
1: Benard Morrison.. What a player🙌 Akiwa hajazoeana vizuri na wenzake, akiwa kwenye kiwanja kibovu na bado aliamua kufanya mapenzi na mpira👏 Ni mtu tishio aliyekosekana kwenye kikosi cha Yanga tangu Simon Msuva.
2: Luc Eymael. Angalau leo presha yake ilikua chini, Yanga ikaonekana inacheza kwa utulivu zaidi. Licha ya changamoto ya kiwanja, bado Yanga ilikua ikifanya build up kutokea chini
.
.
3: Tshishimbi🙌 Siku akiwa kwenye kiwango bora, Yanga inakua bora. Alikua kiongozi kwa mabeki wake na akawa backup kwa viungo wake wa juu.
4: Napenda sana mikimbio ya Balama Mapinduzi kwenye eneo la mwisho. Kasi yake, pasi zake zinawapa kitu cha ziada mastraika wa Yanga.
5: Molinga.. Yes. Ameanza kuimarika. Ari yake kiuchezaji iko juu sana. Ni straika pekee wa Yanga mpaka sasa mwenye uwezo mkubwa wa kunusa hatari kwenye eneo la mwisho
6: Chuji👏 Dakika zake chache uwanjani zilitosha kabisa kutukumbusha Taifa kitu gani tumekimisi kwa viungo wetu wa ‘kisasa’
7: Sumbi🙌 yule namba 27 wa Singida anajua sana. Ni mtulivu mno na pasi zake ni za uhakika. Bahati mbaya kwake, yuko katika kiwango bora akiwa na jezi ya Singida.
8: Navutiwa sana na nidhamu ya Jafar Mohamed kwenye kukaba. Akijiongezea bidii mazoezini, akaboresha kasi yake, anaweza kua mtu sahihi sana kwenye eneo lile
9: Singida imepigwa Mabao 3, lakini ni ngumu sana kuacha kuizungumzia mikono ya Owen Chaima🙌 Alikua kwenye kiwango bora sana aisee.
10: Kama Yikpe huwa anajifanyia tathimini ya uchezaji wake basi bao la leo linaweza kumpa mwanga mzuri. Kwa mwili wake, kimo chake, nguvu anatakiwa awe anazurura sana ndani ya boksi na sio nje.
Nb: Kamati mpya oyee😀