UEFA kutangaza kikosi chake cha msimu. 2018/19

OFFICIAL: Shirikisho La Soka Barani Ulaya, UEFA kupitia kamata zake za Kiufundi wamechagua kikosi chao cha Wachezaji bora 20 cha msimu 2018/19 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
:
– Wachezaji sita wametoka Kikosi cha Mabingwa, Klabu ya Liverpool, kwa ujumla Wachezaji kumi na moja wametoka Ligi Kuu ya Uingereza, @premierleague.
#championsleague #UCLfinalhttps://www.instagram.com/p/ByNuxHaA4rE/?igshid=5eaiytc9bwt

Nahodha.. Gary Cahill. Kuachana na chelsea

✍🏻 OFFICIAL! Klabu ya Chelsea Imethibitisha kuwa nahodha wa Kikosi Chao, Gary Cahill ataachana na Klabu hiyo Mara Moja Baada ya Mkataba wake kufikia tamati Mwishoni mwa mwezi huu.. Cahill kaichezea The Blues Miaka Saba na Nusu.
:
✍🏻 Cahill 33, Alijiunga na Mabingwa hao wa Europa league siku ya January 16,2012 akikamilisha uhamisho wake wa £7m kutoka Klabu ya Bolton Wanderers… Akiongea Baada ya kutua Chelsea, Alisema.
🗣 “Chelsea ni klabu kubwa, ni klabu ambayo inaonekana kushinda mataji msimu na msimu na ni fursa kubwa kwangu kuwa sehemu ya hiyo misimu ya mafanikio, Fursa kama hii huwezi kuipiga chini”.
:
✍🏻 Akiitumikia Klabu ya Chelsea alianza kutwaa taji lake La kwanza msimu wake wa kwanza tu akibeba Champions league.. Kwa ujumla makombe yake akiwa na The Blues..
Premier League : 🏆🏆
FA Cup : 🏆🏆
League Cup : 🏆
UEFA Champions League :🏆
UEFA Europa League : 🏆🏆
#Updates
@Sokawaytz

https://www.instagram.com/p/ByN3dYbAunG/?igshid=vy9d4aum0ehy

UFARANSA.. KUIPIGA KIPIGO KIZITO BOLIVIAN

– Timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kushinda 2-0 dhidi ya Bolivia katika game ya kirafiki, na taarifa mbaya kwao ni majeraha ya Kylian Mbappe ambaye alilazimika kutolewa katika Mchezo huo Baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu.. Jopo La madaktari wa Ufaransa bado hawajaweka wazi Kama yupo fiti au itachukua muda gani kujiuguza na kurejea ndani ya uwanja tena.
.
– Ufaransa inajifua tayari kwa Maandalizi ya game ya kuwania kufuzu kwa EURO 2020, Ambapo watasafiri kwenda Uturuki; Ushindi wa 2-0 Bolivia katika mji wa Nantes ndio Maandalizi ya mwisho kabla ya kuwavaa Waturuki siku ya Juni 08.
.
– Kiungo, Thomas Lemar na Mshambuliaji, Antoine Griezmann walifunga mabao hayo katika Kipindi cha kwanza kwa upande wa mabingwa hao wa dunia..
#updates
@Sokawaytz

https://www.instagram.com/p/ByOPq-CgMN-/?igshid=py5oxd356wfd

HASHIM LUNGWE ATAKIWA KURIPOTI KITUO CHA POLISI KESHO


Inaelezwa kuwa Askari wa Jeshi la Polisi wamefika katika Ofisi ya Chama cha CHAUMMA na kutoa wito huo kwa kiongozi huyo

Hashim Rungwe ametakiwa kufika Kituo cha Polisi Oysterbay kesho ikiwa ni baada ya mkutano wa viongozi wa vyama 8 vya upinzani na Waandishi wa habari

Katika mkutano huo viongozi wa vyama hivyo wameweka msimamo wa pamoja wa kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio kwenye Kata 32 unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 Juni 2019

Viongozi hao wametangaza kususia kwa sababu uchaguzi huo utasimamiwa na Wakurugenzi kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu

RAISI MAGUFULI KUFANYA MKUTANO. NA WAFANYABIASHARA.. IKULU.. DAR ES SALAA.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa mwaliko wa kuhudhuria mkutano kwa wafanyabiashara wakubwa watano kutoka katika kila Wilaya za Tanzania Bara

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 7 Juni, 2019 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kikwete, Ofisi ya Rais-Ikulu Jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi

Wakuu wa Mikoa wametakiwa kuwasilisha majina ya wafanyabiashara hao wakionesha jina la mfanyabiara, aina ya biashara na namba ya simu ya mfanyabiashara

Aidha, Wakuu wa Mikoa wametakiwa kutosita kupendekeza majina ya wafanyabiashara hata kama kuna ambaye ni mtendaji wa serikali au kiongozi wa kisiasa

Vivyo hivyo, wafanyabiashara watakaohudhuria mkutano huo wameombwa kugharamia ushiriki wao

“I Will never beg. Diamond platnum for forgiveness.” Say rich mavoko

A while ago there were rumors making round that Rich Mavoko has begged for forgiveness from Diamond Platnumzz after he walked out of WCB Wasafi Classic records.

However, the bongo sensation has come out to refute the claims, stating that he can never beg anyone for forgiveness. This is what Mavoko said;

“Mimi kwa kweli nilikuwa mgeni. Nilifanya tu kuambiwa na mdogo wangu, kwanza akiwa anacheka eti ameona taarifa kuwa naomba msamaha. Nikamwambia wewe ni kama unaumwa wewe…nimeomba msamaha wapi.”

Mavoko says he was surprised to realize it was Wasafi Records themselves who were claiming he asked for forgiveness.

“Maana mdogo wangu aliponitumia link nikaona wao (Wasafi) ndo wanasema hivo. Lakini mimi sijawahi kujaribu kufanya kitu kama hicho. Niwaambie tu ndugu zangu wale waliokuwa wanategemea hicho hakiwezi kutokea.”

Just to make it clear that he NEVER and will NEVER ask Diamond Platnumz for forgiveness, he said;

“Mimi heri tu nibaki na nguo iliyochanika kuliko kuvua shati nibaki kifua wazi.”

Post Pagination

MWILI WA ETIENNE TSHISEKEDI…. WAWASILI.. ..

M


Mwili wa kiongozi wa zamani wa upinzani nchini humo, Etienne Tshisekedi umewasili kwenye Mji Mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa kutoka Ubelgiji ikiwa ni miaka miwili tokea kufariki kwake

Alifariki Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 84 mnamo Februari 2017 lakini mwili wake ulisalia huko kutokana na wasiwasi wa kisiasa wakati wa utawala wa Rais wa zamani wa Taifa hilo, Joseph Kabila

Kurejeshwa kwa mwili wake kunatimiza mojawapo ya ahadi za Mwanawe Felix Tshisekedi ambaye aliingia madarakani kama Rais wa Congo mapema mwaka huu

Kamati ya maandalizi ya mazishi inasema leo Ijumaa itakuwa ni maombolezi ya kitaifa na hapo kesho itakuwa ni sala na ibada ya wafu kabla ya mazishi jioni katia viwanja vya Mashahidi

Design a site like this with WordPress.com
Get started