SIMBA ILIBANWA MBAVU UHURU KWA MTINDO HUU

KIKOSI cha Simba Jana kimebanwa mbavu Uwanja wa Uhuru mbele ya JKT Tanzania kwa kufungwa bao 1-0 mchezo wa Kwanza wa mzunguko wa pili msimu wa 2019/20.
Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vanderbroeck ilifungwa bao dakika ya 24 kupitia kwa mshambuliaji wa JKT Tanzania, Adam Adam aliyefunga bao hilo kwa kichwa kilichozama nyavuni na kumshinda mlinda mlango, Beno Kakolanya.
Licha ya Simba kuongeza juhudi za kusaka ushindi kipindi cha pili mabao yalikuwa magumu kwani walishindwa kufurukuta mbele ya JKT Tanzania ambao walikuwa na spidi kubwa mwanzo mwisho.
Kipindi cha pili Simba ilifunga bao kupitia kwa Gerson Fraga dakika ya 52 mwamuzi alisema kuwa ni bao la kuotea kwa Simba.
Licha ya Simba kufanya mabadiliko kwa kumtoa Ibrahim Ajibu nafasi yake ikachukuliwa na John Bocco, Francis Kahata kuchukua nafasi ya Shiza Kichuya na Gerson Fraga nafasi yake kuchukuliwa na Clatous Chama bado mambo yalikuwa magumu.
Nyota mpya wa Simba Luis alionyesha makeke kwa mara ya kwanza kwa dakika tisini huku Kichuya akicheza kwa dakika 45 ndani ya Uwanja.
Simba inabaki nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 50 na leo itakuwa zamu ya Yanga Uwanja wa Uhuru dhidi ya Ruvu Shooting.
Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Sven kuambulia kichapo akiwa kwenye bechi baada ya kupokea mikoba ya Patric Aussems aliyepigwa chini jumla.
Sven amesema kuwa sababu kubwa ya kushindwa kupata matokeo ni washambuliaji kutokuwa makini kutumia nafasi walizopata pamoja na kuwa na wachezaji wengi majeruhi.

Visit website

HUU HAPA USHAURI WA SALEH JEMBE KWENDA SIMBA, YANGA YATAJWA

KUTOKANA na kichapo cha bao 1-0 walichopokea Simba mbele ya JKT Tanzania jana, Februari 7,2020 kupokelewa kwa mtindo wa kipekee kwa mashabiki na viongozi.

Huu hapa ushauri wa Saleh Jembe kwa Simba:-Nimesikia kiongozi mmoja wa Simba akilia kuwa ndani yao kuna hujuma. USHAURI WANGU :- Wawe watulivu, Papara za namna hiyo kama anazoonyesha kiongozi huyo zimekuwa ADUI mkubwa wa Simba mara kadhaa.

Kwani Simba ni nani asifungwe. Kama kuna jambo walishughulikie huko na si kulalama hadharani. Akishindwa anaweza kusema watu wamuelewe.

Yanga walionyesha weledi, walifungwa mechi 2 mfululizo, WAKATULIA, wakajipanga na KURUDI mchezoni.Leo wanafanya vema. Huenda hao viongozi wa Simba wanaweza KUJIFUNZA hapo na kupunguza UJUAJI uliopindukia.

Visit website

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck atetea wachezaji wake

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema walipoteza mchezo wa jana dhidi ya JKT Tanzania kutokana na kukosa bahati kwani walitengeneza nafasi nyingi

Aidha Sven amesema wachezaji wote wa Simba ni wazuri na yeyote anaweza kumtumia na wakapata matokeo

Mbelgiji huyo ametoa kauli hiyo baada ya kutupiwa lawama kuwa haeleweki katika upangaji wa timu

“Kilicho tokea na sehemu ya mpira hakuna wa kumlaumu, ni kweli tulibadilishiwa uwanja kutoka Taifa hadi Uhuru na pia tuliwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na kuwa majeruhi lakini huwezi kusema ndio iliyopelekea kupoteza mchezo,” alisema Sven

“Timu yetu ina wachezaji wazuri ambao wanaweza kucheza mechi yoyote na wakaipa Simba ushindi”

Sven pia amelaumu ukaribu wa michezo jambo linalosababisha ‘fatigue’ kwa wachezaji

Lionel Messi hana nia ya kuondoka barcelona

Nyota wa Barcelona, Lionel Messi hana nia ya kuondoka klabuni hapo licha ya maoni yake ya hivi karibuni kuhusu Eric Abidal, (Sky Sports)


MuArgentina huyo alikuwa kwenye mzozo na mkurugenzi wa michezo wa Barca baada ya kuwakosoa hadharani wachezaji wa Barca kwamba hawakuwajibika kipindi cha Ernesto na messi kumtaka “atoe majina” ya wachezaji waliomwangusha Ernesto ….

inasemekana kuwa Messi anafura kusalia Barca hadi majira ya joto, pamoja na kuanza kufungua majadiliano na waajiri wake juu ya upanuzi wa mkataba wake unaofikia ukomo 2021.

Design a site like this with WordPress.com
Get started