.
Inaandikwa na @danirito_thomson
.
Kwanza kabisa HAPPY BIRTHDAY midfielder kisheti, ishi tu, endelea kuwafurahisha WAKALI WA TERMINAL jukwaani
.
Hasan Dilunga akili na mwili na style kama mJapan Shinji Kagawa, anafit kama namba nane wa kulia au kushoto kwenye 4-3-3 anafit kama 10, 7,11 kwenye 4-2-3-1
.
Kiungo mshambuliaji anaeweza pia kucheza winga ya kisasa sahau wale mawinga mbio mwisho mita 100 kwenye kibendera, NO thank you
.
Alianza kuonekana kwa waTanzania akiwa kijana mdogo miaka ya 2013, alikua na mwili usiotisha ila football brain na miguu yenye kipaji
.
Alikuwa pale kwa Masau Bwire msemaji mwenye simu zake, Mpapaso-CEO, kipindi kile wakiitwa Ruvu Shooting
.
Yanga ya kocha Ernest Brandts walimsajili Dilunga kutoka Ruvu Shooting, wengi waliangalia ule mwili wake wakasahau football is upstairs kwenye ubongo
.
Alianza slow kidogo ila mwendo ukachanganya
.
Akaja Hans Van Pluijm na ile Yanga yenye Nizar Khalfan, Niyonzima msimu wa 2015, kuna kipindi alipokezana na Niyonzima ila bado pale jangwani hawakupiga stori zake wakikutana vijiweni
.
Mnaikumbuka ile Stand United chini ya matajiri wa migodi ACCACIA? ile iliyobadili jezi ya orange ya chama la wana mpaka Blue na kuwachefua wapiga debe wa stand mitaa ya Ngokolo na Ndala pale ardhi yenye madini yake Shinyanga, basi ile Stand ilimchukua Dilunga kwa mkopo kutoka Yanga 2015
.
Stand iliyokuwa na Kiemba ya kocha mfaransa Patrick Liewig, pale Dilunga gari lilipungua kasi injini ilichoka kidogo kiwango kilikula pause
.
Akasajiliwa tena kule JKT Ruvu, kisha Ajax ya Bongo Mtibwa chini ya mwalimu Katwila gari likawaka kiwango kikarejea, Simba akamuona na kumsajili kile kipindi wakitafuta nani mbadala wa Niyonzima ambae alisajiriwa ila alionekana majeruhi spana mkononi
.
Dilunga wa Simba hapo sasa ndipo akawa HD tunaemjua, makocha wote pale msimbazi wamemtumia huyu Kagawa
.
Ila naona Sven Van de Broeck anamuhusudu sana bwana HD, ile kasi yake na akili kumkichwa kwenye ule mfumo wa 4-2-3-1
.
HD anampa Sven faida katika mafungu matatu, winga na ile kasi, kiungo na ule ubongo na mshambuliaji na lile jicho
.
Nimeona niandike hii kabla TCRA kwa ushirikiano na NIDA hawafunga line yangu
.
💪