Homa ya korona yamkosesha Odion Ighalo mazoezi

Odion Ighalo alijiunga na Manchester United kwa mkopo hadi mwisho wa msimu katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo atakosa mazoezi na klabu hiyo nchini Uhispania kutokana na hofu kwamba virusi vya corona vinaweza kumzuia kuruhusiwa kuingia nchini Uingereza .

Ighalo mwenye umri wa miaka 30, alisafiri kuelekea mjini Manchester kutoka China wikendi iliopita baada ya kutia saini kandarasi ya mkopo kutoka klabu ya Shenghai Shenhua.

”Angependelea kujiunga na wachezaji wengine ili kuweza kujuana”, alisema Mkufunzi Ole Gunnar Solskjare akizungumza na runinga ya MUTV.

”Lakini hatari ya masharti ya mpakani, hatutaki kuhatarisha”.

Wakati huohuo kiungo wa kati wa Man United Scott McTominay na beki Axel Tuanzebe ambao wote wamekuwa na majeraha ya muda mrefu watasafiri kuelekea Uhispania.

United hawatarudi hadi siku ya Ijumaa kabla ya mechi yao ya ligi ya Uingereza dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 17 February.

AZAM FC YAICHAPA KMC 3-1 NA KUPUNGUZA IDADI YA POINTI

WANAZOZIDIWA NA SIMBA KILELENI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya KMC ya Kinondoni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na kocha Mromania, Aristica Cioaba inafikisha pointi 41 sasa baada ya kucheza mechi 20, ingawa inabaki nafas ya pili nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 50 za mech 20 pia.
Katika mchezo wa leo, mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji wake Muivory Coast, Richard D’jodi dakika ya 25 na Mzambia Obrey Chirwa mawili dakika ya 33 na 43, huku bao pekee la KMC likifungwa na Sadallah Lipangile dakika ya 84.

Mechi nyngine za Ligi Kuu leo, bao pekee la mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga Ndama ‘Falcao’ dakika ya 39 lilitosha kuipa Yanga ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Nayo Coastal Union imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania mabao ya Mtenje Albano dakika ya 69 na Mudathir Said dakika ya 90 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Bao pekee la Mwinyi Elias dakika ya 20 likatosha kuipa Lipuli FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo, Morogoro.
Nayo Mbeya City ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Tanzana Prisons bao pekee la Peter Mapunda kwa penalti dakika ya 13 Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Bao la dakika ya 65 la Sameer Vincent likaisaidia Alliance FC kupata sare ya 1-1 na Mbao FC iliyotangulia kwa bao la Datius Peter dakika ya 55 kwa penalti Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Singida United nayo ikalazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui FC Uwanja wa Liti, SIngida. Mabao ya Singida yalifungwa na Muharami Issa ‘Marcelo’ dakia ya 61 na 90 na ya Mwadui FC yalifungwa na Venance Ludovic dakika ya 24 na Raphael dakika ya 41.
Ndanda SC ikalazimishwa sare ya 0-0 na Namungo FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Kagera Sugar nao wakalazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Visit website

MOLINGA ‘FALCAO’ AING’ARISHA YANGA SC LIGI KUU, YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 UHURU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Ruvu Shooting 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga Ndama ‘Falcao’ dakika ya 39 akimalizia kwa kichwa krosi maridadi ya Ditram Nchimbi kutoka kulia.
Ushindi huo unaifanya Yanga SC ifikishe pointi 37 baada ya kucheza mechi 18, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye point 41 sasa baada ya kucheza mechi 20 na mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 50 za mech 2
Yanga SC nayofundishwa na Mbelgiji Luc Aymael anayesaidiwa na mzawa, Charles Boniface Mkwasa, kocha wa Fiziki, Riedoh Berdien kutoka Afrika Kusini na kipa wa zamani wa klabu, Manyika Peter anayewanoa walinda milango wa timu hiyo wangeweza kuondoka na ushindi mnono zadi kama wangetumia vyema nafasi nzuri walizotengeneza.
Sifa zimuendee kipa Mohamed Makaka wa Ruvu Shooting kwa kuokoa michomo mingine miwili ya Molinda kipindi cha kwanza na mmoja wa Muivory Coast, Yikpe Gislain aliyetokea benchi kipindi cha pili.
Dakika ya 31 Yanga walilalamika kunyimwa penalti baada ya Baraka Mtuwi kumchezea rafu mchezaji wao, Mghana Bernard Morrison kwenye boksi aliyekuwa amefanikiwa kumtoka beki mwingine wa Ruvu Shooting, Kassim Simaulanga upande wa kulia.
Kikosi cha Ruvu Shooting kilikuwa; Mohamed Makaka, Omary Kindamba, Kassim Simbaulanga, Santos Mazengo, Baraka Mtuwi, Zubery Dabi, William Patrick/Shaaban Msala dk58, Shaaban Kisiga, Fully Maganga, Graham Naftali/Saadat Mohamed dk60 na Abdulrahman Mussa/Jamal Mnyante dk62.
Yanga SC; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Ally Mtoni, Papy Kabamba Tshishimbi, Ditram Nchimbi, Haruna Niyonzma/ Said Juma ‘Makapu’ dk90, David Molinga/ Yikpe Gislain dk69, Mapinduzi Balama na Bernard Morrison/Deus Kaseke dk81.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Azam FC imeibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya KMC Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, mabao yake yakifungwa na washambuliaji Muivory Coast, Richard D’jodi dakika ya 25 na Mzambia Obrey Chirwa mawili dakika ya 33 na 43, huku bao pekee la wapinzani wao likifungwa na Sadallah Lipangile dakika ya 84.
Coastal Union ikaibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania mabao ya Mtenje Albano dakika ya 69 na Mudathir Said dakika ya 90 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Bao pekee la Mwinyi Elias dakika ya 20 likatosha kuipa Lipuli FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo, Morogoro.
Nayo Mbeya City ikaibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Tanzana Prisons bao pekee la Peter Mapunda kwa penalti dakika ya 13 Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Bao la dakika ya 65 la Sameer Vincent likaisaidia Alliance FC kupata sare ya 1-1 na Mbao FC iliyotangulia kwa bao la Datius Peter dakika ya 55 kwa penalti Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Singida United nayo ikalazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui FC Uwanja wa Liti, SIngida. Mabao ya Singida yalifungwa na Muharami Issa ‘Marcelo’ dakia ya 61 na 90 na ya Mwadui FC yalifungwa na Venance Ludovic dakika ya 24 na Raphael dakika ya 41.
Ndanda SC ikalazimishwa sare ya 0-0 na Namungo FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Kagera Sugar nao wakalazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa Kaitaba mjin Bukoba.

Visit website

BREAKING: UCHEBE KURUDI BONGO TENA, AZUNGUMZA KUHUSU SIMBA

PATRICK Aussems aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba na kupigwa chini mwishoni mwa mwaka Jana,2019 amesema kuwa anaamini siku moja ataonana na mashabiki wake wa Simba ambao aliowaacha kwa kurudi tena Bongo.

Kwa sasa nafasi yake ipo mikononi mwa Sven Vanderbroeck ambaye jana alipoteza mchezo wake wa kwanza baada ya kuanza kusimamia benchi la ufundi.

Kupitia Ukurasa wake wa Istagram, Aussems amesema kuwa amepokea meseji nyingi ambazo zinamtaka arudi ndani ya Simba jambo ambalo anaamini linaweza kutimia siku moja:-

Visit website

BARCELONA, REAL MADRID JINO KWA JINO KWA TRAORE

KLABU ya Barcelona ipo kwenye mchakato wa kuinasa saini ya nyota wa Wolves, Adama Traore, ambaye alitua kikosini hapo mwaka 2013 akitokea timu ya Barcelona B.
Inaelezwa kuwa Barcelona wanataka kumrejesha mshambuliaji huyo baada ya kuskia kwamba Real Madrid ni miongoni mwa timu inayotaka kuipata saini ya nyota huyo.
Nyota huyo kwa sasa yupo chini ya Nuno Espirito Santo amekuwa na maendeleo mazuri kwenye mechi zake anazocheza kwenye Ligi Kuu England.
Traore anaamini kwamba akirejea kwenye La Liga atamudu mchezo kutokana na uwezo alionao akiwa ndani ya uwanja na timu anayoipenda ni Barcelona.
“Bado nina mkataba ndani ya timu yangu kwa sasa mpaka 2023 ila ikija Barcelona ama Real Madrid nina amini ni suala la kuketi na kuzungumza,” .
Nyota huyo ametupia jumla ya mabao matano na pasi za mabao 10 akiwa chini ya Nuno.

Visit website

Simba kuifuata mtibwa sugar jumapili

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kesho Jumapili kinaelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumanne, Februari 11 kwenye uwanja wa Jamhuri

Vinara hao wa ligi kuu wanakwenda Morogoro wakiwa na lengo moja, tu kuhakikisha wanarejesha furaha ya mashabiki wao baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya KKT Tanzania

Aussems apagawishwa na mashabiki simba ahaidi kurejra

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema amepokea maelfu ya meseji kutoka kwa mashabiki wa Simba wakimtaka arejee kunako klabu hiyo

Aussems ambaye kwa sasa yuko mapumziko huko Ufaransa, ameeleza kuguswa na jumbe hizo kutoka kwa mashabiki wa Simba

Mbelgiji huyo amesema kuwa anaamini siku moja atarudi Simba

“Nimeguswa na maelfu ya meseji nilizopokea kutoka kwa mashabiki wakinitaka nirejee. Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri na mashabiki wa kipekee, nawatakia kila la kheri naamini tutakutana tena wakati mwingine,” aliandika Aussems kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Tangu kuondoka kwa Mbelgiji huyo, timu imeonekana kupunguza kasi siku hadi siku chini ya kocha mpya Sven Vandenbroeck

Jana baada ya kufungwa na JKT Tanzania, mashabiki wa Simba walioshuhudia mchezo huo uwanja wa Uhuru, walikuwa wakiimba jina la Aussems wakiutaka uongozi wa Simba umrejeshe

TFF yakiri Waamuzi bado ni Changamoto VPL

Katibu mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidao amesema bado kuna changamoto katika uchezeshaji wa waamuzi katika mechi za ligi kuu na zile za daraja la kwanza na lipi.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali wa soka kuwa timu zinapendelewa hali iliyopelekea Serikali kupitia kwa Waziri mwenye dhamana, Dk. Harrison Mwakyembe kuliagiza Baraza la Michezo (BMT) kuingilia kati.

Licha ya Kidao kukiri kuwa kuna changamoto ya waamuzi kushindwa kutafsiri sheria hasa kwa wasaidizi lakini sio Tanzania pekee ni suala la dunia nzima.

Kidao amesema “hata kwa nchi zilizoendelea kama Ujerumani, England bado zinatumia teknolojia kama ‘Video Assistance Refaree (VAR), Goal line Technology lakini bado malalamiko bado yapo mengi tu. “Juzi nilikuwa naangalia mechi kati ya Tottenham Hotspur na West Ham licha ya VAR kuamuru bao lakini bado ilionekana kuwa halikuwa sahihi hapo ndipo utagundua kuwa suala la waamuzi ni Changamoto kubwa,” alisema Kidao.

Hata hivyo Kidao amesema wataendelea kuandaa kozi mbalimbali za ndani na nje kwa ajili ya waamuzi ili kuongeza ubora na wamepunguza idadi ya mechi ili kuwapa nafasi ya kupumzika mechi baada ya mechi.

#wapendasokaupdates

SINGIDA UNITED WAPATA PAKUTOKEA

SINGIDA United iliyo chini ya Ramadhan Nswanzurimo imesema kuwa njia ya kuwabakiza kwenye ligi msimu ujao ipo mikononi mwa Mwadui hivyo lazima wapambane kupata pointi tatu.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 imeambulia ushindi mechi mbili, imepoteza mechi 13 na sare nne na pointi zake 10, nafasi ya 20.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana alimesema kuwa wachezaji wana morali kubwa ya kupata pointi tatu mbele ya Mwadui ili waitengeneze njia ya kubaki kwenye ligi.
“Tumekuwa tukishindwa kupata matokeo kutokana na kukosekana kwa muunganiko mzuri ndani ya timu ila kwa sasa tayari mambo yameanza kujipa, tutapambana kupata pointi tatu mbele ya Mwadui ambao watatufungulia njia ya kubaki ndani ya ligi.
“Timu nyingi zitashuka mwishoni mwa msimu hilo lipo wazi, tutakachokifanya ni kuongeza juhudi mara mbili zaidi ushindi utatupa hali ya kujiamini na kuongeza kasi ya kupambana kujinasua hapa tulipo,” amesema.

Visit website

Design a site like this with WordPress.com
Get started