Crystal Palace wapo mbioni kumsaini Kyle Walker-Peters kutoka Tottenham – (The Sun) ..

..
Eagles wana hamu ya kumsaini kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa mkopo wenye chaguo la kumnunua, lakini Spurs wangependelea kumuuza dhahiri mwezi huu.
..
..
Southampton pia wameelezea kupendezwa na Walker-Peters, ambaye ameonekana kwenye mechi tatu za Ligi Kuu na Tottenham msimu huu.

NEWCASTLE UNITED IMEFIKIA MAKUBALIANO NA KLABU YA INTER MILAN

NEWCASTLE UNITED IMEFIKIA MAKUBALIANO NA KLABU YA INTER MILAN ILI KUMCHUKUA KWAMKOPO WINGA WA INTER VALENTINO LAZARO UMRI MIAKA 23
LAZARO anatarajia kufanya vipimo vya afya kesho ijumaa ili kujiunga na STEVE BRUCE huku kukiwa na pendekezo LA kumchukua jumla kwa £20m ifikapo majira ya kiangazi

Ally Ally ameigomea klabu ya Yanga kumpeleka kwa mkopo kunako klabu ya JKT Tanzania

-Beki wa klabu ya Yanga, Ally Ally ameigomea klabu ya Yanga kumpeleka kwa mkopo kunako klabu ya JKT Tanzania. Ally amesema alipoambiwa hayupo kwenye mipango ya kocha aliuomba Uongozi wa Yanga umpeleke kwa mkopo KMC na sio JKT Tanzania. Beki huyo ambaye alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea KMC Sasa ameamua kubaki Yanga. Cc @yossima_sports

JKT Tanzania yabadilisha uwanja mechi ya FA

“Kumefanyika mabadiliko ya uwanja na muda katika mchezo wetu wa ASFC baina yetu na Tukuyu Stars ambao ulikuwa uchezwe Januari 25, 2020 katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo saa kumi jioni, badala yake mchezo huo utachezwa katika uwanja wa Uhuru saa nane mchana Januari 25, 2020. Sababu za mabadiliko hayo ni uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.” Jamila Mutabazi Afisa Habari JKT TZ
#SokaplaceUPDATES

Kamata Ratiba Ya Soka Leo

:
👉AzamSportsFederationCup
16:00 KMC FC vs Pan African
16:00 Panama FC vs Mtwivila City
:
👉England – FA Cup
23:00 Northampton Town vs Derby County
23:00 Queens Park Rangers vs Sheffield Wednesday
:
👉Spain – LaLiga Santander
23:00 Osasuna vs Levante
:
👉Spain – LaLiga SmartBank
23:00 Cadiz vs Racing Santander
:
👉Italy – Serie A
22:45 Brescia vs Milan
:
👉Germany – Bundesliga
22:30 Borussia Dortmund vs 1. FC Köln
:
👉France – Ligue 1
22:45 Nice vs Rennes
:
👉Belgium – First Division A
23:30 Standard Liege vs Oostende
:
👉Scotland – Championship
23:05 Dunfermline Athletic vs Dundee FC
:
👉Africa – Champions League
22:00 El Zamalek vs TP Mazembe
22:00 Wydad Casablanca vs USM Alger

👉Ligi kuu Afrika Kusini
22:00 Cape Town City FC vs Black Leopards
22:00 SuperSport United vs Chippa United FC
:
👉Ghana – Premier League
18:00 Sogakope Wafa vs Liberty Professionals
21:00 Legon Cities FC vs Bechem United

Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

LIVERPOOL YAENDELEZA UBABE EPL JANA

Vinara wa ligi kuu soka England Liverpool imeendelea kujikita kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuibuka na ushindi ugenini wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Wolverhampton wanderers katika uwanja wa Molineux

Liverpool walianza kufunga kupitia kwa Jordan Henderson dakika ya 8 kisha Wolves kusawazisha dakika ya 51, lakini kabla ya kipenga cha mwisho Roberto Firmino anaiandikia bao la ushindi Liverpool dakika ya 84 na kuifanya Liverpool kuongeza alama 3 muhimu hivyo kufikisha alama 67 katika msimamo wa ligi huku wakiwa wamekwisha cheza michezo 23

Wolves yenyewe inabaki nafasi ya 7 ikiwa na alama 34 baada ya kucheza michezo 24 wakiwa alama sawa na Tottenham pamoja na Manchester United

Orlando Pirates kuindosha wachezaji wawili kwa mkopo

Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika kusini imetangaza kuwa wachezaji wao Jastice Chabalala na Tebogo Tlolane wameondoka klabuni hapo.

Wawili hawa wanaondoka kuanza mikataba ya mkopo

Justice Chabala atautimikia mkopo wake katika klabu ya Bloemfontein Celtic

Wakati Mchezaji Tebogo amejiunga na klabu ya Maritzburg United zote za Afrika kusini.

#SokaplaceUPDATES

Horoya AC kunasa saini ya mlinzi wa kimataifa wa Mali Salif Coulibaly (31

Klabu ya Horoya AC ya Gueinea imetangaza kunasa saini ya mlinzi wa kimataifa wa Mali Salif Coulibaly (31) kwa mkataba wa mda mfupi.

Mlinzi huyo wa zamani wa vilabu vya TP Mazembe, Al Ahly SC, Raja Casablanca Salif Coulibaly amesaini mkataba wa miezi sita.

#SokaplaceUPDATES

Design a site like this with WordPress.com
Get started