Kocha wa Aston Villa, athibitisha kusajiliwa kwa mbwana samatta

Kocha wa timu ya Aston Villa, Dean Smith amethibitisha kwamba mpango wao wa kumsajili nyota wa Kitanzania Mbwana Samatta utakamilika hivi karibuni

Akizungumza baada ya mechi yao ya jana dhidi ya Brighton ambayo ilimalizika kwa timu hizo kwenda sare kwa kufungana bao moja kwa moja, kocha huyo amesema kila kitu kimeenda vizuri na Mbwana Samatta alikuwa akikamilisha kusaini nyaraka zilizokuwa zimesalia.

Kocha Smith amesema Samatta ni mshambuliaji bora na atakuwa na msaada mkubwa kwao kutokana na rekodi yake nzuri ambapo alifunga magoli 43 katika michezo 98 kwenye ligi ya Ubelgiji alipokuwa akiichezea timu ya KRC Genk.

KAGERE KUREJEA DIMBANI SIMBA IKISAKA POINT KWA ALLIANCE

Mfungaji bora Wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Meddie Kagere atarejea dimbani Leo kama Kocha ataamua kumtumia wakati Simba ikiikabili Alliance FC ya Jijini Mwanza katika mchezo Wa ligi kuu kwenye uwanja Wa CCM Kirumba.

Kagere ambaye alikosekana katika mchezo wa kati kati ya wiki Simba ikishinda bao 2-1 dhidi ya Mbao FC baada ya kupata kadi tatu za njano katika mchezo iliyopita na kikanuni akalazimika kukosa mechi dhidi ya Mbao

John Bocco pamoja na Ibrahim Ajibu ndiyo waliyoiongoza safu ya ushambuliaji ya Simba katika mchezo uliopita na kurrjea kwa Kagere ambaye ndiye kinara Wa mabao kunampa nafasi kocha machaguo zaidi.

#wapendasokaupdates

Nafikiria juu ya hatma yangu” – kocha wa Yanga

Kocha wa klabu ya Yanga, Luc Eymael ameonesha kutofurahishwa na waamuzi wa mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC uliopelekea kufungwa bao 1-0 jana …

“Nataka nizungumze suala la waamuzi, kweli ile ni kadi nyekundu lakini kabla mchezaji wa azam hajafanyiwa madhambi alimvamia mchezaji wa Yanga, mwamuzi wa pembeni alikuwepo pale lakini akasema hakuona kitu. Mwamuzi akaja kwangu kunipa kadi ya njano nikampa mkono lakini akaukataa, kwanini mko hapa, ni kwasababu mimi ni mzungu?, ni ubaguzi dhidi ya watu weupe?, kiukweli nimefadhaika sana”, ….


“Kwa hali hii ilivyo, ninafikiria juu ya hatma yangu hapa, nitaongea na kamati juu ya hatma yangu. Siridhishwi na kinachoendelea hapa, sizungumzii juu ya Azam FC bali nazungumzia juu ya vitu hivi vingine kwenye mchezo”, alisema Luc

Real Madrid wameunganishwa kushinda mbio za kumsaini kiungo wa Ajax Donny van de Beek

Real Madrid wameunganishwa kushinda mbio za kumsaini kiungo wa Ajax Donny van de Beek – (Daily Star)

..
Manchester United pia wamekuwa wakimfukuzia Mholanzi huyo, lakini sasa anatarajiwa kukamilisha dili la pauni milioni (47,61m) kwenda Santiago Bernabeu.


Van de Beek amefunga mabao nane katika mechi 26 kwenye mashindano yote kwa Ajax msimu huu.

Klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia imetangaza kunasa saini ya mchezaj wa Algeria Redouane Zerdoum

Klabu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia imetangaza kunasa saini ya mchezaj wa Algeria Redouane Zerdoum kwa mkataba wa miaka tatu na nusu.

Klabu hiyo imetumia dola 250,000 za Marekani kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye amefunga mabao 5 katika michezo 11 kwenye Ligue 1 ya Algeria msimu huu.

#SokaplaceUPDATES

Ally mtoni aomba msamaha kwa.makosa aliyofanya jana

#Repost From @ally_mtoni

Naomba msamaha kwa wana mchezo wote kwa kadi niliyoipata siku ya jana na tukio nililofanya kwenye mchezo wetu vs Azam fc,kweli mchezo wa mpira ni mchezo wa furaha na upendo kwa kuwa ni ajira ila changamoto za hapa na pale zipo,pia naomba msamaha kwa wachezaji, viongoz wangu wa @yangasc na pia hata wa @azamfcofficial na hata viongozi wenye dhamana na soka letu @tanfootball na sitaweza kuja rudia tukio la aina ile 🙏🙏🙏

YANGA YALIA NA BODI YA LIGI MABADILIKO YA UWANJA

Uongozi wa klabu ya Yanga umeilalamikia Bodi ya ligi (TPLB) kwa kubadilisha tena sehemu ya mchezo wao dhidi ya Singida United kutoka Arusha kurudi Singida muda mfupi huku wao wakiwa wameshafanya maandalizi ya awali.

Siku chache zilizopita Bodi hiyo ilitangaza kuwa mchezo huo utaenda kupigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwakua uwanja wa Liti (zamani Namfua) unahitaji marekebisho lakini leo kumetoka taarifa nyingine kuwa mchezo huo utapigwa mkoani Singida.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk. David Luhago amesema tayari wameshafanya maandalizi ya usafiri kwa kuweka booking kwenye ndege na kulipa sehemu ya pesa (advance) kwenye hoteli watakayo fikia hivyo hawaelewi jinsi ya kurudisha gharama zao baada ya mabadiliko hayo.

Dk. Luhago amesema kwa kawaida kama kuna mabadiliko ya ratiba ya mchezo taarifa inapaswa kutolewa saa 48 kabla lakini Bodi haikufanya hivyo na kuwashtukiza kuwaambia mchezo huo utapigwa mkoani Singida nasi Arusha tena. “Bodi ya ligi ilituandikia barua kuwa mchezo wetu wa Jumanne dhidi ya Singida utapigwa uwanja Sheikh Amri Abeid Arusha lakini wamebadili tena kuwa tutaenda Singida wakati sisi tushalipa gharama za awali. Taarifa ilipaswa kutolewa mapema, sisi tumejiandaa kuwa tunasafiri kwenda Arusha,” alisema Dk. Luhago.

#wapendasokaupdates

MABADILIKO RATIBA CAF.

.
shirikisho la soka Barani Afrika Caf limebadilisha ratiba ya mechi kwa ajili ya kufuzu fainali za Afcon2021 na zile za kombe la dunia 2022 kutokana na kurejesha ratiba ya zamani ya michuano ya Afcon kutoka Juni-julai hadi januari-februari.
.
Awali mechi za kufuzu Afcon 2021 ilitakiwa zichezwe mwezi Agosti 2020 baada ya kuchezwa za awali lakini zitachezwa mapema mwezi machi.
.
Na zile za kufuzu Kombe la dunia 2022 zimehairishwa na sasa zitachezwa mwezi oktoba ili kupisha mabadiliko hayo yaliyofanyika mapema siku ya jumatano.
.
Raundi mbili za mechi za kufuzu Afcon 2021 zitapigwa mapema mwezi machi na raundi moja itapigwa mwezi Juni huku zile za mwisho na za kufuzu michuano hiyo zitafanyika 31 agosti hadi septemba 8/2020.
.
🏆Afcon2021itafanyika pale Cameroon🇨🇲.
🏆Kombe la dunia 2022 litafanyika pale Qatar🇶🇦.
.
.
Cc. @anode360
.
#sokaonlineUpdates.

Design a site like this with WordPress.com
Get started