Statement ya Simba SC kuhusu kauli ya Kabwili wa Yanga

Ni siku moja imepita toka golikipa wa Yanga SC Ramadhani Kabwili kuituhumu club ya Simba SC kuwa iliwahi kumuahidi hongo ya gari Toyota IST, endapo angekubali kujipatisha kadi ya tatu ya njano katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania, ukiwa ni mchezo mmoja kabla ya game ya watani wa jadi.

Kama Kabwili angefanya hivyo kwa madai yake anasema kwa kuwa angekosa mchezo unaofuata kikanuni, kiongozi huyo wa Simba SC aliyemtaka kufanya hivyo aliamini kukosekana kwake kungelazimika Yanga kumchezesha Kindoki ambaye kimsingi kwa wakati huo alikuwa hafanyi vizuri katika soka.

Leo Simba SC imetoa msimamo wake na kueleza kukerwa na kauli ya Kabwili ila haijachukua hatua yoyote kwakuwa, mamlaka husika (TFF) imechukua hatua za haraka kuhusiana na hilo, hivyo kama Simba SC imeliachia mamlaka husika kuhusiana na hilo.

BUMBULI: KABWILI AMEKOSEA

Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema mlinda mlango wao Ramadhani Kabwili hakupaswa kutoa tuhuma kwa klabu ya Simba mbele ya vyombo vya habari.

Jana mlinda mlango huyo kinda alizungumza na kituo kimoja cha radio kuwa kuna viongozi wa Simba walimfuata msimu uliopita wakimtaka kutapata kadi ya njano makusudi ili katika mchezo utakao fuata dhidi yao asicheze na kuahidiwa gari aina ya IST.

Bumbuli amesema kabla ya kwenda kwenye vyombo vya habari alipaswa kuzungumza na uongozi wa klabu kitu ambacho hakukifanya. “Ramadhani Kabwili amekosea hakupaswa kuzungumza na chombo cha habari suala kama hilo kabla ya kujadiliana na sisi kama klabu,” alisema Bumbuli.

Tayari Shirikisho la soka nchini (TFF) limetoa tamko kuwa limepeleka suala hilo kwenye vyombo husika ili ikibainika kuna aliye husika achukuliwe hatua stahiki.

#wapendasokaupdates

Klabu ya Tp Mazembe Englebert imethibitisha kumrejesha mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu

Klabu ya Tp Mazembe Englebert imethibitisha kumrejesha mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo kipindi cha nyuma

Ulimwengu ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Tanzania ambaye ana umri wa miaka 27 kwa sasa amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Tp Mazembe

Ulimwengu anaikuta Mazembe ikiwa hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kufuzu hivi karibuni, pia anaongeza idadi ya watanzania wanaocheza Mazembe kwa sasa na kuwa watatu wengine wakiwa ni Ramadhan Singano aliyetoka Azam fc na Eliud Ambokile aliyekuwa Mbeya City

All the best Thomas kuanza moja sio ujinga 🙏

#dailysporttz

KRC Genk ya imethibitisha kumsajili golikipa wa Ufaransa Thomas Didillon kutoka Anderlecht

OFFICIAL: KRC Genk ya Ubelgiji imethibitisha kumsajili golikipa wa kimataifa wa Ufaransa Thomas Didillon kutoka Anderlecht kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu

Didillon mwenye umri wa miaka 24 pia aliwahi kuzitumikia timu za vijana Ufaransa za umri wa miaka 16,18,19, 20 na 21 kwenye jumla ya michezo 21 bila kuruhusu goli

Pia aliyewahi kuchezea vilabu vya Metz, na RFC Sareing kabla hajajiunga na Anderleacht

#dailysporttz

Rasmi klabu ya JS Kabylie ya Algeria imemtangaza Zelfani Yamen kuwa kocha wao mkuu •

Rasmi klabu ya JS Kabylie ya Algeria imemtangaza aliyekuwa kocha wa klabu ya Al Merreikh raia wa Tunisia Zelfani Yamen kuwa kocha wao mkuu

Yamen anakuja kurithi mikoba ya mfaransa Hubert Velud ambaye alitangaza kuachana na klabu hiyo mapema wiki iliyopita

Yamen amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia JS Kabylie

#dailysporttz

Uwanja wa KMC kujengwa na JKT

Uongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni imeingia mkataba wa saini ya ujenzi wa uwanja wa soka wa mwenge na jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) utakaogharimu Sh.bilioni 2.7.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo jumatatu kati ya meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta na mkuu wa kikosi cha 361 cha JWTZ Luteni Kanali David Luoga katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za Manispaa hiyo zilizopo Magomeni jijini Dar es salaam.

#wapendasokaupdates

Kamata Ratiba ya Soka Leo :

👉England – EFL Cup
22:45 Aston Villa vs Leicester City
:
👉England – Championship
22:45 Blackburn Rovers vs Queens Park Rangers
22:45 Brentford vs Nottingham Forest
22:45 Cardiff City vs West Bromwich Albion
22:45 Hull City vs Huddersfield Town
22:45 Leeds United vs Millwall
22:45 Luton Town vs Derby County
22:45 Wigan Athletic vs Sheffield Wednesday
23:00 Reading vs Bristol City
:
👉Spain – Copa del Rey
23:00 Tenerife vs Athletic Bilbao
:
👉Italy – Coppa Italia
22:45 Milan vs Torino
:
👉France – Cup
20:30 ASM Belfort vs Montpellier
20:30 Angers vs Rennes
20:30 FC de Limonest vs Dijon
22:55 Monaco vs Saint-Etienne
:
👉Egypt – Premier League
20:30 Wadi Degla FC vs El Zamalek
:
Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Design a site like this with WordPress.com
Get started