TANZIA.KAGERA SUGAR FC

#repost from @kagerasugarfc1 TANZIA.

Kagera Sugar Company Limited kupitia Kagera Sugar Football Club inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wa mchezaji wetu tegemezi katika kikosi cha #wanankurukumbi YUSUPH VALENCE MHILU ambacho kimetokea usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam.
Tunapenda kutoa pole kwa Ndugu jamaa na marafiki wote mlioguswa na msiba huu pamoja na Familia ya ndugu yetu YUSUPH MHILU na tunaahidi kuwa nanyi bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu mnachopitia kwa kuondokewa na mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIDIWE.
#gonetoosoon

POLE SANA MHILU.@mhyusufu26
Poleni sana #wanankurukumbi

ZAHERA: BENO KAKOLANYA ANAWEZA KUWA KAMA SAMATTA

Itakumbukwa, Papaa Mwinyi Zahera alipokuwa kocha wa Yanga aliwahi kuingia katika mgogoro na mlinda Mlango Beno Kakolanya kiasi cha kumuondoa kikosini, na kumfanya Kakolanya aende Simba.
.
Leo akizungumza kwenye #SportsHQ Zahera aliombwa kutaja wachezaji wa Kitanzania ambao anaona wanaweza kutamba kwenye Ligi za Ulaya mithili ya @samagoal77. Miongoni mwa wachezaji akiotaja ni Kipa wa @simbasctanzania, Beno Kakolanya. “Ana akili nyingi ya mpira” alisema Zahera.
.
Unadhani Kakolanya anaweza kucheza timu gani Uingereza?

Cc @efmtanzania

VAN DIJK KUHUSU MAGUIRE

“Mlinzi wa kati wa LIVERPOOL Jogoo wa kidachi VAN DIJK alipoulizwa na Mtandao wa Goal .com alijisikia vipi Rekodi yake ya usajili £75m kutoka SOUTHAMPTON- Liverpool ilipovunjwa na Harry Maguire £80m kutoka LEICESTER -Manchester united
Amesema hakuna kilichobadilika kwake suala LA kununuliwa kwa bei kubwa ni suala LA soko hiyo ni bahati kwake haliwezi kumuumiza
Ila amemtaka MAGUIRE kuwa makini Kwakua Manchester united INA pressure kubwa.

Hivi wakati MWINGINE Manunuzi na mishahara ya wachezaji hayamaanishi EEEEEEEH
MAGUIRE kanunuliwa-£80M
ANalipwa £190,000k

Van DIJK amenunuliwa-£75m
Analipwa £180,000k
…………………

#Tetesi Za Soka Barani Ulaya

:

✍️ Manchester United inaandaa kitita cha £43m ili kumnunua mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Moussa Dembele, baada ya Marcus Rashford kuumia mgongo. (Foot Mercato, via Manchester Evening News)
.
✍️ Inter Milan wako tayari kulipa kitita cha £11m na ada nyingine ili kumsajili kiungo wa kati Christian Eriksen kutoka Tottenham mwezi huu. (Sky Sports)
.
✍️ Manchester United watalazimika kulipa ada ya juu ya uhamisho kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, mwezi huu badala ya kumchukua kwa mkopo – lakini mchezaji huyo yuko tayari kuondoka PSG. (Manchester Evening News)
.
✍️ Kujiunga na Liverpool ndio “lengo kuu” la mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 23, ambaye anataka kucheza katika ligi kuu ya premia. (Bild, via Sport Witness)
.
✍️ Inter Milan wanakaribia kumsajili kwa mkopo beki wa Chelsea Victor Moses, 29, kujiunga na mkufunzi wake wa zamani Antonio Conte. Fenerbahce, klabu ambayo kiungo huyo wa kimataifa wa Nigeria anachezea kwa mkopo imeridhia kumuachilia. (Mail)
.
✍️ Mkufunzi wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anasema Gunners “ilituvunja moyo” lipoondoka Highbury na kuhamia uwanja wa Emirates. (Evening Standard)
.
✍️ Everton imekataa ofa mbili za kumnunua beki Mason Holgate, huku Newcastle, Bournemouth na Sheffield United zikiwa miongoni mwa timu zinazomtaka mchezaji huyo wa miaka 23. (Football Insider)
.
✍️ Liverpool haiko tayari kumpoteza kiungo wa kati wa Uswizi Xherdan Shaqiri, 28, licha ya Roma kuonesha nia ya kutaka kumnunua mwezi huu. (Sky Sports)
.
✍️ Manchester United imekiri kuwa ilishindwa na Real Madrid katika kinyang’anyiro cha usajili wa kiungo wa kati wa Ajax Donny van de Beek, 22. (Star)
.
✍️ Klabu ya Uhispania ya Celta Vigo imekuwa ikiwasiliana na Southampton kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati, Oriol Romeu lakini Saints hawataki Mhispania huyo wa miaka 28-kuondoka (Southern Daily Echo)
.
✍️ Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie ameionya United kutokimbilia kumrudisha uwanjani Marcus Rashford, 22, baaada ya kiungo huyo mshambulizi kuumia mgongo. (Manchester Evening News).
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

NABIL BENTALEB KUREJEA EPL AKITOKEA BUNDESLIGA

Kiungo wa zamani wa TOTTENHAM HOTSPUR BENTALEB RAIA wa ALGERIA YUPO NCHINI UINGEREZA KATIKA KLABU YA NEWCASTLE UNITED Kufanya vipimo vya AFYA Akitarajia kujiunga na NEWCASTLE Kwa mkopo hadi mwisho wa msimu akitokea KLABU ya SHALKE 04 YA UJERUMANI

BENTALEB ALiondoka TOTTENHAM MWaka 2017 na kujiunga na Shalke 04 .tangu March 2019 amekuwa na mzozo na mwalimu wa 04 hali iliyompelekea muda flani kutolewa katika kikosi cha Kwanza na kushushwa timu B kutokana na sababu za kinidham

Rasmi Samatta atangazwq kua mchezaji wa Aston Villa

MICHEZO: Klabu ya Aston Villa @AVFCOfficial ya nchini England yatangaza rasmi kumsajili Mbwana Samatta kutoka Klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji

Samatta (27) ambaye ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania #TaifaStars amesaini kandarasi kuitumikia Klabu hiyo kwa muda wa miaka 4 na nusu

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kwa ada ya Paundi Milioni 10 (takriban Tsh. Bilioni 30) anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza katika Ligi Kuu Soka nchini England

Design a site like this with WordPress.com
Get started