
Muwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu Simba Mo Dewji, amesema kuwa kilichotokea kwenye akaunti zake jana usiku baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Mtibwa Sugar ni bahati mbaya.
Mo amesema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Twitter ikiwa ni saa 13 tangu alipotangaza kujuzulu nafasi ya uenyekiti na kwamba angebaki kama muwekezaji na kuangazia zaidi katika maendeleo ya miundombinu na soka la vijana.
Usiku wa kuamkia Januari 14 Mo Dewji alitangaza kujiuzulu kutokana na Simba kushindwa kutwaa kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa goli moja na Mtwibwa katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Baaada ya kutoa kauli hiyo mashabiki wa Simba walimtaka muwekezaji huo kutafakari upya uamuzi wake kwa madai kuwa tatizo huwa halikimbiwi bali linakabiliwa.
#tbconline







✍️ Mourinho anahitaji washambuliaji wawili Januari hii kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Kane. Mshambuliaji wa AC Milan Krzysztof Piatek, 24, ni mmoja kati ya wachezaji wanaotupiwa macho sambamba na mshambuliaji wa Napoli Fernando Llorente 34 na mshambuliaji wa Crystal Palace Christian Benteke, 29. (Independent)
:
:


© Tar 15, Jumatano