KWAHERI MAMBA!

Achana na alivyoagwa mwaka 2016 wakati akitangaza kustaafu kucheza ligi ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) baada ya kucheza misimu 20 mfululizo.

Wakati ule alipoagwa kucheza ligi hiyo alipata nafasi ya kusema neno lililopata umaarufu, *”what can I say?..Mamba Out”* akimaanisha kuwaaga kwenye mchezo huo baada ya kumaliza muda wake wa miaka 20 akicheza ligi hiyo kubwa Duniani.

Asubuhi ya Jumapili kwa muda wa Marekani na usiku kwa Afrika Mashariki,haikuwa kama ilivyokuwa mwaka 2016 kwa Kobe Bryant (Mamba) kuaga kawaida badala yake alifikia mwisho wake wa kuishi Duniani (miaka 41) akiacha majonzi makubwa kwa wapenzi wa mchezo huo na ulimwengu kwa ujumla kufuatia kifo chake kilichotokana na ajali ya ndege yake binafsi.

Taarifa zimeeleza kuwa Kobe alikuwa njiani kuelekea kilipo kituo chake cha kuendeleza michezo kinachoitwa Mamba Sports Academy ambacho hutoa mafunzo na kuandaa wanamichezo shindani.

Ukiachana na salamu mbalimbali za maombolezo kutoka kote ulimwenguni,Kamishna mkuu wa NBA,Adam Silver amemuelezea Kobe kupitia misimu yake 20 aliyocheza ligi hiyo kama kielelezo tosha cha ushindi na hekima kama mfano bora kwa kizazi kijacho cha wachezaji wa mpira huo.

Tofauti na wachezaji wengi,Kobe aliitumikia Los Angeles Lakers tu katika maisha yake yote ya kucheza kikapu akiitumikia miaka 20 mfululizo akishinda mataji matano,akishinda tuzo ya MVP mara moja pamoja na Kuwa MVP bora wa fainali mara mbili.

Kobe ambaye namba za jezi zake zote mbili (8 na 24) zilistaafishwa kuvaliwa na timu hiyo baada ya kustaafu kwake,anashika nafasi ya nne kwa ufungaji wa muda wote kwenye ligi hiyo,alicheza NBA all-star mara 18,kikosi bora cha NBA mara 15,mlinzi wa muda wote mara 12 mbali na mengineyo.

SEKUNDE 24 ZA MAJONZI MECHI ZOTE*

Haikuwa rahisi kwa wachezaji katika mechi za leo kujizuia kuomboleza kifo cha Kobe Bryant ambapo mechi zote za alfajiri ya leo zililazimika kuchelewa kuanza kwa sekunde 24 kupisha ombolezo la kifo hicho.
.
.
@materekajr
#dailysporttz

BREAKING NEWS | Mcheza Basketball maarufu duniani Kobe Brayant amefariki jioni ya leo kwa ajali ya ndege

BREAKING NEWS | Mcheza Basketball maarufu duniani Kobe Brayant amefariki jioni ya leo kwa ajali ya ndege

Kobe Brayant alizaliwa August 23, 1978 na amefariki akiwa na umri wa miaka 41

Stay Easy brother Kobe 🏀💔

#dailysporttz

Mambo 10 nilioyaona Yanga vs Prison

1: Benard Morrison🙌 Akili kubwa, ufundi mwingi. Jambo gumu zaidi kwa mabeki msimu huu ni kukubaliana na winga fundi, mbishi asiyeogopa
.
.
2: Luc Aymael 👏 Baada ya vichapo viwili, hatimae amepata jibu la Plan gani ni sahihi kulingana na aina ya wachezaji aliowakuta. Siku Balama akielewa vyema majukumu yake, Yanga itakua imara sana inapovuka mstari wa kati

3: Adolf Richard🤔 Kwa Plan aliyokuja nayo leo, inashangaza kwanini alichagua kumtumia Mkandala kwa dakika 10 za mchezo. Adili Buha na Mwashilindi walifanya kazi kubwa kwenye kupokonya mpira lakini walikosa mtu sahihi wa kuwaanzishia shambulizi

4: Niyonzima👏 Shoo alifanya Morrison, muziki alitunga Niyo🙌 Unaona uzoefu wake, ubora wake ulivyowatesa Prison katikati ya kiwanja. Kwangu ndio Man of the match kwenye pambano hili.

5: Yikpe. Kitu kizuri kwake, anafunga siku akiwa hajacheza vizuri. Mpaka sasa Unahisi hatari kwenye movement zake kwenye boksi lakini amekosa utulivu anapokua na mpira mguuni. Pengine akiendelea kufunga, ataendelea kujiamini zaidi.

6: Paul Peter🙌 Amenikosha sana huyu kijana. Kwa umri wake, kwa muda mchache ambao amejiunga na Prison, ameonyesha ubora mkubwa sana. Nje ya matokeo, kitu positive alichoondoka nacho Adolf kwenye mechi hii ni perfomance ya Paul Peter

7: Makame🤔 Aina yake ya mchezo ni hatari kwa wachezaji wa timu pinzani na ni hatari pia kwa Yanga. Nidhamu yake ya mchezo iko chini mno
.
.
8: Nilisema kuhusu Jafary na ninasema tena, kama kuna mchezaji ameimarika kwenye nidhamu ya kulinda kwenye line ya ulinzi ya Yanga basi ni Jafary. Msaada mkubwa kwa sasa ni kucheza upande mmoja na Morrison.

9: Benjamin Asukile🙌 Dume haswa. Direct player. Muda Prison ilipohitaji mtu wa kusogea mbele, alikuwepo kuwapa msaada
.
.
10: Ismail Aziz👏 Mchezaji mzuri anayecheza timu ngumu. Ni winga mzuri wa kisasa anayehitaji changamoto kubwa zaidi

Nb: Ule mjadala wa Morrison vs Deo Kanda tuendelee nao au tumalize tu😀

YANGA YAWAPIGISHA KWATA MAAFANDE WA PRISONS, YATINGA 16 BORA

Timu ya Yanga imefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa.

Bernard Morrison aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 10 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi mmoja wa Prisons kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.

Baada ya bao hilo Prisons wanao nolewa na Adolf Rishard walitulia na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Yanga lakini safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Lamine Moro ilikuwa makini kumlinda mlinda mlango Metacha Mnata.

Yikpe Gislain aliifungia Yanga bao la pili kwa kichwa dakika ya 63 muda mfupi baada ya kuchukua nafasi ya David Molinga akimalizia mpira uliopigwa na Morrison.

Yanga itakuna na Gwambina katika mchezo wa hatua ya 16 bora katika uwanja wa Gwambina uliopo Wilaya ya Misungwi jijini Mwanza.

#wapendasokaupdates

Neymar aonyesha ishara ya vidole viwili mkono wa kulia na vinne mkono wa kushoto

Baada ya kufunga goli dakika ya 52 kwa mkwaju wa Penati, Neymar ameonyesha ishara ya vidole viwili mkono wa kulia na vinne mkono wa kushoto ikiwa na ishara ya namba 24 iliyokuwa namba ya jezi ya mchezaji wa Basketball KOBE BRYANT aliefariki dunia kwa ajali ya helikopta muda
.
.
Wachezaji wa PSG walipata taarifa hiyo kipindi cha mapumziko. Walionekana wakiwa na unyonge na kutoshangilia goli kwa nguvu
.
.
Rest in Peace KOBE BRYANT
#Mamba
.
.
#sokaplaceUPDATES

Kamata Matokeo Ya Soka Jana

:
👉AzamSportsFederationCup
FT Namungo FC 2-1 Biashara United
FT Kagera Sugar 2-0 Mighty Elephant
FT Yanga SC 2-0 Tanzania Prisons.
FT Lipuli FC 2-2 Kitayosa FC (Pen: 4-5)
FT Majimaji FC 1-1 Stand United (Pen: 4-5)
:
👉England – FA Cup
FT Manchester City 4 – 0 Fulham
FT Tranmere Rovers 0 – 6 Manchester United
FT Shrewsbury Town 2 – 2 Liverpool
:
👉Spain – LaLiga Santander
FT Atletico Madrid 0 – 0 Leganes
FT Celta Vigo 0 – 0 Eibar
FT Getafe 1 – 0 Real Betis
FT Real Sociedad 3 – 0 Mallorca
FT Real Valladolid 0 – 1 Real Madrid
:
👉Italy – Serie A
FT Inter 1 – 1 Cagliari
FT Verona 3 – 0 Lecce
FT Parma 2 – 0 Udinese
FT Sampdoria 0 – 0 Sassuolo
FT Roma 1 – 1 Lazio
FT Napoli 2 – 1 Juventus
:
👉Germany – Bundesliga
FT Werder Bremen 0 – 3 Hoffenheim
FT Bayer Leverkusen 3 – 0 Fortuna Düsseldorf
:
👉France – Ligue 1
FT Lyon 3 – 0 Toulouse
FT Nantes 0 – 1 Bordeaux
FT Lille 0 – 2 Paris Saint-Germain
:
👉Netherlands – Eredivisie
FT Vitesse 1 – 1 FC Emmen
FT FC Groningen 2 – 1 Ajax Amsterdam
FT Willem II 0 – 0 PEC Zwolle
FT PSV Eindhoven 1 – 1 FC Twente
:
👉Belgium – First Division A
FT Cercle Brugge 1 – 2 Anderlecht
FT Kortrijk 2 – 2 Club Brugge
FT Royal Antwerp 2 – 1 Zulte Waregem
:
👉AfricaChampions League
FT Al Ahly 1 – 0 Etoile du Sahel
:
👉Africa – Confederations Cup
FT Pyramids FC 0 – 1 Enugu Rangers
FT Al Masry 1 – 0 FC Nouadhibou
FT Horoya AC 2 – 1 Bidvest Wits
FT Djoliba AC 0 – 1 Al-Nasr
FT Esae FC 1 – 5 RSB Berkane
FT Zanaco 2 – 1 Motema Pembe
FT Enyimba 1 – 1 Hassania Agadir
FT Paradou AC 0 – 0 San Pedro
:
👉Egypt – Premier League
FT Al Mokawloon Al Arab 2 – 0 Tanta
:
👉Kenya – Premier League
FT Tusker FC 1 – 1 Ulinzi Stars
:
👉Morocco – Botola Pro
FT Renaissance Club Zemamra 1 – 2 FAR Rabat
FT FUS Rabat 2 – 1 Difaa El Jadida
:
👉South Africa – Premier League
FT Baroka FC 2 – 1 Maritzburg United
:
👉Ghana – Premier League
FT Hearts of Oak 1 – 2 Asante Kotoko
:
👉International – Club Friendlies
FT FC Krasnodar 2 – 1 Jablonec
FT IFK Gothenburg 2 – 3 AaB
FT Arsenal Tula 2 – 2 Mladost
FT FC Tsarsko Selo Sofia 1 – 0 Ural
FT Lokomotiv M 1 – 1 Jeonbuk FC

Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Design a site like this with WordPress.com
Get started