DAKIKA 90 ZA LIVERPOOL VS MANCHESTER UNITED .

Inaandikwa na @danirito_thomson
.
Kwanza kabisa ilikuwa mechi nzuri sana, OLE alimpa wakati mgumu KLOP, timu zote ziligawana dakika za kukaa na mpira, kuna muda anakaa nao united kuna muda anakaa nao Liverpool ila mwisho kabisa Liverpool anamaliza na ushindi nadhani sio matokeo ya kushangaza, just another day in the office
.
OLE alifanya assignment vizuri akaja na 3-5-2 pale nyuma Shaw na Salah na Mane kwa Lindelof kwasababu hawa wachezaji wa Liverpool hukaa zaidi karibu na box na sio pembeni, juu Martial na James, ila James alikuwa na kazi ya kunusa hatari ya counter attack na kwenda kulia ama kushoto na kumuacha Martial katikati
.
KLOP aliendelea na 4-3-3 japo this time full backs zake United waliwazuia kupanda juu kwa kupitia wingbacks Williams na Bissaka
.
Fred the Red, a boy from Brazil, bonge moja la perfomance, alikaba sana na akiwa na mpira alibreak channels, alitembea na mpira kutoka chini mpaka juu, bad enough kulikuwa hakuna msaada wenye kuendeleza quality kama hiyo
.
Van Dijk “Cyrus the Great” alipaa akaweka kamba safiii, haya ndo matatizo ya zonal marking kwenye mipira ya kona, man marking ni bora zaidi kama unacheza na timu ina big man kama Van Dijk, zonal imesababisha ka’William kawe karibu na jitu VVD 😂
.
Martial uwa anamfanya Rashford acheze vizuri ila pia Martial bila Rashford ni kitendawili, Rashford atakuwa nje kwa miezi 2-3 hili ni pigo, mechi kubwa ndizo za Rashford, mechi ya jana ilimuhitaji sana mzaliwa wa Manchester kupambana na hasimu wake
.
Goli la Salah, refa kasema twende kazi hata kama ni offside ilitokea, sasa kama refa hajapuliza ye hafanyaje!? Kwangu mimi fresh tu hakuna kosa pale, Allison kamuona Salah kapiga assist, na kwenye kushangilia yeye ndo wakwanza kufika kwa Salah, kama movie vile 😂, Salah anapata goli lake la kwanza dhidi ya United mbele ya lile jukwaa la The Kop, what a moment
.
Ila dah kwa zile mbinu za jana, tungeshuhudia mechi kali zaidi ya ile kama McTomminay, Pogba na Rashford wangekua ndani, japo bado Liverpool nadhani angeshinda, ila ingekua real battle
.
Muda nao unatuchelewesha tu, Liverpool ni bingwa, ni swala la kuusubiri muda wenyewe uamue
.
I love this game

MAYWEATHER KURUDI TENA ULINGONI MWAKA HUU⁣ ⁣

Baada ya kuisha mpambano wa UFC baina ya Conor McGregor na Donald Cerrone ambapo McGregor alishinda katika sekunde ya 40, Mayweather aliweka picha mbili katika ukurasa wake wa Instagram kuashiria kwamba anarudi ulingoni mwaka huu. ⁣

Picha ya Kwanza inasomeka Mayweather VS McGregor 2 akimaanisha atafanya marudiano ya pambano lake na McGregor na jingine ni Mayweather VS Khabib Nurmegomedov.⁣

Bosi wa UFC, Dana White alithibitisha kuongea na Mayweather na kusema kuna lengo la mapigano hayo na kuna kitu kitafanyika mwaka huu.⁣

Mchezo wa Mwisho na McGregor mwaka 2017, Mayweather alishinda dhidi ya Nyota huyo wa UFC.⁣

Aston Villa wanaripotiwa kujaribu kumsaini Olivier Giroud kutoka Chelsea mwezi huu

Aston Villa wanaripotiwa kujaribu kumsaini Olivier Giroud kutoka Chelsea mwezi huu. Mfaransa ambaye amekuwa kwenye shinikizo la kuondoka Stamford Bridge na Dean Smith anatamani kuunga mkono kampeni ya kumchukua mshambuliaji huyo baada ya Wesley kupata jerala litakalomweka nje ndani ya miezi tisa

Kamata Ratiba Ya Soka Leo

:
👉England – Championship
23:00 West Bromwich Albion vs Stoke City
:
👉Italy – Serie A
22:45 Atalanta vs SPAL
:
👉France – Cup
22:55 St-Pryve St-Hilaire vs Monaco
:
👉Netherlands – Eerste Divisie
22:00 Jong Ajax vs FC Dordrecht
22:00 Jong FC Utrecht vs Roda JC Kerkrade
:
👉Algeria – Ligue 1
18:00 JS Kabylie vs MC Oran
19:00 ASO Chlef vs USM Alger
:
👉Egypt – Premier League
15:30 Aswan FC vs Wadi Degla FC
20:00 El Geish vs Al-Ittihad Al-Sakandary
22:30 El Zamalek vs Al Masry
:
👉Morocco – Botola Pro
21:00 Olympic Club de Safi vs Wydad Casablanca
:
👉Ghana – Premier League
18:00 Bechem United vs Eleven Wonders FC
:
👉International – Club Friendlies
13:00 Sevilla vs SV Sandhausen
17:00 Dinamo Moscow vs Zaglebie Lubin
17:00 FK Akhmat vs Botosani
18:30 FC FCSB vs Lokomotiv Moscow
:
Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Mambo machache niliyoyaona kwenye mchezo wa ligi kuu England kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United. .

.
1 Jurgen klopp ndani ya mfumo wa 4-3-3 🙌 eneo la Kiungo leo alianza na Henderson, kiungo cha ulinzi mtulivu sana presha ya Liverpool ilikuwa mikononi mwake anakaba anapora mpira anajua kunusa hatari ipo wapi. Pale mabeki wake wa pembeni wanapoenda kushambulia.
.
.
2 Virgil Van Djick 🙌 ile paundi milioni 75 imerudi na Liverpool wanaendelea kula pensheni tu mpira yote ya hewani ilikuwa ikiishia kwake alikuwa anajua kucheza timing na washambuliaji wa Manchester United kwenye counter attack 👏 kwangu mie ndo nyota wa mchezo.
.
.
3 Lallan mechi ilimshinda kwa sababu ilikuwa na matumizi mengi ya nguvu kwa nature ya viungo wa Manchester United, klopp ,sijajua aliwaza nini kumtoa Chamberlain, kwenye eneo la kiungo .Chamberlain ana nguvu ya kutosha kupush timu kutoka chini kwenda juu pengine kama matokeo yangekuwa tofauti angejilaumu sana.
.
.
4 Fred, some how anazidi kuonyesha kiwango kizuri kwenye mechi kubwa 💪 kuna mda alikuwa anafanya kazi mbili kwa wakati mmoja aje chini kuanzisha mashambulizi asogee juu kushambulia. Alikosa msaada kwenye eneo la kiungo.
.
.
5 William mechi kubwa ameonyesha kiwango kizuri mbele ya Salah, alikuwa anajua kucheza na timing ya mguu wake wa kushoto alikuwa hamuachi mita moja mpaka apokee mpira kwa sababu Salah ni mzuri kwenye kufanya cuts mbele ya mabeki.
.
.
6 kuingia kwa Mata, na Green Wood Manchester United wakarudi kwenye mfumo wa 4-3-3 walihitaji kushambulia ila wakasahau kuwa kama Liverpool wana wachezaji wenye spidi mbele bao bora la Mo Salah, ile assist ya Becker 🙌 .
.
.
7 Manchester United kacheza na Anfield na sio na Liverpool 🙌 kama ulitabiri huu mchezo na ukapatia njoo inbox nikupe vocha yako ya elf 2.
.
.
Prepared @azizi_mtambo_15
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Kamata Matokeo Ya Soka Jana

:

👉VodacomPremierLeague
FT Allience FC 1- 4 Simba SC
:
👉England – Premier League
FT Burnley 2 – 1 Leicester City
FT Liverpool 2 – 0 Manchester United
:
👉England – Championship
FT Nottingham Forest 3 – 1 Luton Town
:
👉Spain – LaLiga Santander
FT Mallorca 4 – 1 Valencia
FT Real Betis 3 – 0 Real Sociedad
FT Villarreal 1 – 2 RCD Espanyol
FT Athletic Bilbao 1 – 1 Celta Vigo
FT Barcelona 1 – 0 Granada
:
👉Spain – LaLiga SmartBank
FT Elche 1 – 1 Alcorcon
FT Deportivo La Coruna 1 – 0 Cadiz
FT Racing Santander 1 – 1 Las Palmas
FT Real Oviedo 1 – 1 SD Huesca
FT Tenerife 1 – 0 Girona
FT Extremadura 1 – 2 Almeria
:
👉Italy – Serie A
FT Milan 3 – 2 Udinese
FT Bologna 1 – 1 Verona
FT Brescia 2 – 2 Cagliari
FT Lecce 1 – 1 Inter
FT Genoa 1 – 3 Roma
FT Juventus 2 – 1 Parma
:
👉Germany – Bundesliga
FT Hertha BSC 0 – 4 FC Bayern München
FT SC Paderborn 07 1 – 4 Bayer Leverkusen
:
👉France – Cup
FT Athletico Marseille 0 – 2 Rennes
FT Dijon 5 – 0 Nimes
FT Montpellier 5 – 0 Caen
FT Rouen 1 – 4 Angers
FT Lorient 0 – 1 Paris Saint-Germain
:
👉Netherlands – Eredivisie
FT VVV-Venlo 1 – 1 PSV Eindhoven
FT Ajax Amsterdam 2 – 1 Sparta Rotterdam
FT FC Emmen 1 – 0 Heracles
FT ADO Den Haag 2 – 0 RKC Waalwijk
:
👉Netherlands – Eerste Divisie
FT FC Den Bosch 2 – 3 Go Ahead Eagles
:
👉Belgium – First Division A
FT Cercle Brugge 1 – 2 Royal Antwerp
FT Anderlecht 1 – 2 Club Brugge
FT Zulte Waregem 0 – 3 Genk
:
👉International – Friendlies
FT Sri Lanka 0 – 3 Bangladeshi
FT El Salvador 0 – 1 Iceland
:
👉International – Club Friendlies
FT PFC Sochi 0 – 0 Chindia Targoviste
FT 1. FC Union Berlin 1 – 2 St. Gallen
FT Basel 0 – 2 Hamburger SV
FT Rakow Czestochowa 1 – 3 Ural
:
👉Algeria – Ligue 1
FT NC Magra 1 – 1 Paradou AC
:
👉Egypt – Premier League
FT Al Mokawloon Al Arab 0 – 2 Al Ahly
:
👉Morocco – Botola Pro
FT OCK Khouribga 1 – 0 Renaissance Club Zemamra
FT RSB Berkane 2 – 2 Raja Casablanca
:
👉South Africa – Premier League
FT Bloemfontein Celtic 1 – 1 Chippa United FC
FT Polokwane City 1 – 1 Lamontville Golden Arrows
FT SuperSport United 1 – 2 Mamelodi Sundowns FC
:
Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Mambo 10 nilioyaona Alliance Vs Simba

1: Jonas Gerrald Mkude. WOW🙌 Kwangu ndio Man of the match leo👏 Ameimarika sana kiuchezaji. 85 % ya pasi zake zilielekea mbele. Akaipush sana Simba kuisogelea Alliance. Movement zake kwenye boksi ni za akili sana.. Haishangazi kuona amefunga mabao 2, kwenye mechi 2🙌

2: Minziro 🤔 Naheshimu sana kazi yake but leo alikua poor sana kimbinu. Kipindi cha kwanza aliiweka timu kwenye Low Block (Ikabie chini) huku akijua kabisa hana quality ya wachezaji wa kufiti kwenye plan hiyo. Walijazana nyuma na bado Simba walipiga pasi nyingi katikati ya msitu wao

3: Beno Kakolanya 🙌 Perfomance bora sana kutoka kwenye mikono yake👏 Kuna mkwaju aliutoa kipindi cha kwanza, ambao kama ungeingia, Alliance wangekua mbele kwa mabao 2 na pengine utulivu wa Simba ungepotea kabisa. Well done Beno👏

4: Juma Nyangi🙌 Chongo aliyeonekana kwenye msafara wa vipofu. Peke yake, kwa uwezo wake, alikua na madhara makubwa kwa Simba kila alipokua na mpira mguuni. Acha niendelee kumfatilia kwa karibu

5: Chama🙌 Akili yake ya mpira ilikua kubwa kuliko changamoto ya uwanja. Kila alipoisogelea 18 ya Alliance, kila mtu alihisi hatari. Binafsi, naamini alistahili kufunga bao zaidi ya moja leo
.
.
6: Sven👏 Yes, leo alikua na Plan B ya kucheza Kirumba. Kipindi cha pili, Simba walipunguza sana pasi fupi kwenye phase ya mwisho ya uwanja. Kasi ikaongezeka pia kwenye kufanya maamuzi.

7: Kipa wa Alliance alikua na makosa mengi sana. Bahati nzuri kwake, Simba walitumia dakika 45 za kipindi cha kwanza kumsoma. Wakachelewa kiasi. Wangemgundua mapema udhaifu wake, Alliance wangefungwa zaidi ya Mabao 5.

8: Pascal Wawa🙌 This Lad ana akili sana ya mpira. Timing yake kupokonya mpira ni ya ubora wa juu mno. Ni hatari pia akisogea juu. Ni hatari zaidi anapoamua kupiga pasi ya mita 25🙌

9: Hassan Dilunga 🙌 HD inayofanya kazi kwenye viwanja vibovu. Kuna chenga alimpiga mtu juu ya dimbwi la maji 😀 Ndie kiungo pekee wa Simba, mpaka sasa mwenye aina tofauti ya mpira katikati ya uwanja.

10: Kagere. Simba wanahitaji kumtengenezea nafasi nyingi kwenye eneo la mwisho kurejesha confidense yake.
Nb: Mwenye msimamo nauomba😀

Design a site like this with WordPress.com
Get started