
Yanga imepata ushindi wa kwanza katika uwanja wa Liti (zamani Namfua) baada ya kuifunga Singida United mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika muda mfupi uliopita.
Tangu Singida ilipopanda daraja misimu mitatu iliyopita Yanga haikuwa imepata ushindi katika uwanja huo ikiambulia sare au kipigo.
Katika mchezo huo ambao Yanga ilitawala sehemu kubwa bao la kwanza lilifungwa dakika ya 12 na mshambuliaji David Molinga baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Singida.
Kipindi cha pili Yanga iliongeza mengine mawili dakika ya 59 na 74 yaliyofungwa na Haruna Niyonzima na Yikpe Gislain wakati Six Mwakasega akiifungia Singida bao la kufutia machozi dakika ya 84.
Winga mpya Bernado Morrison ambaye alicheza kwa mara ya kwanza ameonyesha uwezo mkubwa huku ikionekana kama unaweza ukawa usajili mzuri kwa Yanga.
#wapendasokaupdates

:





✍️ Liverpool wako tayari kumuuza Xherdan Shaqiri kwa £25m msimu wa joto lakini haitaki kumuachilia winga huyo wa Uswizi wa miaka 28, aondoke kwa mkopo mwezi huu. (Liverpool Echo)
Rio Ferdinand, Martin Keown na Joe Cole 🗣️ “Arsenal haina beki imara” .