Rasmi samatta kuanza kuitumikia EPL…..Akiwa Aston villa

Timu ya Aston Villa ya England inakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji, Mtanzania Mbwana Samatta kwa dau la pauni Milioni kumi sawa na bilioni 30 za kitanzania.

Samatta ni chaguo namba moja la kocha wa Aston Villa Dean Smith katika kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwenye kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania amekuwa kivutio kikubwa kwa timu za England tangu afunge goli kwenye mchezo waligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Liverpool.

Taarifa za kina zinasema hivi sasa pande mbili za timu hizo ziko kwenye mazungumzo ya mwisho ili kukamilisha usajili huo na kocha wa Aston Villa anaonyesha kumtaka sana Samatta ili kuziba nafasi ya mshambuliaji wa Kibrazil Wesley ambae ni majeruhi.

Hata kama usajili huo utakamilika leo au kesho Mbwana Samatta hataweza kucheza mchezo ujao wa ligi ya dhidi ya Brighton kwasababu atakuwa bado hajakamilisha vibali vya kufanya kazi lakini itakuwa habari njema kwake kwasababu itakuwa ametimiza ndoto yake ya kucheza England.

Frank Lampard anasubiri utimamu wa N’Golo Kante kabla ya mchezo wa Chelsea dhidi ya Newcastle tarehe 18/1/2020



Arsenal na Tottenham wapo njia moja kumwania mlinzi wa Bournemouth Nathan Ake lakini mlinzi huyo wa zamani wa Chelsea huenda akarejea darajani kulingana na mkataba wake kutoka Blues kuelekea Bournemouth kuwa na chaguo la kumrudisha tena kwa pauni 40m

Kiungo wa klabu ya Everton Andre Gomes ameanza mazoezi mara baada ya kupona majerha

Kiungo wa klabu ya Everton Andre Gomes ameanza mazoezi mara baada ya kupona majerha yake ya kifundo cha mguu alichoumizwa na nyota wa Tottenham Hotspurs Son Heung-Min wakati timu hizo zilipokutana katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza
.
.

Kocha wa klabu hiyo Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa kiungo atarejea kuanzia wiki ijayo
.

.
#sokaonlineupdates

Kamata msimamo wa VLP baada ya mechi ya leo kuchezwa

.

1. Simba Sc Pointi 38 Mechi 15.
2. Coastal Pointi 30 Mechi 17
3. Azam Fc Pointi 29 Mechi 14.
4. Namungo Pointi 28 Mechi 15.
5. Kagera Pointi 27 Mechi 17.
6. Jkt Pointi 26 Mechi 17.
7. Lipuli Fc Pointi 25 Mechi 17.
8. Yanga Pointi 25 Mechi 13.
9. Polisi Tz Pointi 24 Mechi 15
10. Mtibwa Pointi 22 Mechi 15.
11. Prisons Pointi 21 Mechi 16.
12. R.Shooting Pointi 20 Mechi 17.
13. Alliance Pointi 20 Mechi 16.
14. Mbao Pointi 18 Mechi 17.
15. Biashara Pointi 18 Mechi 17.
16. Mwadui Pointi 17 Mechi 15
17. Kmc Fc Pointi 14 Mechi 16.
18. Mbeya Pointi 13 Mechi 17.
19. Singida Pointi 10 Mechi 16.
20.Ndanda Pointi 09 mechi 17.

#fullsokatzupdates

Leo • Mbao FC Vs Simba Sc | ⏰ 10:00 Jioni | 🏟️ CCM Kirumba | 🏆 Vodacom Premier League.

#VplUpdates | Leo • Mbao FC Vs Simba Sc | ⏰ 10:00 Jioni | 🏟️ CCM Kirumba | 🏆 Vodacom Premier League.
:
Kuelekea pambano la ligi kuu ya kandanda Tz bara, kati ya Mbao FC ya Jijini Mwanza na Simba Sc hii leo, nimekusogezea Taarifa kutoka ndani ya klabu hizo.
:
🔥 MAKOCHA WANENA YAO.
Kocha wa Mbao “Abulmutiki Khaji” 🗣️”Ukiangalia Simba ni wazuri maeneo yote, kwahiyo tumewaandaa vizuri wachezaji na hatutawapa nafasi ya kumiliki mpira, tayari Mtibwa Sugar wameshatuonyesha kwamba inawezekana” alisema Kocha huyo msaidizi Khaji.
.
Kocha Simba Sc Sven 🗣️”Naamini mchezo utakuwa na ushindani, lakini kutokana na lengo latu ni kuhakikisha tunashinda na kuondoka na pointi tatu.”
.
❌ WACHEZAJI WANAOWEZA KUKOSEKANA
Mboa Fc | Said Khamis – Nahodha.
.
Simba Sc | kiungo Mzamiru Yassin, Deo Kanda na Miraji Athuman walioumia katika mechi zilizopita.
.
🎯 NAFASI TIMU HIZI ZILIPO KWENYE LIGI
Mbao ipo nafasi ya 14 kwa pointi 18 baada ya mechi 16. Simba wanaoongoza Ligi kwa alama 35 kwa michezo 14.
.
⏰ KUMBUKUMBU INASEMAJE.
Simba itawakabili ‘Wabishi’ hao ikiwa na rekodi mbaya kwani mara ya mwisho kukutana timu hizo kwenye uwanja huo, walilala bao 1-0, ikiwa chini ya Kocha Patrick Aussems aliyerushiwa chupa za maji na mashabiki baada ya mpambano.
.
🗣️ UTABIRI WAKO ____________________?
.
#bakinasisi__
#NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Design a site like this with WordPress.com
Get started