Miamba ya soka As vita. Kuonekana katika kagame cup

– Miamba wa Kinshasa, klabu ya AS Vita Club, na Klabu ya DC Motema Pembe zote za DR Congo na Miamba wa Zambia Klabu ya, ZESCO United zote kwa pamoja zimethibitisha kushiriki Michuano ya CECAFA Kagame Cup; Michuano hii inatarajia kuanza kufanyika Julai 07 na Kufikia tamati Julai 21 jijini Kigali nchini Rwanda the forthcoming Cecafa Kagame Cup.
.
– Katibu Mkuu Mkongwe wa CECAFA, Nicholas Musonye Amethibitisha kuwa Maandalizi yote yanakwenda sawa kwa ajili ya Michuano hiyo ya takribani wiki mbili; Azam FC ya Tanzania ndio Bingwa mtetezi wa Kombe hili.
#Updates
@Sokawaytz

https://www.instagram.com/p/ByFjFatAxKs/?igshid=1uv5k931inc47

WALIOTAMBA KWENYE. MosimbaAward2019

Tuzo za Moo dewji
Aishi Manula ameshinda Tuzo ya Golikipa Bora wa Mwaka

Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Beki Bora wa Mwaka

James Kotei ameshinda Tuzo ya Kiungo Bora wa Mwaka

John Bocco ameshinda Tuzo ya Mshambuliaji Bora wa Mwaka

Rashid Juma ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka

Mwanahamisi Omary Shurua ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwanamke wa Mwaka Erasto Nyoni ameshinda Tuzo ya Wachezaji

Meddie Kagere ameshinda Tuzo ya Mfungaji Bora wa Mwaka

Goli la Clatous Chama dhidi ya Nkana limeshinda Tuzo ya Goli Bora la Mwaka

Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya Mo Simba 2019 ni Meddie Kagere

Tuzo ya Heshima inakwenda kwa Azim Dewji

https://www.instagram.com/p/ByGSXJTAlhd/?igshid=ysuv7rbnek12

HAZARD. KUONDOKA CHELSEA

Eden Hazard amedokeza kuwa amemaliza safari yake na klabu ya Chelsea baada ya kufunga goli mbili zilizosaidia kuizamisha Arenal jana usiku.

Chelsea imeibuka na ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Arsenal kwenye fainali ya kombe la Europa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Real Madrid na amesema kwa sasa “anasubiria klabu hizo (kukubaliana).” Kocha wake anasema anaheshimu maamuzi hayo…
📸getty

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE. AKATISHA MASOMO KWA UJAUZITO


Ni Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Welezo Halmashauri ya Shinyanga mwenye umri wa miaka 11 amekatisha masomo baada ya kukutwa na ujauzito wa miezi 7

Mwanafunzi huyo alipewa ujauzito mwaka 2018 na mwanaume ambaye hajafahamika

Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi, 2019 wanafunzi 26 wamebainika kuwa na ujauzito huku 3 kati ya hao ni wa Shule za Msingi Mkoani Shinyanga

Design a site like this with WordPress.com
Get started