Atalanta pts 35 | mechi 19
5: Roma pts 35 | mechi 18.
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

#EPLUpdates | City kurudi nafasi ya Pili __________?

#EPLUpdates | City kurudi nafasi ya Pili __________?
.
Man City hii leo watakuwa wageni wa ASTON VILLA katika dimba la VILLA Park majira ya 1:30 Usiku, kufungwa kwa Leicester City Jana kutaipa nguvu CITY kwani endapo wakishinda hii leo watasogea nafasi ya Pili na kuishusha Leicester CITY katika nafasi hiyo. Aston Villa wapo nafasi ya 17 na alama zao 21 hawana muendelezo mzuri katika mechi zao huku wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Burnley.
:
Mechi Nyingine Hii Leo Ligi Kuu Uingereza.
Bournemouth Vs WATFORD | 11:30 Jioni.
.
#bakinasisi__
#NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Design a site like this with WordPress.com
Get started